Home
Categories
EXPLORE
Society & Culture
True Crime
Business
TV & Film
Science
Comedy
History
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
Loading...
0:00 / 0:00
Podjoint Logo
TH
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts126/v4/1d/57/81/1d578167-1cb3-fd3f-c67a-c7b34ef3cc1d/mza_13975209208286552282.jpg/600x600bb.jpg
LENZI Podcast with Michael Kamukulu
Michael Kamukulu
23 episodes
6 days ago
Jifunze kupitia mijadala na maelezo yanayohusu mada mbalimbali ili upate ufahamu juu mienendo ya sasa katika nyanja na tasnia tofauti. Pata uchambuzi wa takwimu rasmi katika kuleta uhalisia wa mada tunazozijadili. Uwe ni mmiliki wa biashara unayetaka kuboresha biashara yako ama kufungua mradi mpya, au mtu binafsi unayetaka kuongeza ufanisi wako, podcast yetu ina kitu kwa ajili yako. SIKILIZA ILI UWEZE KUJIFUNZA
Show more...
Self-Improvement
Education
RSS
All content for LENZI Podcast with Michael Kamukulu is the property of Michael Kamukulu and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Jifunze kupitia mijadala na maelezo yanayohusu mada mbalimbali ili upate ufahamu juu mienendo ya sasa katika nyanja na tasnia tofauti. Pata uchambuzi wa takwimu rasmi katika kuleta uhalisia wa mada tunazozijadili. Uwe ni mmiliki wa biashara unayetaka kuboresha biashara yako ama kufungua mradi mpya, au mtu binafsi unayetaka kuongeza ufanisi wako, podcast yetu ina kitu kwa ajili yako. SIKILIZA ILI UWEZE KUJIFUNZA
Show more...
Self-Improvement
Education
Episodes (20/23)
LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E22 Unatumia Siku 28 kwenye Social Media kwa Mwaka: Ijue Gharama Halisi | LENZI | Michael Kamukulu

Ijue gharama halishi ya muda ambao unautumia kwenye social media (mitandao ya kijamii). Kwa wastani mtumiaji wa kawaida wa internet anatumia saa 2.5 mpaka 3 kwenye mitandao ya kijamii kwa siku. Mtanzania wa kawaida anatumia wastani wa saa 2.5 kwa siku ambayo ni sawa na siku 28 za kazi kwenye social media kwa mwaka. Huu ni muda mwingi ambao usipotumika vizuri unasababisha hasara kifedha na kiafya pia. Jifunze na upate siri na maarifa zaidi kuhusu ukweli juu ya matumizi ya simu, internet na mitandao ya kijamii. Ungana na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast 

Show more...
1 year ago
4 minutes 6 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E21 Digital Detox: Jinsi nilivyojiondoa kwenye addiction ya SIMU na Mitandao | Michael Kamukulu LENZI

DIGITAL DETOX Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi. Mawasiliano ni kitu cha kuhimu lakini ni muhimu kufuatilia miendendo ya matumizi ya simu za mkononi na mitandao ili kuepuka madhara na athari mbaya. Punguza matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi ili ulinde maisha na afya yako. Kabla ya kukabiliana na athari hizi, ni muhimu sana mtu akafahamu kama tayari anapitia changamoto hizi au la. Kuna njia nyingi za kutammbua kama umeathiriwa na matumizi makubwa ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Njia rahisi ni kuangalia kama una mojawapo ya dalili zifuatazo: 1. Kutopendelea kuzungumza na watu, na badala yake kukaa na simu za mkononi au mitandao ya kijamii 2. Kuwa na hali ya wasiswasi uliopitiliza mara kwa mara (Anxiety) 3. Kukosa usingizi (kushindwa kulala vizuri) 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) Zipo njia nyingi za kuondokana na madhara ya matumizi yaliyopitiliza ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi pamoja na TV.; kati ya hizi ni hizi hapa tano (5): 1. KUTENGA MUDA wa kukaa bila simu/mitandao 2. Kudhibiti APPS 3. Kudhibiti MUDA wa matumizi 4. Kudhibiti MAENEO ya matumizi 5. Balance: Maisha BINAFSI na Maisha ya KAZI Ungana na Michael Kamukulu uweze kujifunza zaidi kupitia LENZI  @lenzipodcast  Chapters 00:00 Madhara: matumizi yaliyopitiliza ya simu na mitandao 01:33 Digital Detox 02:36 1. KUTENGA MUDA wa kukaa bila simu/mitandao 04:26 2. Kudhibiti APPS 06:43 3. Kudhibiti MUDA wa matumizi 08:13 4. Kudhibiti MAENEO ya matumizi 08:39 5. Balance: Maisha BINAFSI na Maisha ya KAZI Jifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI @lenzipodcast

