Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Society & Culture
Business
Sports
Health & Fitness
Technology
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Podjoint Logo
US
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts221/v4/6c/bf/54/6cbf5495-a8ed-d84b-9ebf-d5d3af04e72c/mza_14241915264083627507.jpg/600x600bb.jpg
Biblia Inasema Usiogope
Pastor Msafiri
31 episodes
4 days ago
Mafundisho mbalimbali ya Biblia yaliyobeba ujumbe kwamba USIOGOPE. Namna pekee ya kukua katika imani na kukua katika uhusiano wetu na Mungu ni kuweka woga mbali nasi. Tubaki majasiri tukipiga mbio kuumaliza mwendo tuliowekewa na kuufikia mwisho mwema, tukibarikiwa na kufanyika baraka kwa wengine.
Show more...
Religion & Spirituality
RSS
All content for Biblia Inasema Usiogope is the property of Pastor Msafiri and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Mafundisho mbalimbali ya Biblia yaliyobeba ujumbe kwamba USIOGOPE. Namna pekee ya kukua katika imani na kukua katika uhusiano wetu na Mungu ni kuweka woga mbali nasi. Tubaki majasiri tukipiga mbio kuumaliza mwendo tuliowekewa na kuufikia mwisho mwema, tukibarikiwa na kufanyika baraka kwa wengine.
Show more...
Religion & Spirituality
Episodes (20/31)
Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Kuuliza
Lakini hawakulifahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue; wakaogopa kumwuliza maana yake neno lile. Luka 9:45
Show more...
11 months ago
25 minutes 19 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Kumtafuta Bwana Kunaondoa Hofu
"Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote." Zaburi 34:4
Show more...
11 months ago
18 minutes 50 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Kumwona Bwana
Kuna mambo hutavuka usipomwona Bwana; Kuna kiwango cha imani hutafikia usipomwona Bwana. Sikiliza somo hili ujue kwa nini ni mapenzi Yake umwone na kuondoa hofu ya kumwona. Usiogope kumwona Bwana.
Show more...
11 months ago
28 minutes 55 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Zaka
Linapokuja suala la matoleo, sadaka na zaka au changizo mbalimbali, wengi huwa hawatoi au wanatoa kidogo kwa sababu ya woga. Unaogopa hela itaisha wakati bado kuna matumizi. Unahofia too much month at the end of the money. Usiogope kutoa. Usiogope zaka.
Show more...
11 months ago
34 minutes 53 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Baraka Ndogo
Wengi wetu tuna baraka ndogo lakini tunaogopa kuukubali ukweli huu na hivyo kuzuiwa kuongezeka katika baraka. Nyumba nzima ya Yakobo ilikuwa imebarikiwa lakini baraka ndogo ukilinganisha na Yusufu; taifa zima la Israeli walikuwa wamebarikiwa lakini kwa baraka ndogo ukilinganisha na Musa. Ukishaelewa kwamba una baraka ndogo basi umekaa mahali pa kuanza kuongezeka katika baraka. Usiogope kuwa mwenye baraka ndogo.
Show more...
12 months ago
13 minutes 45 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Kubariki
Unapokuwa katikati ya watu wasioamini; au uko chini ya bosi asiyeamini, kumbuka kwamba watu hao wanapaswa kuona baraka za Mungu maishani mwao kwa kupitia wewe. Unapaswa kuwa baraka kwao. Usiogope kuwabariki.
Show more...
1 year ago
15 minutes 9 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Jambo Jipya
Wakati jambo jipya linatukia au kutendeka, usiogope. Kama wewe ni wa Bwana basi fahamu kwamba yote ni kwa wema. Kama hauko na Bwana basi mrejee Yeye uwe upande wake ndiko kwenye amani.
Show more...
1 year ago
18 minutes 1 second

Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Kukataliwa
Usiogope Kukataliwa, kuwa Hodari.
Show more...
1 year ago
25 minutes 17 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Nanyi Iweni Hodari

Biblia inatuonyesha namna ambavyo Bwana Mungu anataka watu wake wawe hodari katika kufanya yale aliyowaamuru wayafanye; hakuna haja ya kuogopa kwa sababu Roho Yake ipo kati ya watu Wake.

