Episodi hii inaangazia mila, desturi na tamaduni katika uhifadhi wa maliasili, hususan namna jamii ya Wangoni kutoka mkoani Ruvuma ilivyotumia majina na utamaduni wao kulinda Wanyamapori na Misitu tangu enzi za mababu zetu.
Hadithi hii ya kuvutia inaonesha jinsi urithi wa jadi ulivyokuwa chachu ya kulinda rasilimali za Taifa ambazo leo hii zinachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya uhifadhi na utalii.
Sikiliza simulizi hii adhimu kutoka kwa Chifu Songea Mbano wa Kwanza, kupitia TANAPA Podcast – Episode ya 14.
Mwongozaji: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena
Mgeni: Samweli Vitus Mbano (Chifu Songea Mbano I)
Usikose kila Jumatatu na Alhamisi kupitia majukwaa mbalimbali ya TANAPA Podcast
Episodi hii inakuletea mazungumzo ya kina kuhusu mila, tamaduni na makatazo ya Kabila la Wagongwe lililopo mkoani Katavi na jinsi taratibu hizo zilivyochangia kulinda maliasili na vyanzo vya maji. Mathalani; ilikuwa hairuhusiwi kukata miti iliyokuwa katika vyanzo vya maji kutokaana na imani ya kuwepo kwa nyoka mkubwa wala kuua mnyamapori hadi upewe kibali na pepo au jini Katabi anayepatikana katika Hifadhi ya Taifa Katavi. Sikiliza simulizi hii ya kuvutia katika epsodi ya 13.Eneo: Hifadhi ya Taifa KataviMwongoza kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena Wageni:1. Moses Edward Tende ( Mtemi Sigulu) Chifu wa Kabila la Wagongwe.2. Lukas Moses Msaga - Mtoto wa Mtemi Sigulu anayefundishwa kurithi mikoba ya Mtemi Sigulu.3. Askari Uhifadhi Daraja la Pili - Kimori Shiwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ikolojia, Hifadhi ya Taifa Katavi. Endelea kutufuatilia kupitia Platifomu za TANAPA Podcast.TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.
Episodi hii imeangazia zoezi endelevu la kuwahamisha tembo walowezi kutoka maeneo ya karibu na wananchi kwenda hifadhini na zoezi zima la kuwaswaga tembo waliotoka hifadhini kuvamia maeneo ya wananchi na kuwarudisha hifadhini.
Sikiliza Episodi hii kwa taarifa hiyo na mengine mengi kupitia Epsode ya 12.
Eneo: Misenyi - Bukoba.
Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena
Guests: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Fredrick Mofulu - Mkuu wa Hifadhi Ibanda - Kyerwa.
Na
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Charles Ngendo - Mkuu wa Hifadhi Rumanyika - Karagwe.
Fuatilia kupitia Platform za TANAPA Podcast.
Kuelekea Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, TANAPA PODCAST tunakueletea uchambuzi kuhusu historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika zilizoongozwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Hapa utapata kujifunza mengi kuhusu harakati za Uhuru wa Tanganyika na Afrika kwa ujumla.
Ikumbukwe historia hii imehifadhiwa katika Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere iliyopo Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam.
Fuatilia uhondo huo katika Epsode ya 11.
Eneo: Dar es salaam
Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena
Guest: Afisa Mhifadhi Mkuu Mariam Njaritha - Mkuu wa Kituo Nyumba Kumbukizi ya Mwl. Nyerere
Usikose kila Jumatatu na Alhamisi kupitia Platform za TANAPA Podcast.
TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.
Episodi hii inaangazia mazungumzo ya kina kuhusu zoezi la upandaji wa Mlima Kilimanjaro ambapo Profesa Kamuzora anaeleza uzoefu wake katika kupanda mlima kwa muda mrefu.
Fahamu faida ya kushiriki kampeni ya “Twenzetu Kileleni katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa Taifa letu, kuhamasisha utalii pamoja na utunzaji wa mazingira.
Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena - Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano - TANAPA
Guest: Prof. Faustin Kamuzora - Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi UTT AMIS.
