
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia kwa kina wapi Ole Gunnar Solskjær alikwama kimbinu, tumezichambua kwa kina mbinu za raia huyo wa Norway kwa kuzingatia washindani wake kimbinu.
Pia tumegusia mambo ambayo kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick ameyabadili katika kikosi hicho kwa muda mfupi aliopo.
Wakati tunarekodi episode hii dili la Manchester United, Lokomotiv Moscow na Raph Ranginick limekamilika kwa asilimia kubwa hivyo unaweza ukasikiliza kumfahamu zaidi kocha huyo ikiwemo falsafa zake na yeye ni kocha wa aina gani, pia tutarajie nini kutoka kwake akiwa Manchester United.
Unataka kujua wachezaji gani watafaidika na ujio wa Ranginick? Sikiliza episode hii.