Show more...
1 year ago
10 minutes 32 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E20 Matumizi ya SIMU: Fahamu athari za matumizi yaliyopitiliza ya simu | LENZI | Michael Kamukulu

Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi. Mawasiliano ni kitu cha kuhimu lakini ni muhimu kufuatilia miendendo ya matumizi ya simu za mkononi na mitandao ili kuepuka madhara na athari mbaya. Punguza matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi ili ulinde maisha na afya yako. Kabla ya kukabiliana na athari hizi, ni muhimu sana mtu akafahamu kama tayari anapitia changamoto hizi au la. Kuna njia nyingi za kutammbua kama umeathiriwa na matumizi makubwa ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Njia rahisi ni kuangalia kama una mojawapo ya dalili zifuatazo: 1. Kutopendelea kuzungumza na watu, na badala yake kukaa na simu za mkononi au mitandao ya kijamii 2. Kuwa na hali ya wasiswasi uliopitiliza mara kwa mara (Anxiety) 3. Kukosa usingizi (kushindwa kulala vizuri) 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) Zipo njia nyingi za kuondokana na madhara ya matumizi yaliyopitiliza ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi pamoja na TV. Fuatilia zaidi uweze kujifunza na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast #mitandaoyakijamii #digitaldetox #mitandao #socialmedia #overused #lenzi #afyayaakili #afyayako #simuyako * * * Timestamps 00:00 Ukweli kuhusu matumizi ya simu na mitandao 01:55 1. Kupendelea kutozungumza na watu 03:49 2. Wasiswasi uliozidi (Anxiety) 04:59 3. Kukosa Usingizi (kushindwa kulala) 05:32 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) 06:54 Jinsi ya kujiondoa kwenye madhara ya matumizi makubwa ya simu na mitandao ya kijamii

Show more...
1 year ago
7 minutes 48 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E19 Mjasiriamali: YAJUE MAENEO MANNE (4) YA UWEKEZAJI USIOKUWA WA KIBIASHARA | LENZI | Michael Kamukulu

Mafanikio hayatokei kwa bahati, wanaofanikiwa wote wanajuia na kuifuata misingi inayowapelekea mafanikio kwa kuwekeza kwenye maeneo yanayoongeza thamani yao kwenye maisha. Siri ya mjasiriamala au mfanyakazi mwenye mafanikio iko kwenye uwezo wake wa kuongeza thamani yake katika biashara au kazi anayoifanya. Thamani huongezeka kwa kuzingatia misingi mkuu ya fedha, maisha na mafanikio. Unaweza kutumia nguvu na muda mwingi kwenye kuikuza biashara na kutafuta mafanikio, lakini mara baada ya kuyafikia mafanikio hayo, ukashindwa kuyafurahji. Unahitaji kufuata misingi ya uwekezaji kwa kuwekeza kwenye maeneo muhimu yatakayokuongezea thamani na kukuwezesha kudumu kwa muda mrefu katika mafanikio yako. Acha mazoea ya kuwekeza kwenye pesa, ongeza thamani maana pesa hufuata thamani. Haya ni maeneo manne (4) yanayofaa kwa uwekezaji usiokuwa wa kibiashara: 1) Afya Imara 2) Elimu & Maarifa 3) Mahusiano bora (ya aina zote) 4) Taaluma (Career) Jifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast  #mafanikio #biashara #thamani #hela #tanzanianyoutuber #tanzania #kenya #rwanda #timizamalengoyako #lenzi #michaelkamukulu * * * Time Stamps 00:00 Uwekezaji wenye tija 00:32 1. Uwekezaji kwenye Afya 01:59 2. Uwekezaji kwenye Elimu & Maarifa 03:06 3. Uwekezaji kwenye Mahusiano 03:54 4. Uwekezaji kwenye Taaluma (career) 04:48 Fedha inatafuta thamani (money follows value)