Katika Episode hii tunaangaIa mazungumzo ya kuhusu Kampeni ya Twenzetu Kileleni 2015 inayofanyikaga Desemba 09 kila mwaka kukumbuka mashujaa wetu waliopigania uhuru wa Tanganyika ambapo kwa mwaka huo huo bendera ya Taifa ilipandishwa Mlima Kilimanjaro wenye kilele kirefu kuliko vyote Barani Afrika chenye urefu wa mita “5985 asl” kuangazia nuru ya Uhuru ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Sikiliza TANAPA PODCAST Epsode 08 kwa habari za kweli na uhakika kuhusiana na historia ya Taifa letu, Uhifadhi na Utalii.
Eneo: Dar es Salaam.
Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena
Guest: Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Marwa Waitara.
Episodi hii inaangazia uchambuzi wa kina kuhusu maneno mbalimbali yanayoleta mkanganyiko wa maana na matumizi yake katika jamii.
Katika Episode 07 Mtopezi wa lugha ya Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) Ndugu Oni Sigala anachambua na
kudadavua maneno kadha wa kadha yenye utata katika sekta ya uhifadhi na utalii.
Eneo: Dar es salaam
Mwongozaji: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena
Mgeni: Oni Sigala - Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA)
Usikose kila Jumatatu kupitia Platifomu za TANAPA Podcast.
Sikiliza Episode 06 uchambuzi wa kina katika mwendelezo wa mada inayoeleza elima ya Uhifadhi ikihusisha Mila, Desturi, Tamaduni na Miiko iliyozuia uharibifu wa Maliasili za Taifa ambapo moja ya maeneo hayo kwa sasa ni Hifadhi za Taifa
Host: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena
Guest: Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara, Massana Mwishawa.
TANAPA Podcast Episode 05 inaangazia mwendelezo wa mada inayoeleza elimu ya Uhifadhi iliyohusisha Mila, Tamaduni, Desturi na Miiko anuwai iliyozuia baadhi ya wanyamapori kuuwawa lengo likiwa ni kuhifadhi maliasili zilizokuwa ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa ambayo baadhi yake kwa sasa ndio Hifadhi za Taifa tunazozishuhudia zikitiririsha nyomi ya watalii nchini.
Eneo: Hifadhi ya Taifa Serengeti
Mwongozaji: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena
Wageni: Barnabas Murigo, Kenyatta, Musoka na Stanslaus Mayani
Usikose kila Jumatatu saa 11:00 jioni kupitia TANAPA Podcast.
TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.
Episode hii inaangazia mazungumzo katika ya Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena na Mzee Fanuel Mbise, Eliona Miley na Elikesia Akyoo kuhusu elimu ya Uhifadhi kupitia mila, desturi na tamaduni zilizotumika katika kusheshimu na kutunza maliasili zilizokuwa zimehifadhiwa.
Sikiliza TANAPA Podcast, Episode 03 uelimike kuhusu
Chimbuko la Uhifadhi
Uanzishaji wa Hifadhi mpya na malengo yake
Maeneo matano ya Malikale yaliyokasimishwa TANAPA na
Uzalendo katika kutembelea Hifadhi za Taifa.
Mgeni maalum: Nakaaya Sumari (Tanzania Safari Channel)
Host: ACC Catherine Mbena, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano TANAPA
Fuatilia mfululizo huu wa elimu ya uhifadhi, utalii na mirindimo iliyojaa burudani na maarifa tele.
Katika episode ya pili ya mfululizo huu, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena anaelezea kwa kina kazi mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuhakikisha maliasili zilizopo ndani ya hifadhi za Taifa zinaendelea kulindwa na kuhifadhiwa kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Katika episode hii ya kwanza, tunazungumzia kwa kina kuhusu Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) – kuanzia majukumu yake makuu, muundo wa utendaji kazi, hadi maeneo ya hifadhi yanayosimamiwa chini ya sheria. Ni programu endelevu inayokufahamisha nafasi muhimu ya TANAPA katika kulinda maliasili na kukuza mapato yatokanayo na shughuli za utalii.