Home
Categories
EXPLORE
Society & Culture
Comedy
Business
Education
News
Music
Sports
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
Loading...
0:00 / 0:00
Podjoint Logo
IL
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts125/v4/0e/44/af/0e44af17-fc29-ac16-6ba9-db2bf25c4dca/mza_12684382132760653712.jpg/600x600bb.jpg
Nukta the Podcast
Nukta Habari
71 episodes
6 days ago
Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.
Show more...
Entertainment News
News
RSS
All content for Nukta the Podcast is the property of Nukta Habari and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.
Show more...
Entertainment News
News
Episodes (20/71)
Nukta the Podcast
VITA YA MAJI ILIVYOLETA UMOJA KATI YA WAFUGAJI NA WAKULIMA MOROGORO

Katika episode hii tutaangazia jinsi tatizo la maji Ilivyowaunganisha wakulima na wafugaji Kilosa.

Hapa utasikia simulizi ya wafugaji na wakulima waliokuwa maadui kutokana na mgogoro wa maji walivyogeuka marafiki baada ya kumfahamu adui wao wa kweli.

Kama nilivyoeleza katika episode ya kwanza mimi na producer wangu tulipata wasaa wa kuzunguka baadhi ya vijiji vya wilaya za Kilombero, Kilosa na Morogoro mjini kuona mwenendo wa utunzaji wa vyanzo vya maji, mienenendo ya migogoro inayohusiana na rasilimali maji na malisho na hatua zilizofikiwa hadi sasa.  Karibu twende nami mpaka mwisho wa episode hii. 


Show more...
2 months ago
23 minutes 52 seconds

Nukta the Podcast
HATARI INAYOUKABILI MTO NGERENGERE

Hujambo msikilizaji wa Nukta the Podcast, karibu katika mfululizo wa episode zetu maalumu zinazoangazia Usimamizi wa rasilimali maji pamoja na mazingira katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. 

Katika sehemu hii tutamulika hatari inayoukabili Mto Ngerengere uliopo mkoani Morogoro kutokana na uchafuzi unaofanywa wa mto huo.

Pia tutachambua hatua zilizochukuliwa na zinazotakiwa kuchukuliwa ili kuunusuru mto huo unaopita Morogoro mjini.

Mimi ni Esau Ezra Ng’umbi kwa niaba ya mtayarishaji wa makala hii Daniel Samson, pamoja na mhariri wetu, Nuzulack Dausen, ninakukaribisha kuungana nami mpaka tamati.


Show more...
2 months ago
21 minutes 3 seconds

Nukta the Podcast
Wafahamu watu 10 tajiri zaidi duniani 2025

Ukuaji wa teknolojia umeendelea kuchochea ongezeko la utajiri duniani jambo ambalo limesababisha watu waliowekeza katika sekta hiyo kuendelea kujikusanyia ukwasi na kutawala orodha ya watu wenye ukwasi mwingi zaidi duniani.

Orodha ya watu matajiri duniani ya mwaka 2025 inayotolewa na Jarida la Forbes la nchini Marekani inaonesha chanzo cha utajiri wa watu 10 matajiri zaidi ni uwekezaji katika teknolojia na biashara.

Kwa mujibu Forbes duniani kuna zaidi ya mabilionea 2,700 wakiwa na jumla ya utajiri wa Dola Trilioni 14.2 za Marekani wakitokea katika sekta mbalimbali kama teknolojia, biashara, na huduma za kifedha na makala hii inaangazia watu 10 tajiri zaidi.

Show more...
4 months ago
10 minutes 40 seconds

Nukta the Podcast
VITA YA MAJI ILIVYOLETA AMANI NA MSHIKAMANO KATI YA WAFUGAJI NA WAKULIMA KILOSA

Katika episode hii tutaangazia jinsi tatizo la maji Ilivyowaunganisha wakulima na wafugaji Kilosa.

Hapa utasikia simulizi ya wafugaji na wakulima waliokuwa maadui kutokana na mgogoro wa maji walivyogeuka marafiki baada ya kumfahamu adui wao wa kweli.

Karibu twende nami mpaka mwisho wa episode hii.

