
Watumiaji wengi hawazifahamu athari zinazotokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii, simu, TV pamoja na aina nyingine ya vifaa vinavyotumia screen. Athari hizi zina madhara makubwa sana ikiwemno kusababisha changamoto za afya ya akili. Athari nyingine ni kama matumizi mabaya ya muda, kupunguza ufanisi kwenye uzalishaji, kuvunjika kwa mahusiano pamoja na madhara mengine mengi. Mawasiliano ni kitu cha kuhimu lakini ni muhimu kufuatilia miendendo ya matumizi ya simu za mkononi na mitandao ili kuepuka madhara na athari mbaya. Punguza matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi ili ulinde maisha na afya yako. Kabla ya kukabiliana na athari hizi, ni muhimu sana mtu akafahamu kama tayari anapitia changamoto hizi au la. Kuna njia nyingi za kutammbua kama umeathiriwa na matumizi makubwa ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii. Njia rahisi ni kuangalia kama una mojawapo ya dalili zifuatazo: 1. Kutopendelea kuzungumza na watu, na badala yake kukaa na simu za mkononi au mitandao ya kijamii 2. Kuwa na hali ya wasiswasi uliopitiliza mara kwa mara (Anxiety) 3. Kukosa usingizi (kushindwa kulala vizuri) 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) Zipo njia nyingi za kuondokana na madhara ya matumizi yaliyopitiliza ya mitandao ya kijamii na simu za mkononi pamoja na TV. Fuatilia zaidi uweze kujifunza na Michael Kamukulu kupitia LENZI @lenzipodcast #mitandaoyakijamii #digitaldetox #mitandao #socialmedia #overused #lenzi #afyayaakili #afyayako #simuyako * * * Timestamps 00:00 Ukweli kuhusu matumizi ya simu na mitandao 01:55 1. Kupendelea kutozungumza na watu 03:49 2. Wasiswasi uliozidi (Anxiety) 04:59 3. Kukosa Usingizi (kushindwa kulala) 05:32 4. Kushindwa kutuliza akili (failure to focus) 06:54 Jinsi ya kujiondoa kwenye madhara ya matumizi makubwa ya simu na mitandao ya kijamii