Show more...
1 year ago
5 minutes 59 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E18 MTUMIAJI WA SIMU: Fahamu njia tano (5) za kuongeza usalama wako mtandaoni | LENZI | Michael Kamukulu

Katika zama hizi za kidijitali tulizonazo, kulinda usalama wa taarifa zako kwenye mitandao ni muhimu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Jiunge nasi katika video hii tunapoongelea njia tano (5) muhimu za kuimarisha usalama wako mtandaoni. Jifunze jinsi ya kulinda namba yako ya simu, kuweka kinga imara kwenye akaunti zako za baruapepe, kuhifadhi alama za vidole vyako, kujilinda dhidi ya tishio la "deepfake," na kuweka sauti yako salama kutokana na matumizi mabaya kwa njia ya uigizaji wa AI. Epuka vitisho vya kimtandao na kufurahia mtandao usalama zaidi Usisahau kubofya kitufe cha like, kusajili, na kugonga kengele ya taarifa ili kupata taarifa nyingine kama hizi na kuongeza mbinu za usalama wa mtandao! #UsalamaMtandaoni #UsalamaWaMtandaoni #KulindaData #KulindaFaragha #UsalamaWaInterneti #UhamasishajiWaMtandao #UsalamaWaTeknolojia Ungana na Michael Kamukulu ili ujifunze zaidi kupitia LENZI  @lenzipodcast  #mpesa #usalama #cybercrime #cybersecurity #email #iphone #iphone15 #mafanikio #biashara #thamani #hela #tanzanianyoutuber #tanzania #kenya #rwanda #timizamalengoyako #lenzi * * * Time Stamps: 00:00 Uhalisia kuhusu usalama mtandaoni 01:04 1. Namba ya Simu 01:37 2. Email / Baruapepe 02:50 3. Fingerprint / Alama za vidole 03:35 4. Sura 04:50 5. Sauti

Show more...
1 year ago
6 minutes 45 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E17 Jinsi ya Kufanya Manunuzi Salama Mtandaoni: Mambo Matano (5) ya Muhimu | LENZI | Michael Kamukulu

Watu walio wengi hawajui jinsi ya kununua bidhaa kwa njia salama kwenye mtandao kama vile Alibaba, Amazon, Kikuu, Ali Express na mitandao mingine ya aina hii. Kabla ya kuagiza bidhaa kwenye mtandao au simu, ni muhimu kuhakikisha kwamba pesa yako iko salama na unanunua kwa wauzaji wanaoaminika. Unaweza kutumia njia kama vile M Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money au nyingine kama vile Sim Banking. Na unaweza pia ukaagiza buidhaa kwa delivery na ukalipia cash baada ya kupokea bidhaa yako. Ni muhimu kujua Mamboi matano (5) muhimu ambayo yatakusaidia kuwa salama wakati wa manunuzi ya mtandaoni: 1. Kuwa na Akaunti Maalum ya Malipo 2. Nunua kwa Wauzaji Wanaoaminika 3. Tunza/Ficha Taarifa Zako zote Muhimu 4. Fanya Mawasiliano ya kina na Muuzaji kabla ya kununua/kulipia 5. Usifanye Manunuzi Makubwa kwa njia ya Mtandao Fuatilia na ujifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI  @lenzipodcast 

