
Kila siku makocha katika vilabu mbalimbali barani Ulaya wamekuwa wakitafuta kila namna ya kuweka vikosi vyao sawa na kuhakikisha falsafa zao zinaonekana vizuri.
Ili kuhakikisha hayo yote yanatimia basi tumekuwa tukishuhudia mbinu mbalimbali za soka na hapo ndipo Clifford Sangai anapoketi na Prosper Bartalomew kuchambua timu mbalimbali pamoja na mwenendo wa timu hizo.
Tumeangazia mabadiliko aliyoyafanya Mikel Arteta katika kikosi chake cha Arsenal hali iliyopelekea yeye kuwa kocha bora wa mwezi.
Pia tumeangazia jukumu analopewa Christiano Ronaldo katika kikosi cha Manchester United bila kusahau ubora wa Napoli chini ya Spalleti.
Prosper ametufafanulia takwimu mbalimbali kama PPDA, High Turnovers, nk pamoja na umuhimu wake katika soka la kisasa.
Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5
Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09