
Ukuaji wa teknolojia umeendelea kuchochea ongezeko la utajiri duniani jambo ambalo limesababisha watu waliowekeza katika sekta hiyo kuendelea kujikusanyia ukwasi na kutawala orodha ya watu wenye ukwasi mwingi zaidi duniani.
Orodha ya watu matajiri duniani ya mwaka 2025 inayotolewa na Jarida la Forbes la nchini Marekani inaonesha chanzo cha utajiri wa watu 10 matajiri zaidi ni uwekezaji katika teknolojia na biashara.
Kwa mujibu Forbes duniani kuna zaidi ya mabilionea 2,700 wakiwa na jumla ya utajiri wa Dola Trilioni 14.2 za Marekani wakitokea katika sekta mbalimbali kama teknolojia, biashara, na huduma za kifedha na makala hii inaangazia watu 10 tajiri zaidi.