Show more...
10 months ago
23 minutes 57 seconds

Nukta the Podcast
SCRAMBLE FOR WATER RESOURCES

This is the part of the three episodes that we have produced after visiting several districts in Morogoro region, eastern Tanzania meeting with farmers, livestock keepers, environmentalists, factory owners and government officials. 

In this first episode we will hear about how pastoralists fight for water resources in Eastern Tanzania due to the increase in demand of water amid ongoing decline of water levels in their localities, highly  influenced by climate change. You are warmly welcome. 


Show more...
10 months ago
19 minutes 31 seconds

Nukta the Podcast
Restoration of Lake Manyara Tilapia remains an uphill duty

Join Daniel Samson to explore in detail about endangered Manyara Tilapia in Lake Manyara.

Stocks of Manyara tilapias have plummeted to alarmingly low levels in recent decades due to unsustainable fishing. 

The International Union for Conservation of Nature (IUCN) Red List of Threatened Species Report 2006 shows that the area of occurrence of the fish, which previously accounted for 73.6% of the total catch in the region, has shrunk from 5,000 km2 to 1800 km2 in recent decades.

As a result, the fish is now listed as an endangered species by the IUCN because of driving forces, including overfishing and pollution.

The fish can only be found in the soda lakes of north-central Tanzania: Lakes Manyara, Kitangiri, Singida, Kindai, and Sulunga. 

Researchers argue that 20 years have passed since the last estimation of fish caught from Lake Manyara. The current stock of Tilapia in the lake is unknown.

The lake's proximity to villages, including Barabarani, Migombani, Majengo, and Oltukai, has led to an overdependence on its resources, with many locals relying on fishing for daily sustenance. 

Using illegal nets to maximize catches has further exacerbated the problem, significantly reducing fish populations and shifting towards smaller-sized fish.


Show more...
1 year ago
10 minutes 59 seconds

Nukta the Podcast
From sunlight to harvest: How solar energy brings hopes to farmers in Iringa

For decades, farmers in Lupembe Lwa Senga village in Iringa region had relied on the traditional farming system for their livelihoods. Apart from using hand hoes, animal plows, they would wait for the rain to irrigate their crops.  

For small plots like gardens, they would use buckets or recently fuel-powered water pumps for irrigation. 

“We started irrigation farming as a group in1999, by that time we were using a fuel-powered pump with the cost of 200,000 for buying petrol to irrigate all five acres a day, it was terrible,” Gabriel Mmewa, farmer in Lupembe Lwa Senga said. .

With outdated oil pump machines driving the irrigation process, he said the cost of production soared, leaving the farmers trapped in a cycle of diminishing returns.

However, as the demands of a growing population and the uncertainties of rains, the need for innovation became apparent.

Show more...
1 year ago
7 minutes 51 seconds

Nukta the Podcast
UPUNGUFU WA WALIMU SHULE YA MSINGI UNAVYOATHIRI ELIMU TANZANIA

Wakati watahiniwa zaidi ya milioni moja wa elimu ya msingi Tanzania Bara wakiwa wanasubiri hatma yao, baada ya kumaliza mitihani yao jana Septemba 14, 2023, utoshelevu wa walimu katika ngazi hiyo muhimu ya elimu kwa shule za Serikali umeendelea kuwa kitendawili

Kitabu cha hali ya uchumi cha mwaka 2022, kinabainisha kuwa mpaka Disemba mwaka 2022 kulikuwa na jumla ya wanafunzi milioni 10.8 katika shule za msingi za Serikali Tanzania, huku idadi ya walimu katika shule za Serikali ikiwa 173,276.

Hii ni sawa na kusema idadi ya wanafunzi waliopo ni mara 62 zaidi ya idadi ya walimu na hivyo kwa wastani mwalimu mmoja hufundisha darasa lenye wanafunzi 63 kwa wakati mmoja uwiano ambao uko juu ya kiwango kinachotakiwa cha wanafunzi 45 kwa darasa.

Aidha, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inataja Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma kuwa ndio wilaya ambayo mwalimu mmoja hufundisha darasa lenye wanafunzi wengi zaidi wanaofika 103.

