Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Business
Society & Culture
Health & Fitness
Sports
Technology
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Podjoint Logo
US
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts115/v4/7f/8e/f5/7f8ef5df-8d7b-3b35-7877-93f3c6daf729/mza_18328732929746753772.jpg/600x600bb.jpg
SportsCast
Clifford Sangai
62 episodes
1 week ago
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mada mbalimbali zinazohusu mpira wa miguu. Tunaangazia uwekezaji, mbinu na historia mbalimbali za Soka.
Show more...
Sports
RSS
All content for SportsCast is the property of Clifford Sangai and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mada mbalimbali zinazohusu mpira wa miguu. Tunaangazia uwekezaji, mbinu na historia mbalimbali za Soka.
Show more...
Sports
Episodes (20/62)
SportsCast
Makosa ya Makipa katika Ligi Kuu Tanzania Bara

Katika ulimwengu wa soka, kipa anaweza kuwa shujaa au mhanga wa lawama kwa sekunde chache tu. Goli linaweza kuwa matokeo ya shambulizi lililopangwa kwa ustadi, lakini mara nyingi, kosa la kipa linatosha kuamua hatma ya mchezo. Je, unakumbuka mechi yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo kosa la kipa lilibadili mwelekeo wa matokeo?


Show more...
8 months ago
47 minutes 30 seconds

SportsCast
Washambuliaji wawili, mawinga wenye kasi na namba 10

Kuna surprise kibao kwenye Ligi Kuu Tanzania bara ambazo tumeziona baada ya Game week mbili.

Matumizi ya washambuliaji wawili

Timu kuhamia back-four

Mawinga wenye speed

Singida Big Star

Aziz Ki vs Chama

Sikiliza episode hii kuyajua yote hayo kisha tupe maoni yako

 

Show more...
3 years ago
28 minutes 17 seconds

SportsCast
Chelsea ya Thomas Tuchel

Tangu amechukua mikoba ya kukinoa kikosi cha Chelsea, Tuchel amekuwa akihusudu mfumo wa mabeki watatu kuliko ule wa mabaki wanne ambao alikuwa akiutumia akiwa PSG.

Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadili kwa kina falsafa za raia huyo wa Ujerumani. Miongoni mwa yaliyoongelewa ni kama Tuchel anaweza badili mfumo au atasalia na wa sasa? Kitendawili cha Havertz, Werner na Lukaku bila kusahau namna anavyotegemea Wingback wakati wa kufanya mashambulizi.

Sikiliza zaidi Episode hii

Show more...
3 years ago
23 minutes 24 seconds

SportsCast
Mwaka mmoja wa Nabi: Mbinu na Ufundi
Ni mwaka mmoja sasa tangu Nasreddine Nabi achukue mikoba ya kukinoa kikosi cha Yanga kutoka kwa Cedric Kaze ambaye kwa sasa ni msaidizi wake. Kuna mambo mengi ameyabadili katika kikosi hicho ambayo Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanayajadili katika episode hii. Kati ya hayo ni kumfanya kiungo Feisal Salum kucheza katika eneo la mbele zaidi kuliko alipokuwa akicheza hapo awali. Swala la muhimu zaidi ni nafasi ambayo wachezaji vijana waliopo Yanga wanapewa nafasi na Nabi. Sikiliza episode hii kisha tupe maoni yako.
Show more...
3 years ago
24 minutes 22 seconds

SportsCast
Taifa Stars ya Kim Poulsen

Stars ya Kim ni tofauti na ya Etienne lakini kuna vitu vinaendana. Episode hii emejikita katika kuangazia falsafa za kocha Kim Poulsen anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'


Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili hayo yote bila kusahau aina ya wachezaji ambao Kim hapendi kuwakosa kwenye timu. Je ni wachezaji gani hao? Sikiliza Episode hii hadi mwisho

Show more...
3 years ago
16 minutes 33 seconds

SportsCast
Je, Carlo Ancelottii amebadilika?

Tangu miaka ya 90 wapenzi wa soka walianza kushuhudia kazi za Carlo Ancelotti ambaye ni raia wa Italia. Katika miaka yake yote kama kocha ameshuhudia mabadiliko mbalimbali katika soka barani Ulaya lakini amwezaje kudumu katika taaluma hiyo kwa kipindi kirefu?

Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadiliana kuhusu falsafa, mbinu na ufundi wa kocha huyo ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Real Madrid kwa muhula wa pili.

Kuna mengi sana tusiyoyajua kuhusu Ancelotti, sikiliza episode hii kisha utupe maoni yako.

Show more...
3 years ago
15 minutes 21 seconds

SportsCast
Falsafa ya Marcelo Bielsa

Wengi huvutiwa na soka la timu anazofundisha kama Marseille, Lille na Leeds ambayo kwa sasa imemtimua. Kuna mengi ya kujifunza juu ya falsafa ya Marcelo Bielsa na hapo ndipo kunamfanya Clifford Sangai aketi chini na Prosper Bartalomew kujadili kwa kina mbinu na ufundi wa raia huyo wa Argentina.

Tumeongelea aina yake ya ukabaji ambayo ni 'MAN TO MAN" tukiangazia kwa kina namna ilivyofaulu na kufeli hasa akiwa na Leeds United.

Prosper alienda mbali zaidi kwa kulinganisha mbinu za Bielsa dhidi ya Gian Piero Gasperini ambaye anakinioa kikosi cha Atalanta kinachoshiriki ligi kuu ya nchini Italia maarufu kama Serie A.

Sikiliza uchambuzi huu pia share na wengine zaidi.

Show more...
3 years ago
15 minutes 51 seconds

SportsCast
Kwanini kiwango cha Lukaku kimeshuka?
Tangu Lukaku afanye mahojiano na Sky sports, amecheza mechi sita za Ligi Kuu bila kufunga bao. Clifford Sangai ameamua kukaa chini na Prosper Bartalomew kuangalia mwenendo wa mshambuliaji huyo wa Chelsea ambaye msimu uliopita alifunga mabao 24 na assists 11 akiwa na klabu ya Inter. Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni mifumo ya Chelsea, Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji. Prosper ameenda mbali zaidi kwa kuangalia aina ya pasi ambazo Lukaku anapokea pia maeneo anayokaa ili kupokea pasi. Episode hii imeelezea kila kitu kuhusu Romelu Lukaku.
Show more...
3 years ago
13 minutes 9 seconds

SportsCast
Mikimbio ya Washambuliaji wa Simba SC

Bila shaka ulimsikia beki wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda aliposema kwamba washambuliaji wa Simba ni rahisi kuwakaba. Je kauli hii inaukweli?

Clifford Sangai amekutana na Prosper Bartalomew chini ya mti ili kuangazia na kuchambua kwa undani mikimbio ya washambuliaji wa Simba yaani Kagere, Mugalu na Bocco

Usisite kushea na marafiki Episode hii

Pia unaweza kupakua majarida yetu BURE kuhusu AFCON:

https://sportscasttz.gumroad.com/l/stajt

https://sportscasttz.gumroad.com/l/jbxud

Show more...
3 years ago
16 minutes 55 seconds

SportsCast
Arsenal: 'Pattern' ya ushambuliaji

Hawakuanza msimu vizuri lakini hivi karibuni inaonekana kama gari limewaka. 

Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia wapi Arsenal walikuwa wanakwama pamoja na vitu ambavyo Mikel Arteta ameviongeza ili kuongeza ubora katika safu ya ushambuliaji. 

Tumegusia pia patnership ya Xhaka na Partey inavyowasaidia katika kufanya mashambulizi.

Katika episode hii tumegusia mbinu za Mikel Arteta kwa undani zaidi, usisite kuisikiliza hadi mwisho.

Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09

Show more...
3 years ago
19 minutes 48 seconds

SportsCast
Kufeli na kufaulu kwa Viungo wa Simba na Yanga

Watani hawa wa jadi wametuonesha mambo mengi katika mechi mbili walizokutana, kuanzia maswala ya ufundi hadi mbinu za makocha wao na hapo ndipo Clifford Sangai anapojadiliana na Prosper Bartalomew kuhusu timu hizo.

Tumeangazia eneo moja muhimu sana kwa timu zote mbili nalo ni Safu ya Viungo ambapo kila timu imeonesha ubora na madhaifu yake na kama yanaweza kusahihishwa.