Show more...
1 year ago
5 minutes 2 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E16 Harufu Ya Chakula Haitibu Njaa: Furaha inayotegemea kuwaridhisha watu wengine bila faida binafsi, ni UTUMWA

Njaa hutibiwa na chakula, wala harufu nzuri na hata sio lazima chakula kiwe kitamu sana. Haijalishi kama kinaliwa jioni, mchana, asubuhi wala usiku. Harufu ni hisia inayokuvutia kuelekea kwenye chakula, lakini usipokula hicho chakula, njaa haitaondoka. Hii inatokea sana kwenye maisha yetu ya kila siku katika kutafuta mafanikio ya career, mahusiano, nk. Tunahitaji maarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi yatakayotupa kufanikiwa kwenye kazi, kukuza faida kwenye biashara, kuongeza wigo kama viongozi / kiongozi, kuboresha mahusiano ndani na nje ya ndoa pamoja na mambo mengine mengi. Mojawapo ya njia za kuongeza mafanikio yanayotokana na maamuzi yetu ni kujitambua, kuweka malengo na kuwa na uwezo wa kuyapima malengo kwa kipimo sahihi. Zipo siri na kanuni nyingi ambazo zinaweza kumsaidia kila mtu, lakini walio wengi wamechagua hisia kuliko uhalisia. Watu wengi hupima mafanikio ya maamuzi yao katika maisha, biashara, mahusiano hata kazi kwa kuangalia ni kwa kiasi jamii ikiyowazunguka inaridhishwa. Hata kama itahusisha maumivu, hasara au majuto, bado watu walio wengi wako tayari kufanya jambo wasilolitaka ilimradi wengine wawakubali na kuwaheshimu. Si mara zote matokeo yanakuwa chanya, na ndio maana kuna umuhimu wa kuangalia faida zote, binafsi na zile za jumla ili matokeo ya maamuzi yoyote yale yasije yakaishia kuwa majuto, hasira, chuki, aibu ama kukata tamaa. * * * Hadithi/Simulizi Mtoto (yatima) aliomba chakula cha kwake na wadogo zake ili wasife njaa baada ya kukaa siku nyingi bila mlo wowote. Mtu mzima aliyeombwa chakula alimjibu kwa kutoa ushauri, “chukua kitunguu swaumu ukakichome kwenye moto, majirani wakisikia watasema mmepika na kuka chakula kizuri”. Huu ushauri haukulenga kutatua tatizo halisia, ulilenga kuionesha jamii kwamba hakuna tatizo wakati huo huo madhara yakiendelea kutokea kwa watoto. * * * Ongeza uwezo wako katika kufanya maamuzi sahihi kwa kutumia njia bora ambazo hazina madhara. Sikiliza uweze kujifunza zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI |  @lenzipodcast 

Show more...
1 year ago
3 minutes 14 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E15 Ishara 5 kwamba unapoteza kuliko unavyopata (unapoteza MUDA, THAMANI, FEDHA kwenye kazi na biashara)

Kama hasara ama gharama ya kupata jambo lolote inakuwa kubwa kuliko faida zinazotokana na jambo hilo, basi hatuna budi kuachana na jambo husika na kutafuta mbadala unataofaa na kutupa manufaa tunayoyahitaji. Kama gharama za matumizi zinazidi kiwango cha mshahara ama faida ya biashara, ni wakati wa kubadilisha kazi au biashara hiyo. Mara nyingine inakuwa vigumu kufahamu kwamba tayari uko kwenye hali ya kupoteza na kuliko kunufaika. Hizi ni ishara 5 kati ya nyingi zinazokufungua macho ili kujua kwamba ni wakati wa kufanya jambo tofauti. 1. Gharama za matumizi ni kubwa kuliko kipato (mshaharara au faida ya biashara) 2. Kutokuona mabadiliko (matokeo) yanayotokana na kazi au biashara 3. Kushindwa kumiliki na kusimamia muda na ratiba binafsi 4. Kushindwa kuishi katika uhalisia wa ndani (failure to be your authentic self) 5. Kushindwa kutumia uwezo binafsi (vipaji na karama) Ungana na Michael Kamukulu ili kujifunza zaidi kupitia LENZI |  @lenzipodcast 