Wilaya ya Muleba iliyopo mkoani Kagera ndiyo wilaya pekee iliyofanikiwa kufikia uwiano stahiki kwa wanafunzi 45 kufundishwa na mwalimu mmoja kwa darasa mwaka 2021.

Wadau wa elimu nchini Tanzania, wanatoa maoni yao juu ya namna upungufu wa walimu shule za msingi unavyoathiri sekta ya elimu nchini.

Karibu.

Show more...
1 year ago
9 minutes 34 seconds

Nukta the Podcast
Elimu ya Veta inavyowainua walemavu wa akili Tanzania

Awali, ilikuwa ni vigumu kushuhudia watu wanaozaliwa na ulemavu wakipata huduma muhimu wanazozihitaji kama elimu, afya, pamoja na kushirikiana na wanajamii wengine kuibua suluhu za matatizo yanayozikabili jamii zao.

Hivi sasa zama hizo zimepita. Kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali pamoja na wadau, ikiwemo kuielimisha jamii kutowabagua na kushirikiana na kundi hilo, kama binadamu wengine watu wenye ulemavu nao wanapata huduma wanazostahili.

Miongoni mwao ni kijana Paulo Ngunyali, mhitimu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kilichopo Chang’ombe, Jijini Dar es Salaam. Pamoja kuwa mlemavu wa akili amehitimu fani ya uundaji wa mashine, na sasa ni mwalimu msaidizi katika kitengo cha watu wenye mahitaji maalumu.

Katika maonesho ya kimataifa ya kibiashara maarufu kama Saba Saba, Paulo (32), amekuwa kivutio cha wengi kutokana na namna anavyoelezea kwa ufasaha jinsi mashine ya kupima uwezo wa kufundishaa  watu wenye ulemavu wa akili inavyofanya kazi.

Show more...
1 year ago
8 minutes

Nukta the Podcast
MFAHAMU MBUNIFU WA MAJIKO YANAYOTUMIA MAWE TANZANIA

Nishati ya kupikia ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya binadamu duniani kote, hiyo ndio huwezesha mapishi ya aina mbalimbali za vyakula tunavyokula ili kuimarisha afya na kuwezesha utendaji wa shughuli za kila siku.

Watu wengi wanatambua gesi, mkaa, umeme, mafuta pamoja na kuni kama ndio vyanzo vya nishati ya kupikia kwa kuwa ndio ambavyo vinatumika kwa kiasi kikubwa kwa sasa huku jitihada nyingi zikielekezwa kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Hata hivyo, jijini Dar es Salaam kuna ubunifu mpya wa nishati ya kupikia inayotumia mawe, ambapo inatajwa kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kupikia kwa gesi, umeme, mkaa au nishati nyingine.

Ndiyo! Ubunifu, udadisi pamoja na uthubutu umewezesha ugunduzi huu ambapo sasa mawe yanayopatikana kwa urahisi katika maeneo mengi nchini Tanzania yanaweza kutumika kama chanzo cha nishati ya kupikia.

Raymond James (25) maarufu kama Mr Majiko, ndiye mbunifu wa majiko hayo yanayotumia mawe, umeme kidogo pamoja na chenga za mkaa mbadala zinazotokana na vifuu vya nazi.

Kijana huyo mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, ameiambia Nukta Habari kuwa kukosa ajira ndio sababu kubwa iliyommchochea kubuni majiko hayo ili aweze kujiingizia kipato kitakachomuwezesha kuendesha maisha.

Katika podcast hii, amezungumza mengi. karibu kumsikiliza

Show more...
1 year ago
7 minutes 41 seconds

Nukta the Podcast
JINSI MATAPELI WANAVYOTUMIA TAASISI YA MO FOUNDATION KUIBIA WATU

 Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Facebook huenda umewahi kukutana na chapisho linalohusu fursa ya mikopo kutoka kwenye taasisi ya mfanyabiashara bilionea nchini Tanzania Mohamed Dewji Foundation

Sehemu ya chapisho hilo lianasomeka ‘𝐉𝐈𝐏𝐀𝐓𝐈𝐄 𝐌𝐊𝐎𝐏𝐎 𝐊𝐔𝐓𝐎𝐊𝐀 𝐌𝐎𝐇𝐀𝐌𝐄𝐃 𝐃𝐄𝐖𝐉𝐈 𝐅𝐎𝐔𝐍𝐃𝐀𝐓𝐈𝐎𝐍 kwa maelekezo ya kupata vigezo na masharti njoo hwatspp kwa no👉🏿 0748923136’.