Kama wewe ni mwaminini basi huna haja ya kuogopa kwa sababu yale aliyosema nao wakati ule bado yanakuhusu wewe hata leo hii kwa sababu kama mwamini bado Roho Mtakatifu yuko ndani yako. Ukiwa hodari kufanya kazi ya Bwana ndipo utaona utukufu wa mwisho unakuwa mkuu kuliko utukufu wa kwanza.

Sikiliza fundisho hili, utaimarika.

Show more...
1 year ago
27 minutes 4 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Kauli ya Mtu Jasiri

Mtu asiyeogopa ni jasiri, na mtu jasiri ana kauli tofauti na mtu mwoga. Waoga hukimbia wasipofuatiwa na mtu yeyote bali mwenye haki ni jasiri kama simba. Mwenye haki, haki ipatikanayo kwa imani katika Kristo Yesu, ni mtu jasiri katika Bwana na anapaswa kujua kwamba Bwana anategemea kauli yake iwe tofauti na mwoga asiye haki. Kama wewe ni mwenye haki katika Bwana kwa imani ni vema ukajifunza namna kauli yako inapaswa kuwa. Jifunze kuwa na kauli ya mtu jasiri.

Show more...
2 years ago
32 minutes 29 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Kauli ya Mtu Jasiri TRAILER

Mtu asiyeogopa ni jasiri, na mtu jasiri ana kauli tofauti na mtu mwoga. Waoga hukimbia wasipofuatiwa na mtu yeyote bali mwenye haki ni jasiri kama simba. Mwenye haki, haki ipatikanayo kwa imani katika Kristo Yesu, ni mtu jasiri katika Bwana na anapaswa kujua kwamba Bwana anategemea kauli yake iwe tofauti na mwoga asiye haki. Kama wewe ni mwenye haki katika Bwana kwa imani ni vema ukajifunza namna kauli yako inapaswa kuwa. Hii ni trailer ya somo la kujifunza  kuwa na kauli ya mtu jasiri.

Show more...
2 years ago
2 minutes

Biblia Inasema Usiogope
Mambo Yanayoathiri Imani

Kutoogopa ni suala la imani kwa sababu inakupasa kusimama na maandiko kwa imani kwamba yuko Mungu anayakuzungukia pande zote na tena anayeangalia kwamba ufikie mwisho mwema. Na pia kwa sababu woga ni udhihirisho wa kutoamini au kuwa na imani haba hivyo haikwepeki kwamba mambo yanayoathiri imani yako yanagusa moja kwa moja kuogopa au kutoogopa kwako. Katika episode hii tunaangalia mambo manne yanayoathiri imani ili kukuwezesha kuikuza imani yako uweze kuwa jasiri, usiyeogopa, kwa sababu Biblia inasema usiogope.


Show more...
2 years ago
47 minutes 4 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Tetesi za Vita

Sasa hivi kuna vita vinapiganwa kati ya Urusi na Ukraine, taifa dhidi ya taifa, na bado chokochoko za vita kusambaa ni kubwa. Huku Afrika vita vya wenyewe kwa wenyewe zimezoeleka. Lakini bado tunafahamu kwamba majaribio ya silaha kali na ripoti za gunduzi mbalimbali za namna za kupigana vita na kuua mamilioni ya watu kwa muda mfupi zinavyotisha wengi. Kuhusu siku hizi za mwisho, Yesu alisema "msiogope mtakaposikia matetesi ya vita". Karibu tujifunze...

Show more...
2 years ago
17 minutes 46 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Watoto Alionipa Bwana

Katika nyakati hizi tulizopo sio kitu kigeni masikioni kusikia mtoto kabakwa au kanajisiwa, kauawa na dada wa kazi au kaibwa. Yaani kesi ni chungu nzima. Mambo ni magumu kiasi kwamba wazazi wanaishi kwa hofu juu ya watoto wao. Kama wewe ni mzazi na unamwamini Mungu Aliye hai katika Kristo Yesu basi huna haja ya kuogopa kwa sababu ya Jina hili la fahari na lenye kutisha. Watoto hao aliokupa Bwana wanalindwa na Yeye mwenyewe.