Show more...
2 years ago
8 minutes 51 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E14 Fahamu sababu za kuichoka kazi yako (Mambo Matatu [3] ya kuzingatia) | LENZI | Michael Kamukulu

Wengi wetu tunaamini kwamba biashara ya bodaboda inawanufaisha zaidi waendesha pikipiki na bajaji lakini ukweli unaweza ukawa tofauti. Waendeshaji wengi wa vyombo hivi vya moto sio wamiliki wa biashara, wao ni watoa huduma. Mtazamo wao kwenye biashara hii unawafanya wasiwe wamiliki wa kazi yao wenyewe. Wanaweka mkazo zaidi kwenye kurejesho hesabu ya mabosi wao kuliko kuisimimaia biashara kwa ajili ya maslahi mapana ya uchumi wao binafsi na familia zao. Ungana na Michael Kamukulu kwenye LENZI ​⁠​⁠ @lenzipodcast  ili uweze kujifunza zaidi ni kwa jinsi gani bodaboda wanaweza kujikomboa na kuimiliki kazi yao wenyewe. Zifahamu huduma za ziada ambazo waendesha bodaboda na bajaj wanazitoa mbali na kusafirisha abiria. Kama wewe ni dereva bodaboda au bajaji unaweza kuongeza ushawishi na nguvu yako katika kutengeneza shilingi na kumiliki biashara yako. Jifunze na upate majibu ya maswali yako kwenye video hii na video nyungine kupitia LENZI ​⁠​⁠ @lenzipodcast  Utafutaji bila malengo na ufahamu ni sawa na kucheza michezo ya tamthilia.

Show more...
2 years ago
10 minutes 9 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E13 Ni Nani Anashikilia Uchumi, Soko na Umiliki wa Biashara ya Bodaboda?? | LENZI | Michael Kamukulu

Wengi wetu tunaamini kwamba biashara ya bodaboda inawanufaisha zaidi waendesha pikipiki na bajaji lakini ukweli unaweza ukawa tofauti. Waendeshaji wengi wa vyombo hivi vya moto sio wamiliki wa biashara, wao ni watoa huduma. Mtazamo wao kwenye biashara hii unawafanya wasiwe wamiliki wa kazi yao wenyewe. Wanaweka mkazo zaidi kwenye kurejesho hesabu ya mabosi wao kuliko kuisimimaia biashara kwa ajili ya maslahi mapana ya uchumi wao binafsi na familia zao. Ungana na Michael Kamukulu kwenye LENZI ​⁠​⁠ @lenzipodcast  ili uweze kujifunza zaidi ni kwa jinsi gani bodaboda wanaweza kujikomboa na kuimiliki kazi yao wenyewe. Zifahamu huduma za ziada ambazo waendesha bodaboda na bajaj wanazitoa mbali na kusafirisha abiria. Kama wewe ni dereva bodaboda au bajaji unaweza kuongeza ushawishi na nguvu yako katika kutengeneza shilingi na kumiliki biashara yako. Jifunze na upate majibu ya maswali yako kwenye video hii na video nyungine kupitia LENZI ​⁠​⁠ @lenzipodcast  Utafutaji bila malengo na ufahamu ni sawa na kucheza michezo ya tamthilia.

