
Elimu rasmi ni muhimu sana katika kufungua milango ya kazi (ajira); lakini vyeti peke yake havitoshi kukupa mafanikio unayotamanni kuyapata kwenye Maisha kwa kupitia kazi/ajira yako. Kuna mbinu na kanuni nyingi ambazo hazifundishwi kwenye mifumo ya elimu rasmi lakini zinapatikana mtaani baada ya kuanza kufanya kazi.
Mfanyakazi yeyote asiyejiendeleza (binafsi) kwa kuongeza maarifa yake katika anachokifanya na zaidi ya hichi anachokifanya, uwezekano wake wa kufanikiwa kwenye Maisha ni mdogo.
Kupata madaraja ya juu ya ufaulu shuleni au vyuoni sio kigezo cha kupata mafanikio makubwa kwenye Maisha.
Ni muhimu pia kujua mafanikio ni kitu gani. Endapo mtu ataweka malengo ya kufanya kitu fulani kwa wakati Fulani na akafanya hivyo, basi amefanikiwa; na kinyume chake. Hivyo basi, mafanikio yanahoitaji kupimwa kwa vigezo vya (1) Malengo na (2) Muda. Malengo yanatakiwa kuwekwa katika vipindi vywa muda mfupi na muda mrefu pia ili kupima maendeleo kwenye vipindi vifupi vifupi na kupima mafanikio ya jumla (muda mrefu) ifikapio mwishi wa safari.
Kutokana na mabadiliko ya maendeleo na teknolijia, baadhi ya kazi zitaendela kupoteza umuhimu wako jambo litakalopelekea kazi hizo kutoweka sokoni taratibu mpaka hapo zitakapokwisha kabisa, kwa sababu hakuna mtu yeyote atakayekuwa akizihitaji. Kwa upande mwingine, KAZI mpya zinazaliwa kila siku na uhitaji wake katika soko ni mkubwa kwa sababu ujuzii na maarifa yanayoamnbatana na kazi hizo ni adimu. Kazi mpya zina nafasi kubwa ya kumpa mtu nafasi ya kupata kipato kizuri, kukua na kuongezeka na hatimaye kufanikiwa kwenye Maisha nje ya kazi.