
Katika mfululizo huu mpya wa episodes za 'Soka Langu', tutaongelea maswala ya mbinu na aina ya soka la wachezaji pamoja na makocha mbalimbali.
Clifford Sangai anakaa chini na Prosper Bartalomew pamoja na Francis Baraza, kocha wa timu ya Kagera Sugar kujadili aina na mbinu za soka ambazo amekuwa akizitumia.
Baraza anatupitisha katika safari yake ya ukocha tangu akiwa katika klabu ya Biashara United akitufafanulia baadhi ya maamuzi ya kiufundi aliyowahi kuyafanya.
Kocha huyo wa Kagera Sugar ametueleza kwanini anapendelea wachezaji ambao hawana majina pia amegusia matumizi ya mfumo wa 3-4-3.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5
Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09