Show more...
2 years ago
9 minutes 40 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E12 Kwa nini hatuwezi kulipa madeni?? (2/3 ya watanzania hawawezi kumudu gharama za maisha)

Ripoti ya  @finscope  ya 2023 imeongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na sababu zinazowafanya Watanzania kukopa fedha. Katika kuichambua zaidi hii ripoti na kuunganisha taarifa nyingine (nje ya ripoti) tumegundua kuwa watu wengi wanaamini kwamba kumekuwepo na u]kukosekana kwa uaminifu baina yta watu hususani kwenye masuala ya kifedha ambapo watu walio wengi wanakopa na wanakuwa hawalipi madeni yao. Uaminifu sio sababu PEKEE inayopelekea watu kutolipa madeni yao, kuna sababu nyingine kama vile kutokuwa na ELIMU sahihi kuhusu masuala ya kifedha, ugumu wa maisha (kipato kidogo) - jambo ambalo linasababisha watu kukosa njia ya kuzalisha (kutengengeza) kipato cha kutosha na kmwisho wa siku kuamua kuweka kipaumbele kwenye kuishi (survive) na sio kulipa madeni yao. Lakini kwa upande mwingine, kukopa kumegeuka kuwa mtindo wa maisha kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakichukulia kukopa kama njia rahisi ya kutatua matatizo hata yale ambayo yasingehitaji mkopo endapo wangefikira kwa umakini madhara ambayo yangejitokeza endapo wangechukua mikopo katika hali walizonazo za kiuchumi. Madhara ya mikopo yamekuwa ni makubwa yakijumuisha kuvunjiuka kwa urafiki, familia na hata baadhi ya ndoa. Ungana na Michael Kamukulu ujifunze zaidi kwenye LENZI  @lenzipodcast ​

Show more...
2 years ago
13 minutes 31 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E11 Zijue Kazi 10 Mpya Kwenye Soko la Ajira (Duniani!)

Kama ni mwanafunzi, episode hii itakusaidia kuchagua kozi sahihi za kusomea vyuoni katika kipindi hiki ambacho ajira hazitabiliki. Kozi zenye ajira leo zinaweza zisiwe na nafasi za ajira tena sokoni ndani ya mmiaka michache. Mfanyakazi yeyote asiyejiendeleza (binafsi) kwa kuongeza maarifa yake katika anachokifanya, uwezekano wake wa kufanikiwa kwenye Maisha ni mdogo. Kutokana na mabadiliko ya maendeleo na teknolijia, baadhi ya kazi zitaendela kupoteza umuhimu wako jambo litakalopelekea kazi hizo kutoweka sokoni taratibu mpaka hapo zitakapokwisha kabisa, kwa sababu hakuna mtu yeyote atakayekuwa akizihitaji. Kwa upande mwingine, KAZI mpya zinazaliwa kila siku na uhitaji wake katika soko ni mkubwa kwa sababu ujuzii na maarifa yanayoamnbatana na kazi hizo ni adimu. Kazi mpya zina nafasi kubwa ya kumpa mtu nafasi ya kupata kipato kizuri, kukua na kuongezeka na hatimaye kufanikiwa kwenye Maisha nje ya kazi. Ungana na Michael Kamukulu kujifunza zaidi kupitia  @lenzipodcast ​

Show more...
2 years ago
14 minutes 16 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E10 SIRI 5 za KUKUA, na KUFANIKIWA kwenye KAZI (AJIRA) na maisha

Elimu rasmi ni muhimu sana katika kufungua milango ya kazi (ajira); lakini vyeti peke yake havitoshi kukupa mafanikio unayotamanni kuyapata kwenye Maisha kwa kupitia kazi/ajira yako. Kuna mbinu na kanuni nyingi ambazo hazifundishwi kwenye mifumo ya elimu rasmi lakini zinapatikana mtaani baada ya kuanza kufanya kazi.

Mfanyakazi yeyote asiyejiendeleza (binafsi) kwa kuongeza maarifa yake katika anachokifanya na zaidi ya hichi anachokifanya, uwezekano wake wa kufanikiwa kwenye Maisha ni mdogo.

Kupata madaraja ya juu ya ufaulu shuleni au vyuoni sio kigezo cha kupata mafanikio makubwa kwenye Maisha.

