Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Society & Culture
Business
News
Sports
TV & Film
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts126/v4/1d/57/81/1d578167-1cb3-fd3f-c67a-c7b34ef3cc1d/mza_13975209208286552282.jpg/600x600bb.jpg
LENZI Podcast with Michael Kamukulu
Michael Kamukulu
23 episodes
4 days ago
Jifunze kupitia mijadala na maelezo yanayohusu mada mbalimbali ili upate ufahamu juu mienendo ya sasa katika nyanja na tasnia tofauti. Pata uchambuzi wa takwimu rasmi katika kuleta uhalisia wa mada tunazozijadili. Uwe ni mmiliki wa biashara unayetaka kuboresha biashara yako ama kufungua mradi mpya, au mtu binafsi unayetaka kuongeza ufanisi wako, podcast yetu ina kitu kwa ajili yako. SIKILIZA ILI UWEZE KUJIFUNZA
Show more...
Self-Improvement
Education
RSS
All content for LENZI Podcast with Michael Kamukulu is the property of Michael Kamukulu and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Jifunze kupitia mijadala na maelezo yanayohusu mada mbalimbali ili upate ufahamu juu mienendo ya sasa katika nyanja na tasnia tofauti. Pata uchambuzi wa takwimu rasmi katika kuleta uhalisia wa mada tunazozijadili. Uwe ni mmiliki wa biashara unayetaka kuboresha biashara yako ama kufungua mradi mpya, au mtu binafsi unayetaka kuongeza ufanisi wako, podcast yetu ina kitu kwa ajili yako. SIKILIZA ILI UWEZE KUJIFUNZA
Show more...
Self-Improvement
Education
https://d3t3ozftmdmh3i.cloudfront.net/staging/podcast_uploaded_nologo/37663812/37663812-1696569596794-1d116ff4a1c74.jpg
S1E16 Harufu Ya Chakula Haitibu Njaa: Furaha inayotegemea kuwaridhisha watu wengine bila faida binafsi, ni UTUMWA
LENZI Podcast with Michael Kamukulu
3 minutes 14 seconds
2 years ago
S1E16 Harufu Ya Chakula Haitibu Njaa: Furaha inayotegemea kuwaridhisha watu wengine bila faida binafsi, ni UTUMWA

Njaa hutibiwa na chakula, wala harufu nzuri na hata sio lazima chakula kiwe kitamu sana. Haijalishi kama kinaliwa jioni, mchana, asubuhi wala usiku. Harufu ni hisia inayokuvutia kuelekea kwenye chakula, lakini usipokula hicho chakula, njaa haitaondoka. Hii inatokea sana kwenye maisha yetu ya kila siku katika kutafuta mafanikio ya career, mahusiano, nk. Tunahitaji maarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi yatakayotupa kufanikiwa kwenye kazi, kukuza faida kwenye biashara, kuongeza wigo kama viongozi / kiongozi, kuboresha mahusiano ndani na nje ya ndoa pamoja na mambo mengine mengi. Mojawapo ya njia za kuongeza mafanikio yanayotokana na maamuzi yetu ni kujitambua, kuweka malengo na kuwa na uwezo wa kuyapima malengo kwa kipimo sahihi. Zipo siri na kanuni nyingi ambazo zinaweza kumsaidia kila mtu, lakini walio wengi wamechagua hisia kuliko uhalisia. Watu wengi hupima mafanikio ya maamuzi yao katika maisha, biashara, mahusiano hata kazi kwa kuangalia ni kwa kiasi jamii ikiyowazunguka inaridhishwa. Hata kama itahusisha maumivu, hasara au majuto, bado watu walio wengi wako tayari kufanya jambo wasilolitaka ilimradi wengine wawakubali na kuwaheshimu. Si mara zote matokeo yanakuwa chanya, na ndio maana kuna umuhimu wa kuangalia faida zote, binafsi na zile za jumla ili matokeo ya maamuzi yoyote yale yasije yakaishia kuwa majuto, hasira, chuki, aibu ama kukata tamaa. * * * Hadithi/Simulizi Mtoto (yatima) aliomba chakula cha kwake na wadogo zake ili wasife njaa baada ya kukaa siku nyingi bila mlo wowote. Mtu mzima aliyeombwa chakula alimjibu kwa kutoa ushauri, “chukua kitunguu swaumu ukakichome kwenye moto, majirani wakisikia watasema mmepika na kuka chakula kizuri”. Huu ushauri haukulenga kutatua tatizo halisia, ulilenga kuionesha jamii kwamba hakuna tatizo wakati huo huo madhara yakiendelea kutokea kwa watoto. * * * Ongeza uwezo wako katika kufanya maamuzi sahihi kwa kutumia njia bora ambazo hazina madhara. Sikiliza uweze kujifunza zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI |  @lenzipodcast 