Unataka kujua madhaifu hayo basi sikiliza episode hii

Show more...
3 years ago
21 minutes 27 seconds

SportsCast
Azam FC: Msimu mpya mambo yale yale


Msimu mpya huu, unaona mabadiliko yoyote ndani ya kikosi cha Azam FC?


Swali hilo ndio limemfanya Clifford Sangai aketi chini pamoja na Prosper Bartalomew kujadili mambo mbalimbali hususani ya kimbinu katika kikosi cha Azam FC.


Tumeangazia namna timu inavyojilinda hadi inavyoshambulia huku tukilinganisha na msimu uliopita.


Hatujaangazia mechi za Ligi Kuu Tanzania bara tu bali michuano yote ambayo Azam FC imeshiriki.


Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5

Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09

Show more...
3 years ago
22 minutes 56 seconds

SportsCast
Manchester United Special

Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia kwa kina wapi Ole Gunnar Solskjær alikwama kimbinu, tumezichambua kwa kina mbinu za raia huyo wa Norway kwa kuzingatia washindani wake kimbinu.

Pia tumegusia mambo ambayo kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick ameyabadili katika kikosi hicho kwa muda mfupi aliopo.

Wakati tunarekodi episode hii dili la Manchester United, Lokomotiv Moscow na Raph Ranginick limekamilika kwa asilimia kubwa hivyo unaweza ukasikiliza kumfahamu zaidi kocha huyo ikiwemo falsafa zake na yeye ni kocha wa aina gani, pia tutarajie nini kutoka kwake akiwa Manchester United.

Unataka kujua wachezaji gani watafaidika na ujio wa Ranginick? Sikiliza episode hii.

Show more...
3 years ago
37 minutes 50 seconds

SportsCast
Ligi Kuu Tanzania Bara: Mbinu na Ufundi Part 2
Huu ni mwendelezo wa pale tulipoishia katika episode iliyopita lakini mwendelezo huu ni wa kipekee zaidi. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuchambua mbinu na ufundi katika Ligi Kuu Tanzania Bara maarudu kama NBC Premiere League. Tumeangazia mwenendo wa timu nyingi zinapokutana na Yanga zimekuwa zikijaza wachezaji wengi katika eneo la kiungo (Midfield overload) je kuna faida yoyote inayotakana na mbinu hiyo? Kibwana Shomari ameanza kuonesha mabadiliko makubwa sana katika matumizi ya mguu wake wa kushoto, Prosper amechambua style ya uchezaji wake na namna alivyokuwa hatari dhidi ya wapinzani wake. Ibrahim Ajibu Migomba anaweza pata nafasi ya kudumu katika kikosi cha Simba kwa sasa? Sikiliza episode hii kisha utupe maoni yako. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Show more...
3 years ago
30 minutes 17 seconds

SportsCast
Ligi Kuu Tanzania Bara: Mbinu na Ufundi Part 1

Bado unaamini Ligi Kuu Tanzania bara haina mbinu?


Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mbinu za makocha mbalimbali na ufundi wa wachezaji katika Ligi Kuu ya NBC.


Je kocha wa Yanga ameshaonesha mfumo wake rasmi katika kikosi chake? Ipi ni nafasi inayomfaa Bwalya awapo uwanjani?


Hayo ni kati ya maswali tuliyojadili bila kusahau ubora wa Chirwa na Lusajo na mabadiliko ya kimfumo katika kikosi cha Namungo.


Bila shaka jina Abdul Sopu umewahi kulisikia katika story mbalimbali za michezo lakini unajua yeye ni Kiungo wa aina gani? Vipi kuhusu Ramadhan Chombo (Redondo)?


Sikiliza episode hii Prosper amechambua kwa kina mambo yote hayo.


Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5

Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09

Show more...
4 years ago
37 minutes

SportsCast
Mbinu zilizotrend katika ligi tano bora barani Ulaya. Part 2

Kila siku makocha katika vilabu mbalimbali barani Ulaya wamekuwa wakitafuta kila namna ya kuweka vikosi vyao sawa na kuhakikisha falsafa zao zinaonekana vizuri.

Ili kuhakikisha hayo yote yanatimia basi tumekuwa tukishuhudia mbinu mbalimbali za soka na hapo ndipo Clifford Sangai anapoketi na Prosper Bartalomew kuchambua timu mbalimbali pamoja na mwenendo wa timu hizo.