Ni muhimu pia kujua mafanikio ni kitu gani. Endapo mtu ataweka malengo ya kufanya kitu fulani kwa wakati Fulani na akafanya hivyo, basi amefanikiwa; na kinyume chake. Hivyo basi, mafanikio yanahoitaji kupimwa kwa vigezo vya (1) Malengo na (2) Muda. Malengo yanatakiwa kuwekwa katika vipindi vywa muda mfupi na muda mrefu pia ili kupima maendeleo kwenye vipindi vifupi vifupi na kupima mafanikio ya jumla (muda mrefu) ifikapio mwishi wa safari.

 

Kutokana na mabadiliko ya maendeleo na teknolijia, baadhi ya kazi zitaendela kupoteza umuhimu wako jambo litakalopelekea kazi hizo kutoweka sokoni taratibu mpaka hapo zitakapokwisha kabisa, kwa sababu hakuna mtu yeyote atakayekuwa akizihitaji. Kwa upande mwingine, KAZI mpya zinazaliwa kila siku na uhitaji wake katika soko ni mkubwa kwa sababu ujuzii na maarifa yanayoamnbatana na kazi hizo ni adimu. Kazi mpya zina nafasi kubwa ya kumpa mtu nafasi ya kupata kipato kizuri, kukua na kuongezeka na hatimaye kufanikiwa kwenye Maisha nje ya kazi.

Show more...
2 years ago
14 minutes 53 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E9 Biashara na Wajasiriamali 7 wenye washindani usioutegemea (bila kujali pesa) - Unusual Rivals

Unveiling the Hidden Rivals: How Unexpected Foes Shape the Market! 🚀 Discover the secret competition behind the scenes as seemingly unrelated products and services battle for your attention and loyalty. From phone-camera filters vs cosmetics makers to writing AI vs editors, we expose the surprising clashes that influence customer choices. 🤔 Join us for an eye-opening journey into the world of indirect competitors and how they serve YOU! 🌟 Don't miss this mind-bending episode! 🎬 #MarketSecrets #HiddenRivals #BusinessCompetition


***


Wajue washindani waliofichika: Jinsi baadhi ya biashara, bidhaa na huduma zinavyoathiri mwenendo wa soko kwa kushindania walaji hata kama wauzaji hawajui kuhusu ushindani wao.


Bidhaa na huduma zisizofanana zinashindana bila kujua ili kukuuzia bidhaa na huduma zao. Kuanzia kamera za simu v/s wazalishaji wa vipodozi hadi AI v/swahariri.


Show more...
2 years ago
18 minutes

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E8 [Part 2] Simu Sio Chanzo za Migogoro kwenye Mahusiano ft. Teacher Gonza

Katika ulimwengu huu ambao matumizi ya simu na mitandao ya kijamii yamekuwa makubwa, simu zinadhaniwa kuwa mojawapo ya vyanzo vikuu vinavyosababisha migogoro na kuvunjika kwa mahusiano na ndoa. Msikilize Michael Kamukulu pamoja na Teacher Gonza wakielezea ni kwa namna gani simu SIO chanzo cha migogoro ya mahusionao kama wengi wanavyodhani.

Show more...
2 years ago
24 minutes 37 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E7 [Part 1] Simu Sio Chanzo cha Migogoro kwenye Mahusiano ft Teacher Gonza

Katika ulimwengu huu ambao matumizi ya simu na mitandao ya kijamii yamekuwa makubwa, simu zinadhaniwa kuwa mojawapo ya vyanzo vikuu vinavyosababisha migogoro na kuvunjika kwa mahusiano na ndoa. Msikilize Michael Kamukulu pamoja na Teacher Gonza wakielezea ni kwa namna gani simu SIO chanzo cha migogoro ya mahusionao kama wengi wanavyodhani.