Chapisho hilo pamoja na kuhamasisha watu kuomba mikopo wametaja kigezo cha kutoa kwanza kiasi cha hisa ya mkopo unaotaka kupewa kabla ya kupata mkopo wenyewe.

Ufafanuzi zaidi wa taarifa hiyo unaonesha kama unahitaji kukopa Sh100,000 basi utalazimika kutoa kwanza hisa ya Sh22,000 ndipo upewe mkopo huo.

Taarifa hiyo imesambaa katika mtandao wa Facebook kupitia akaunti zenye majina tofauti tofauti toka mwaka 2022  huku ikiwa imeambatanishwa na  video fupi inayomnukuu Mohamed Dewji kuwa anatoa mikopo.

Hata hivyo, Habari hiyo haina ukweli wowote kwa kuwa ni habari za uzushi zinazotumiwa na matapeli kuwalaghai wananchi na kujipatia vipato kwa njia zisizo halali. 

Nukta Fakti imefanya utafiti ili kubaini ukweli wa akaunti hizo za mtandao wa Facebook na kugundua kuwa akaunti hizo hazina uhusiano wowote na Mohamed Dewji mwenyewe au taasisi yake ya Mohamed Dewji Foundation.

Akaunti sahihi ya Facebook ya mfanyabiashara huyo maarufu nchini ni Mohammed Dewji huku ile ya taasisi yake ni Mo Dewji Foundation na sio Mikopo Tanzania kama inavyojitambulisha akaunti hiyo inayodai kutoa mikopo.

Mohamed Dewji hatoi mikopo

Utafiti zaidi uliofanywa na Nukta Fakti umebaini kuwa, si Mohamed Dewji mwenyewe wala taasisi yake ambayo inajihusisha na utoaji wa mikopo kwa namna yoyote ile.

Kupitia mtandao wa Linkedin Mohamed Dewji amewahi kutoa taarifa kwa umma akifafanua kuwa taasisi yake inajihusisha zaidi kutoa misaada ya kielimu kwa kufadhili masomo, upatikanaji wa maji pamoja na kutatua changamoto katika sekta ya afya.

Show more...
1 year ago
7 minutes 29 seconds

Nukta the Podcast
KWA NINI BANGI INALIMWA ZAIDI TANZANIA LICHA YA OPARESHENI KALI ZA DAWA ZA KULEVYA?

Mapema Agosti mwaka huu Serikali ya Tanzania ilitangaza kukamata magunia 131 ya bangi, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketeza jumla ya hekari 489 za mashamba ya bangi mkoani Morogoro, katika moja ya operesheni kubwa za kutokomeza dawa za kulevya iliyowahi kufanyika nchini. 

Katika operesheni hiyo Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo anasema wakulima hao wa bangi hufanya uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kuchepusha maji pamoja na kukata misitu ili kufanya kilimo cha zao hilo haramu.

Watu 18 walikamatwa katika operesheni hiyo iliyoshika mjadala katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya mamlaka hiyo kueleza kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakifanya kilimo katika mazingira ambayo si rahisi kufikika. 

Hili ni miongoni mwa matukio makubwa ya kudhibiti dawa za kulevya ndani ya miaka mitano, jambo linaloashiria kuwa washirika wa dawa hizo hatari kwa afya ya binadamu wanaendelea kuzalisha licha ya jitihada za Serikali na wadau kuzidhibiti.

Mwaka 2021 tani 22.74 za bangi zilikamatwa nchini Tanzania ikiwa ni ongezeko la asilimia 72 ya kiasi kilichokamatwa mwaka 2020.

Aidha, takwimu za uhalifu nchini zilizopo katika kitabu cha hali ya uchumi mwaka 2022 kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonesha mashamba ya bangi yameongezeka takriban mara mbili ndani ya miaka minne kutoka 49 mwaka 2018 hadi kufikia mashamba 87 mwaka 2022.

