KUISHI MAISHA NJE YA NCHI UKIWA MBALI NA WAZAZI NDUGU NA JAMAA
Kwenye episode hii Bad Man na The Road wanachambua committments ambazo zinajitokeza kwenye mahusiano hasa yale mahusiano ya mbali yaan long distance. Je unaweza kusafiri na kumfuata mpenzi wako alie mbali na wewe
Story na Bienvenu kutoka Burundi kuhusiana na fursa mbalimbali za kusoma nchini Taiwan. Ndani ya podcast hii tumechambua maswala na experience ya maisha ya Taiwan, huku Bien akiwasilisha uzoefu wake kwenye kazi alizowahi kuzifanya hapo awali kwenye mashirikika makubwa alivyokuwa Burundi
Interview hii imefanyika kati ya Yuba na Dauphin ambae ni mwanafunzi kutoka Burundi. Ameelezea experience yake tangu afike Taiwan na mambo mengi ambae amepitia kwenye safari yake ya maisha nchini Taiwan.
MacMuga ni Jina lilitumiwa na msanii wa Bongo Flava almaarufu kama King Kiba " Alikiba" kwenye wimbo uitwao MacMuga lengo la wimbo huo ulikua ni kutoa funzo kwa Vijana wanaotafuta maisha nje ya nchi, pindi wanapofanikiwa na kutojisahau kwa kuendekeza starehe na matumizi mabaya ya kile walichokichuma bila kuwekeza hasa nyumbani walikutoka.
Katika episode hii, tunajadili baadhi ya tamaduni za Taiwan na Tanzania. Mgeni wetu, Jane ambaye ni Mtaiwan, anashiriki nasi kwa kuelezea maoni na uelewa wake kuhusu Afrika na Watanzania. Karibu ufurahie mazungumzo yetu ya kuvutia.
🎙️ SISINISISI - Episode 03:
Leo tunazungumzia mapenzi na mahusiano kati ya Taiwan na Tanzania ❤️
Mpanga the Road na Yuba the Bad Man wanachambua tofauti, changamoto, na vichekesho vinavyotokea kwenye mapenzi ya pande hizi mbili.
Usikose burudani, ukweli na ushauri wa mapenzi kutoka kwa SISINISISI ! 😄
#Sisinisisi #MapenziTaiwanNaTanzania #SwahiliPodcast
Katika episode hii ya pili, Mpanga the Road na Yuba the Bad Man wanaingia deep kwenye mada ya maisha ya kazi kwa vijana wa Kiafrika wanaoishi Taiwan. Je, ni rahisi kupata kazi? Changamoto zipi zinawakumba? Na vipi kuhusu uzoefu wao binafsi kazini – kuanzia viwandani hadi kwenye ofisi?
YUBA the BadMan na Mpanga the Road wanajadili maisha ya Taiwan katika vipindi tofauti na kuyalinganisha na maisha ya Tanzania. Podcast hii imejaa burudani, ikiwakilisha simulizi zenye hisia na hadithi zenye mvuto wa kipekee.