Tumeangazia mabadiliko aliyoyafanya Mikel Arteta katika kikosi chake cha Arsenal hali iliyopelekea yeye kuwa kocha bora wa mwezi.

Pia tumeangazia jukumu analopewa Christiano Ronaldo katika kikosi cha Manchester United bila kusahau ubora wa Napoli chini ya Spalleti.

Prosper ametufafanulia takwimu mbalimbali kama PPDA, High Turnovers, nk pamoja na umuhimu wake katika soka la kisasa.

Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5

Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09

Show more...
4 years ago
38 minutes 18 seconds

SportsCast
Martin Ødegaard ni suluhu kwa matatizo ya Arsenal?
Tuliwahi kuongelea kuhusu kukosekana kwa kiungo mshambuliaji katika kikosi cha Arsenal kwenye Podcast hii. Sasa Arsenal chini ya Arteta imemsajili kiungo Martin Ødegaard kutoka Real Madrid. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kama Ødegaard ataleta ahueni katika eneo la kiungo mshambuliaji. Ødegaard aliweza kuwashawishi mashabiki kipindi yupo kwa mkopo? Takwimu zake zinasemaje klabuni hapo? Je ni chaguo muhimu kwa Arsenal?. Basi sikiliza episode hii. Tumeangazia pia kama Mikel Arteta anaweza kutumia tena mfumo wa 3-4-3 ambao ulimpa mafanikio kipindi anaichukua timu. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Show more...
4 years ago
23 minutes 41 seconds

SportsCast
Tofauti ya Joshua Kimmich na Trent Alexander-Arnold

"Kwanini umchezeshe beki bora wa kulia duniani katika nafasi ya kiungo?" - Jürgen Klopp

Kumeibuka maswali mengi sana tangu kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate alipomtumia beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold kama kiungo katika mechi dhidi ya Andorra huku wengine wakijaribu kumfananisha beki huyo na Joshua Kimmich.

Clifford Sangai amekaa chini na Prosper Bartalomew kuchambua kwa kina utofauti uliopo baina ya wachezaji wawili, tukiangazia hasa ubora na mapungufu yao katika nafasi mbalimbali wanazocheza.

Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5

Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09


Show more...
4 years ago
17 minutes 34 seconds

SportsCast
Soka Langu: Francis Baraza

Katika mfululizo huu mpya wa episodes za 'Soka Langu', tutaongelea maswala ya mbinu na aina ya soka la wachezaji pamoja na makocha mbalimbali.

Clifford Sangai anakaa chini na Prosper Bartalomew pamoja na Francis Baraza, kocha wa timu ya Kagera Sugar kujadili aina na mbinu za soka ambazo amekuwa akizitumia.

Baraza anatupitisha katika safari yake ya ukocha tangu akiwa katika klabu ya Biashara United akitufafanulia baadhi ya maamuzi ya kiufundi aliyowahi kuyafanya.

Kocha huyo wa Kagera Sugar ametueleza kwanini anapendelea wachezaji ambao hawana majina pia amegusia matumizi ya mfumo wa 3-4-3.

Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5

Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09

Show more...
4 years ago
49 minutes 5 seconds

SportsCast
Mbinu zilizotrend katika ligi tano bora barani Ulaya. Part 1
SportsCast imekuandalia uchambuzi wa ligi kuu tano bora barani ulaya tukiangazia hasa mechi za awali kabla ya mapumziko kwa ajili ya timu za taifa (International Break) Kama kawaida Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kudadavua mbinu za makocha mbalimbali na Wachezaji walioonesha viwango katika hatua za awali. Tumegusia mbinu ya Manchester city ilivyofeli katika mechi za mwanzoni kabisa msimu huu. Pia tumeangalia kikosi cha Real Madrid chini ya Carlo Ancelloti kama kuna mabadiliko yoyote. Pia Prosper ametaja orodha ya makocha wanaopaswa kuangaliwa kwa umakini katika Ligi Kuu nchini Ufaransa, pia ameelezea ubora wa Jose Mourinho na Julian Naglesmann. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
Show more...
4 years ago
41 minutes

SportsCast
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mada mbalimbali zinazohusu mpira wa miguu. Tunaangazia uwekezaji, mbinu na historia mbalimbali za Soka.