Show more...
1 year ago
9 minutes 12 seconds

Nukta the Podcast
Teknolojia ya vifuu vya nazi itakavyo waokoa wachimbaji na madhara ya zebaki

Huenda wachimbaji wadogo wa madini Tanzania wakaepukana na athari za afya pamoja na uchafuzi wa mazingira ikiwa wataasili matumizi ya bidhaa mpya ya kusafishia madini (Activated carbon) inayozalishwa nchini.

Bidhaa hiyo inayotengenezwa kwa kutumia vifuu vya nazi itachochea uzalishaji wa madini na kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la taifa  kwa kuwa itapatikana kwa urahisi jambo litakaloongeza kasi katika shughuli za uchenjuaji huku mazingira na wachimbaji wakwa salama.

Upatikanaji wa bidhaa hiyo mbadala wa zebaki katika shughuli za uchechuaji itakuwa mkombozi kwa wachimbaji pamoja na jamii ambayo inaweza kuathirika kwa kwa kuvuta hewa, kula chakula au maji yaliyo na sumu ya zebaki.

Shirika la Afya Duniani (WHO), linabainisha kuwa athari za kiafya zitokanazo na zebaki ni pamoja na kuharibiwa kwa mifumo ya neva, kuharibiwa kwa mfumo wa upumuaji, mmeng’enyo, mifumo ya kinga, figo, mapafu na wakati mwingine husababisha kifo.

WHO wamesisitiza kuwa sumu hiyo inaweza kusababisha magonjwa katika mfumo wa fahamu ikiwemo kifafa, kupoteza uwezo wa kuona au kusikia, udumavu pamoja na kupoteza kumbukumbu

Mpango Kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki 2020/25 unabainisha kuwa zebaki ni miongoni mwa kemikali hatarishi inayosababisha athari kwa afya ya binadamu na mazingira duniani

Show more...
2 years ago
7 minutes 7 seconds

Nukta the Podcast
Hizi ndio hifadhi tano kubwa za Taifa, Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yamebarikiwa vivutio vingi vya utalii ambavyo sio tu vinapendezesha nchi bali ni chanzo kizuri cha mapato hususani fedha za kigeni ambazo hutumika kwa shughuli za maendeleo.

Tovuti ya runinga ya Tanzania Safari Channel ambayo hutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, inabainisha kuwa Asilimia 40 ya ardhi ya Tanzania imetengwa kwa ajili ya uhifadhi.

Hii inajumuisha hifadhi za Taifa 22, eneo la hifadhi ya Ngorongoro, mapori tengefu, hifadhi za misitu asilia na misitu ya kupandwa, maeneo ya kihistoria pamoja na hifadhi za bahari.

Maeneo yote hayo ndio kitovu kikubwa cha utalii nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa kitabu cha hali ya uchumi kwa mwaka 2022, kinachotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) hifadhi za taifa ni moja kati ya vivutio vilivyotembelewa zaidi na watalii wa ndani na nje ya nchi.

Mwaka 2022 hifadhi hizo zilitembelewa na jumla ya watalii milioni 1.4 kati yao watalii 787,742 walitoka ndani ya nchi na watalii 697,264 kutoka mataifa mengine yaliyopo nje ya  nchi.

Huenda wewe ni miongoni mwa watu wanaofahamu kuhusu uwepo wa hifadhi hizi lakini hujui ni ipi inaongoza kwa ukubwa, inapatikana wapi, na gharama za kufika huko.

Makala hii imeorodhesha hifadhi tano ambazo ndio kubwa zaidi nchini Tanzania pamoja na aina ya vivutio utakavyokutana navyo.

Show more...
2 years ago
7 minutes 10 seconds

Nukta the Podcast
MVUVI MPAMBANAJI NDANI YA ZIWA VICTORIA

Ziwa Victoria ni moja ya maziwa makuu ya Afrika Mashariki. Ni ziwa ambalo lipo kwenye mstari wa ikweta na limezungukwa na nchi tatu zilizopo Afrika Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda.

