Katika ulimwengu wa soka, kipa anaweza kuwa shujaa au mhanga wa lawama kwa sekunde chache tu. Goli linaweza kuwa matokeo ya shambulizi lililopangwa kwa ustadi, lakini mara nyingi, kosa la kipa linatosha kuamua hatma ya mchezo. Je, unakumbuka mechi yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo kosa la kipa lilibadili mwelekeo wa matokeo?
Kuna surprise kibao kwenye Ligi Kuu Tanzania bara ambazo tumeziona baada ya Game week mbili.
Matumizi ya washambuliaji wawili
Timu kuhamia back-four
Mawinga wenye speed
Singida Big Star
Aziz Ki vs Chama
Sikiliza episode hii kuyajua yote hayo kisha tupe maoni yako
Tangu amechukua mikoba ya kukinoa kikosi cha Chelsea, Tuchel amekuwa akihusudu mfumo wa mabeki watatu kuliko ule wa mabaki wanne ambao alikuwa akiutumia akiwa PSG.
Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadili kwa kina falsafa za raia huyo wa Ujerumani. Miongoni mwa yaliyoongelewa ni kama Tuchel anaweza badili mfumo au atasalia na wa sasa? Kitendawili cha Havertz, Werner na Lukaku bila kusahau namna anavyotegemea Wingback wakati wa kufanya mashambulizi.
Sikiliza zaidi Episode hii
Stars ya Kim ni tofauti na ya Etienne lakini kuna vitu vinaendana. Episode hii emejikita katika kuangazia falsafa za kocha Kim Poulsen anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili hayo yote bila kusahau aina ya wachezaji ambao Kim hapendi kuwakosa kwenye timu. Je ni wachezaji gani hao? Sikiliza Episode hii hadi mwisho
Tangu miaka ya 90 wapenzi wa soka walianza kushuhudia kazi za Carlo Ancelotti ambaye ni raia wa Italia. Katika miaka yake yote kama kocha ameshuhudia mabadiliko mbalimbali katika soka barani Ulaya lakini amwezaje kudumu katika taaluma hiyo kwa kipindi kirefu?
Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadiliana kuhusu falsafa, mbinu na ufundi wa kocha huyo ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Real Madrid kwa muhula wa pili.
Kuna mengi sana tusiyoyajua kuhusu Ancelotti, sikiliza episode hii kisha utupe maoni yako.
Wengi huvutiwa na soka la timu anazofundisha kama Marseille, Lille na Leeds ambayo kwa sasa imemtimua. Kuna mengi ya kujifunza juu ya falsafa ya Marcelo Bielsa na hapo ndipo kunamfanya Clifford Sangai aketi chini na Prosper Bartalomew kujadili kwa kina mbinu na ufundi wa raia huyo wa Argentina.
Tumeongelea aina yake ya ukabaji ambayo ni 'MAN TO MAN" tukiangazia kwa kina namna ilivyofaulu na kufeli hasa akiwa na Leeds United.
Prosper alienda mbali zaidi kwa kulinganisha mbinu za Bielsa dhidi ya Gian Piero Gasperini ambaye anakinioa kikosi cha Atalanta kinachoshiriki ligi kuu ya nchini Italia maarufu kama Serie A.
Sikiliza uchambuzi huu pia share na wengine zaidi.
Bila shaka ulimsikia beki wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda aliposema kwamba washambuliaji wa Simba ni rahisi kuwakaba. Je kauli hii inaukweli?
Clifford Sangai amekutana na Prosper Bartalomew chini ya mti ili kuangazia na kuchambua kwa undani mikimbio ya washambuliaji wa Simba yaani Kagere, Mugalu na Bocco
Usisite kushea na marafiki Episode hii
Pia unaweza kupakua majarida yetu BURE kuhusu AFCON:
https://sportscasttz.gumroad.com/l/stajt
https://sportscasttz.gumroad.com/l/jbxud
Hawakuanza msimu vizuri lakini hivi karibuni inaonekana kama gari limewaka.
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia wapi Arsenal walikuwa wanakwama pamoja na vitu ambavyo Mikel Arteta ameviongeza ili kuongeza ubora katika safu ya ushambuliaji.
Tumegusia pia patnership ya Xhaka na Partey inavyowasaidia katika kufanya mashambulizi.
Katika episode hii tumegusia mbinu za Mikel Arteta kwa undani zaidi, usisite kuisikiliza hadi mwisho.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Watani hawa wa jadi wametuonesha mambo mengi katika mechi mbili walizokutana, kuanzia maswala ya ufundi hadi mbinu za makocha wao na hapo ndipo Clifford Sangai anapojadiliana na Prosper Bartalomew kuhusu timu hizo.
