Mwl. Erick’s Podcast
IWENI WATENDAJI WA NENOYak 1:22-25 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Maana mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, huyo ni kama mtu anayejitazama uso wake wa asili katika kioo; Lakini yeye anayeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.1. Ni udanganyifu kuwa msikiaji wa Neno pekeeMt 7:24-27 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile; nayo haikuanguka, kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga, mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba hiyo; ikaanguka: na anguko lake lilikuwa kubwa. 2. Anguko katika maisha si kwa sababu ya yale tunayokabiliana nayo bali ni yale tunayofanyaJifunze zaidi kwenye somo hili
Show more...