Ziwa hili ni chanzo cha Mto Nile wenye urefu wa kilomita 6,650 na urefu huo unaufanya kuwa mto mrefu zaidi duniani, Ziwa Victoria ndiyo ziwa kubwa zaidi barani Afrika na lina ukubwa wa kilomita za mraba 68,800 ambapo ni la pili duniani kwa ukubwa likitanguliwa na Ziwa Superior lililopo Amerika ya kaskazini, kwa ukubwa huu nchi za Rwanda na Burundi zinaweza kuwa visiwa ndani ya ziwa hili.

Ziwa hili linahudumia wakazi takribani milioni 40 wa Afrika Mashariki kupitia shughuli za uvuvi, utalii na usafirishaji ambazo hufanyika kila siku, miongoni mwa wanaotegemea ziwa hili katika shughuli zao za kila siku ni Mwajuma Chamuriho, mwanamama huyu amejiajiri na ametengeneza ajira zaidi ya 50 owa watu wengine kupitiz Ziwa Victoria.

lakini Mwajuma ni nani hasa, nini kilimsukuma kuwekeza katika uvuvi kazi ambayo inatafsiriwa kuwa nya wanaume zaidi, fuatana na Abdulshakur katika makala hii ya dakika saba, natumai utajifunza mengi.

Show more...
2 years ago
6 minutes 17 seconds

Nukta the Podcast
ELIMU YA SAIKOLOJIA INAVYOWABEBA WATU WENYE UALBINO TANZANIA

Watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali unyanyapaa ikiwa miongoni, licha ya afua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kuelimisha watu wanaowazunguka, baadhi ya walemavu hushindwa kujumuika na wanajamii wengine kutokana na hofu au mitizamo ya kifikra waliyonayo wao wenyewe hata kama jamii ina mtizamo chanya juu yao.

Abdushakur Mrisho ametuandalia makala yanayoonesha ni kwa namna gani elimu ya saikolojia inavyoweza kuwakomboa watu hawa na kuwafanya wajione kama watu wengine na kuchangamana na wanajamii wengine katika shughuli za kijamii.


Show more...
2 years ago
9 minutes 15 seconds

Nukta the Podcast
Ifahamu zahanati iliyoanzishwa kwa mkopo wa halmashauri

Ni Zahanati ya Afya ya Jamii iliyopo Kata ya Kipunguni jijini Dar es Salaam ambayo ni ya kwanza katika kata hiyo. Vijana nane wametumia mkopo Sh100 milioni wa Halmashauri ya Ilala kuianzisha ili kupunguza changamoto za afya jijini humo. Esau Ng'umbi anasimulia zaidi.

Show more...
2 years ago
8 minutes 20 seconds

Nukta the Podcast
Mradi wa umemejua unavyowafaidisha wanavijiji Tanzania

Ni mradi wa jiko linalotumia mionzi ya umemejua kupikia vyakula mbalimbali. jiko hilo la aina yake limebuniwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. 

Show more...
3 years ago
7 minutes 30 seconds

Nukta the Podcast
Wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi shuleni Pangani

Salaaam msikilizaji wa NUKTA THE PODCAST karibu katika muendelezo wa makala zetu na leo tunasafiri hadi Wilayani pangani mkoani Tanga kumulika namna wazazi wanavyopambana kuwapatia chakula wanafunzi katika shule za sekondari, i mimi ni Suleman Omar Mwiru.

Show more...
3 years ago
6 minutes 34 seconds

Nukta the Podcast
Zaidi ya Watanzania 500,000 kukumbukwa na uhaba wa chakula

Wakati baadhi ya Watanzania wakila na kusaza kiasi cha kutupa chakula, ripoti mpya ya usalama wa chakula na lishe Tanzania inakadiria kuwa kuanzia Mei 2022 watu 592,000 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini.

Ripoti hiyo ya Tathmini ya Usalama wa Chakula na Lishe iliyotolewa Februari 2022 na Wizara ya Kilimo na Idara ya Udhibiti Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza kuwa hali hiyo ya uhaba mkubwa wa chakula itashudiwa kati ya mwezi Mei hadi Septemba mwaka huu.

Nini sababu? Herimina Mkude anasimulia zaidi.

Show more...
3 years ago
3 minutes 29 seconds

Nukta the Podcast
Nukta Habari inakusogeza na mambo mtambuka yanayokuhusu ikiwemo burudani, mtindo maisha, safari, teknolojia na biashara.