
Kama ni mwanafunzi, episode hii itakusaidia kuchagua kozi sahihi za kusomea vyuoni katika kipindi hiki ambacho ajira hazitabiliki. Kozi zenye ajira leo zinaweza zisiwe na nafasi za ajira tena sokoni ndani ya mmiaka michache. Mfanyakazi yeyote asiyejiendeleza (binafsi) kwa kuongeza maarifa yake katika anachokifanya, uwezekano wake wa kufanikiwa kwenye Maisha ni mdogo. Kutokana na mabadiliko ya maendeleo na teknolijia, baadhi ya kazi zitaendela kupoteza umuhimu wako jambo litakalopelekea kazi hizo kutoweka sokoni taratibu mpaka hapo zitakapokwisha kabisa, kwa sababu hakuna mtu yeyote atakayekuwa akizihitaji. Kwa upande mwingine, KAZI mpya zinazaliwa kila siku na uhitaji wake katika soko ni mkubwa kwa sababu ujuzii na maarifa yanayoamnbatana na kazi hizo ni adimu. Kazi mpya zina nafasi kubwa ya kumpa mtu nafasi ya kupata kipato kizuri, kukua na kuongezeka na hatimaye kufanikiwa kwenye Maisha nje ya kazi. Ungana na Michael Kamukulu kujifunza zaidi kupitia @lenzipodcast