
Katika episode hii tutaangazia jinsi tatizo la maji Ilivyowaunganisha wakulima na wafugaji Kilosa.
Hapa utasikia simulizi ya wafugaji na wakulima waliokuwa maadui kutokana na mgogoro wa maji walivyogeuka marafiki baada ya kumfahamu adui wao wa kweli.
Kama nilivyoeleza katika episode ya kwanza mimi na producer wangu tulipata wasaa wa kuzunguka baadhi ya vijiji vya wilaya za Kilombero, Kilosa na Morogoro mjini kuona mwenendo wa utunzaji wa vyanzo vya maji, mienenendo ya migogoro inayohusiana na rasilimali maji na malisho na hatua zilizofikiwa hadi sasa. Karibu twende nami mpaka mwisho wa episode hii.