Tumeangazia eneo moja muhimu sana kwa timu zote mbili nalo ni Safu ya Viungo ambapo kila timu imeonesha ubora na madhaifu yake na kama yanaweza kusahihishwa.
Unataka kujua madhaifu hayo basi sikiliza episode hii
Msimu mpya huu, unaona mabadiliko yoyote ndani ya kikosi cha Azam FC?
Swali hilo ndio limemfanya Clifford Sangai aketi chini pamoja na Prosper Bartalomew kujadili mambo mbalimbali hususani ya kimbinu katika kikosi cha Azam FC.
Tumeangazia namna timu inavyojilinda hadi inavyoshambulia huku tukilinganisha na msimu uliopita.
Hatujaangazia mechi za Ligi Kuu Tanzania bara tu bali michuano yote ambayo Azam FC imeshiriki.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5
Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia kwa kina wapi Ole Gunnar Solskjær alikwama kimbinu, tumezichambua kwa kina mbinu za raia huyo wa Norway kwa kuzingatia washindani wake kimbinu.
Pia tumegusia mambo ambayo kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick ameyabadili katika kikosi hicho kwa muda mfupi aliopo.
Wakati tunarekodi episode hii dili la Manchester United, Lokomotiv Moscow na Raph Ranginick limekamilika kwa asilimia kubwa hivyo unaweza ukasikiliza kumfahamu zaidi kocha huyo ikiwemo falsafa zake na yeye ni kocha wa aina gani, pia tutarajie nini kutoka kwake akiwa Manchester United.
Unataka kujua wachezaji gani watafaidika na ujio wa Ranginick? Sikiliza episode hii.
Bado unaamini Ligi Kuu Tanzania bara haina mbinu?
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mbinu za makocha mbalimbali na ufundi wa wachezaji katika Ligi Kuu ya NBC.
Je kocha wa Yanga ameshaonesha mfumo wake rasmi katika kikosi chake? Ipi ni nafasi inayomfaa Bwalya awapo uwanjani?
Hayo ni kati ya maswali tuliyojadili bila kusahau ubora wa Chirwa na Lusajo na mabadiliko ya kimfumo katika kikosi cha Namungo.
Bila shaka jina Abdul Sopu umewahi kulisikia katika story mbalimbali za michezo lakini unajua yeye ni Kiungo wa aina gani? Vipi kuhusu Ramadhan Chombo (Redondo)?
Sikiliza episode hii Prosper amechambua kwa kina mambo yote hayo.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5
Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Kila siku makocha katika vilabu mbalimbali barani Ulaya wamekuwa wakitafuta kila namna ya kuweka vikosi vyao sawa na kuhakikisha falsafa zao zinaonekana vizuri.
Ili kuhakikisha hayo yote yanatimia basi tumekuwa tukishuhudia mbinu mbalimbali za soka na hapo ndipo Clifford Sangai anapoketi na Prosper Bartalomew kuchambua timu mbalimbali pamoja na mwenendo wa timu hizo.
Tumeangazia mabadiliko aliyoyafanya Mikel Arteta katika kikosi chake cha Arsenal hali iliyopelekea yeye kuwa kocha bora wa mwezi.
Pia tumeangazia jukumu analopewa Christiano Ronaldo katika kikosi cha Manchester United bila kusahau ubora wa Napoli chini ya Spalleti.
Prosper ametufafanulia takwimu mbalimbali kama PPDA, High Turnovers, nk pamoja na umuhimu wake katika soka la kisasa.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5
Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
"Kwanini umchezeshe beki bora wa kulia duniani katika nafasi ya kiungo?" - Jürgen Klopp
Kumeibuka maswali mengi sana tangu kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate alipomtumia beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold kama kiungo katika mechi dhidi ya Andorra huku wengine wakijaribu kumfananisha beki huyo na Joshua Kimmich.
Clifford Sangai amekaa chini na Prosper Bartalomew kuchambua kwa kina utofauti uliopo baina ya wachezaji wawili, tukiangazia hasa ubora na mapungufu yao katika nafasi mbalimbali wanazocheza.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5
Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Katika mfululizo huu mpya wa episodes za 'Soka Langu', tutaongelea maswala ya mbinu na aina ya soka la wachezaji pamoja na makocha mbalimbali.
Clifford Sangai anakaa chini na Prosper Bartalomew pamoja na Francis Baraza, kocha wa timu ya Kagera Sugar kujadili aina na mbinu za soka ambazo amekuwa akizitumia.
Baraza anatupitisha katika safari yake ya ukocha tangu akiwa katika klabu ya Biashara United akitufafanulia baadhi ya maamuzi ya kiufundi aliyowahi kuyafanya.
Kocha huyo wa Kagera Sugar ametueleza kwanini anapendelea wachezaji ambao hawana majina pia amegusia matumizi ya mfumo wa 3-4-3.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5
Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09