
Wengi wetu tunaamini kwamba biashara ya bodaboda inawanufaisha zaidi waendesha pikipiki na bajaji lakini ukweli unaweza ukawa tofauti. Waendeshaji wengi wa vyombo hivi vya moto sio wamiliki wa biashara, wao ni watoa huduma. Mtazamo wao kwenye biashara hii unawafanya wasiwe wamiliki wa kazi yao wenyewe. Wanaweka mkazo zaidi kwenye kurejesho hesabu ya mabosi wao kuliko kuisimimaia biashara kwa ajili ya maslahi mapana ya uchumi wao binafsi na familia zao. Ungana na Michael Kamukulu kwenye LENZI @lenzipodcast ili uweze kujifunza zaidi ni kwa jinsi gani bodaboda wanaweza kujikomboa na kuimiliki kazi yao wenyewe. Zifahamu huduma za ziada ambazo waendesha bodaboda na bajaj wanazitoa mbali na kusafirisha abiria. Kama wewe ni dereva bodaboda au bajaji unaweza kuongeza ushawishi na nguvu yako katika kutengeneza shilingi na kumiliki biashara yako. Jifunze na upate majibu ya maswali yako kwenye video hii na video nyungine kupitia LENZI @lenzipodcast Utafutaji bila malengo na ufahamu ni sawa na kucheza michezo ya tamthilia.