Show more...
2 years ago
25 minutes 57 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E5. UBUNIFU [Part 2]: Jinsi DIGITALI inavyofungua milango ya FURSA za uzalishaji wa MAUDHUI na MAWASILIANO ft. Jane Shussa

Katika episode hii, Michael Kamukulu anaongea na Jane Shussa kuhusu jinsi mabadiliko ya kidigitali yanavyobadilisha namna ya UZALISHAJI WA MAUDHUI na MAWASILIANO. Pamoja, wanachunguza athari za mabadiliko haya kwenye sekta mbalimbali. Wanaongeleo pia usalama mitandaoni nan je ya mitandao katika zama hizi mpya. Jiunge nao kwenye mada hii ya kuvutia inayojikita katika mabadiliko yasiyokwepeka kwa wabunifu wa maudhui na mawasilino.

 

***

Creative Disruption: The Transformative Power of Digital Shifts in Content Creation and Communication

 

In this episode of "Creative Disruption," host Michael Kamukulu engages in a captivating conversation with special guest Jane Shussa. They explore how digital shifts are transforming content creation and communication. From the rise of social media to the role of artificial intelligence, they provide valuable insights into the future of these industries. Join them on this inspiring journey through the evolving landscape of content and communication.

Show more...
2 years ago
28 minutes 2 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E5. UBUNIFU [Part 1]: Jinsi DIGITALI inavyofungua milango ya FURSA za uzalishaji wa MAUDHUI na MAWASILIANO ft. Jane Shussa

Katika episode hii, Michael Kamukulu anaongea na Jane Shussa kuhusu jinsi mabadiliko ya kidigitali yanavyobadilisha namna ya UZALISHAJI WA MAUDHUI na MAWASILIANO. Pamoja, wanachunguza athari za mabadiliko haya kwenye sekta mbalimbali. Wanaongeleo pia usalama mitandaoni nan je ya mitandao katika zama hizi mpya. Jiunge nao kwenye mada hii ya kuvutia inayojikita katika mabadiliko yasiyokwepeka kwa wabunifu wa maudhui na mawasilino. *** Creative Disruption: The Transformative Power of Digital Shifts in Content Creation and Communication In this episode of "Creative Disruption," host Michael Kamukulu engages in a captivating conversation with special guest Jane Shussa. They explore how digital shifts are transforming content creation and communication. From the rise of social media to the role of artificial intelligence, they provide valuable insights into the future of these industries. Join them on this inspiring journey through the evolving landscape of content and communication.

Show more...
2 years ago
28 minutes 10 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E4. [Part 2] Je, tuko salama kwenye ulimwengu wa Data na Teknolojia? ft. Miriam Mwaibula

SEHEMU YA PILI

Zifahamu siri na maarifa ya kuwa salama katika zama mpya za Data na Teknolojia. Jifunze: Data ni nini? Matumizi salama ya mitandao! Utunzaji wa taarifa muhimu, na mengine mengi...

Show more...
2 years ago
20 minutes 58 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
S1E3. [Part 1] Je, tuko salama kwenye zama mpya za Data na Teknolojia? ft.Miriam Mwaibula

Zifahamu siri na maarifa ya kuwa salama katika zama mpya za Data na Teknolojia. Jifunze kuhusu:

1. Maana ya data na takwimu! 2. Matumizi salama ya mitandao! 3. Utunzaji wa taarifa muhimu, na mengine mengi...

Show more...
2 years ago
23 minutes 10 seconds

LENZI Podcast with Michael Kamukulu
Jifunze kupitia mijadala na maelezo yanayohusu mada mbalimbali ili upate ufahamu juu mienendo ya sasa katika nyanja na tasnia tofauti. Pata uchambuzi wa takwimu rasmi katika kuleta uhalisia wa mada tunazozijadili. Uwe ni mmiliki wa biashara unayetaka kuboresha biashara yako ama kufungua mradi mpya, au mtu binafsi unayetaka kuongeza ufanisi wako, podcast yetu ina kitu kwa ajili yako. SIKILIZA ILI UWEZE KUJIFUNZA