Show more...
2 years ago
15 minutes 29 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Hao Wamchao Bwana

Moja ya jambo litakalokufanya usiogope ni kumcha Bwana. Lakini si tu kutoogopa, Kumcha Bwana kunaleta mambo mengi ya baraka maishani mwako. Lakini hata kumcha Bwana maana yake nini? Haya ndiyo tunayojifunza katika episode hii.

Show more...
2 years ago
17 minutes 9 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Mambo 7 ya Kutoogopa

Biblia Inasema Usiogope; usiogope nini? Yako mengi ambayo watu wanayaogopa lakini Biblia inasema usiyaogope. Katika episode hii tunaangalia mambo 7 ya kutoogopa ili kupiga hatua katika imani.

Show more...
2 years ago
20 minutes 31 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Huna Hatia

Katika maisha ya imani Shetani hupigana vita ili kututoa katika ujasiri tulionao katika Kristo Yesu. Na adui hufanikiwa katika hili pale anapoweza kutujaza dhamiri ya hatia ndani yetu kwamba sisi ni wakosa na hatuna haki mbele za Mungu. Wakristo wengi wanaishi katika dhamiri ya hatia au wataingia kwenye huo mtego hivi karibuni kwa sababu wameshapelekwa kwenye kona ya kuamini kwamba haki yao inatokana na matendo yao mazuri, yaani hawajavunja sheria au torati. Haki yetu haitokani na sheria bali imani na tena tunalo ondoleo la dhambi. Hati iliyokuwa na mashtaka dhidi yako iligongomewa msalabani pale alipokufa Mwokozi wa ulimwengu. Huna hatia! Sikiliza somo hili.


Show more...
3 years ago
15 minutes 14 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Usione Shaka

Mara nyingine tunakuwa na imani ya kuanza kitu au kupokea uponyaji lakini baada ya muda kidogo uponyaji unapeperuka au kile tulichokianza kinakwama. Tunakuwa kama Petro ambaye alianza kutembea juu ya maji halafu akaona upepo mkali akaogopa na kuanza kuzama. Tunaacha kuangalia chanzo cha imani yetu, yaani Kristo Yesu, na kuangalia mazingira. Kumbuka mwenye haki ataishi kwa imani si kwa kuona.

Show more...
3 years ago
22 minutes 2 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Anguko la Watesi Wako

Katika maisha unapokuwa unafanya mapenzi ya Mungu, wale wanaoinuka dhidi yako yaani watesi wako na kwa sababu unafanya mapenzi ya Mungu basi watesi wako wanakuwa kinyume na Mungu. Kama uko katika mapenzi ya Mungu na unakutana na watesi, jipe moyo, maandiko yanasema watesi wako wataanguka.

Show more...
3 years ago
26 minutes 25 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Usiogope Uchawi part 3

Tumepewa mamlaka ya kukanyaga simba na nyoka, naam, mwanasimba na joka tunapaswa kuwaseta kwa miguu. Ukifuatilia hili "joka" ambalo Mkristo umepewa mamlaka ya kulikanyaga utafahamu kwamba ni lile joka, yaani Shetani au Ibilisi kwa jina. Kwa mamlaka uliyonayo siyo tu kwa vibaraka wa shetani bali hata kwa shetani mwenyewe. Ndiyo maana maandiko yanasema mpingeni Shetani naye atawakimbia. Kama baba yao anawakimbia itakuwaje kwa wanae, yaani wachawi!? Kama umeokoka na unajua mamlaka na nguvu ulizonazo, wewe ni tishio kwa nguvu za giza. Sikiliza somo hili fupi ukawafundishe na wengine.


Show more...
3 years ago
25 minutes 24 seconds

Biblia Inasema Usiogope
Mafundisho mbalimbali ya Biblia yaliyobeba ujumbe kwamba USIOGOPE. Namna pekee ya kukua katika imani na kukua katika uhusiano wetu na Mungu ni kuweka woga mbali nasi. Tubaki majasiri tukipiga mbio kuumaliza mwendo tuliowekewa na kuufikia mwisho mwema, tukibarikiwa na kufanyika baraka kwa wengine.