Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.
1. Maombi ya kufunga yanaweza kukufanya uongezeke kiimani.
Mathayo 17:21 ‘’ [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] ‘’
2. Macho yako ya ndani yatakuwa yanaona vizuri.
Zaburi 119:18 ‘’ Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. ‘’
. 3. Mwili wako utakuwa umetiishwa.
Wakolosai 3:5 ‘’ Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;‘’
4. Kupokea maana ni ahadi ya MUNGU kujibu maombi yako.
Yeremia 29:13 ‘’Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.'' Tena Biblia inasema ''Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;-Mathayo 7:7'' na kwa sababu MUNGU analiangalia neno lake alitimize basi hata aliposema tuombe ni hakika atajibu maana yeye hajipingi na Neno lake, labda tu sisi tuombe vibaya na tupungukiwe na imani katika maombi yetu.
5. Utamruhusu ROHO MTAKATIFU kukutumia.
1 Kor 12:11 ‘’ lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. ‘’
Maisha Mapya Katika Kristo
1 Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana. 2Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.
3 Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa. 4Kama vile katika mwili mmoja tulivyo na viungo vingi, navyo viungo vyote havina kazi moja, 5vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake. 6Tuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani. 7Kama ni kuhudumu na tuhudumu, mwenye kufundisha na afundishe, 8kama ni kutia moyo na atie moyo, kama ni kuchangia kwa ajili ya mahitaji ya wengine na atoe kwa ukarimu, kama ni uongozi na aongoze kwa bidii, kama ni kuhurumia wengine na afanye hivyo kwa furaha.
Alama Za Mkristo Wa Kweli
9 Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema. 10Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine. 11Msiwe wavivu, bali mwe na bidii katika roho mkimtumikia Bwana. 12Kuweni na furaha katika tumaini, katika dhiki kuweni na saburi, dumuni katika maombi. 13Changieni katika mahitaji ya watakatifu, wakaribisheni wageni.
14Wabarikini wale wanaowatesa, barikini wala msilaani. 15Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao. 16Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu.
17 Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. 18Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. 19Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana. 20Badala yake:
“Kama adui yako ana njaa, mlishe;
kama ana kiu, mpe kinywaji.
Kwa kufanya hivyo,
unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.”
21Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.
Mistari mbalimbali ambayo Mungu amezungumza nasi katika maandiko kwenye Biblia,kuhusu kutokuogopa "USIOGOPE"
JIFUNZE MAARIFA MBALIMBALI YA KIMUNGU KUPITIA PLATFORM ZA SIRI ZA BIBLIA.
YESU KARIBU ANARUDI
KUJIWEKA WAKFU UPYA MBELE ZA MUNGU NA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE WA MANA MINISTRY
Maana halisi ya kuokoka
MUNGU ASIPOKUJIBU MAOMBI YAKO MUULIZE KWANINI: MWAKASEGE
SAA YA WOKOVU NI SASA
maroho yaliyo ndani ya wote wanaotazama picha chafu za ngono/ukombozi upo bado
MAOMBI YA KUVUNJA MAAGANO NA MIKATABA YA KUZIMU
FAIDA 13 ZA MAOMBI YA USIKU
Maarifa ya kiMungu
Jifunze neno la Mungu katika maisha yako
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
MAMBO MUHIMU YANAYOUNDA MADHABAHU
Mungu wa madhabahu
Kuhani wa madhabahu
Washirika wa madhabahu
Kafara ya madhabahu
Nguvu ya madhabahu
28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;
31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
#sirizabiblia
Youtube/siri za biblia
Ndoto kwa kawaida ya wanaadamu katika ulimwengu wa mwili ni mambo unaunayoyaona wakati umelala mara nyingi ndoto utaota wakati umelala
Aina za ndoto kwa tafsiri za ulimwengu wa kimwili
- Ndoto unaota kwa sababu umechoka sana mara nyingi ukiota hivyo watu na wewe mwenyewe unasema kua ni ndoto tu kwa sababu ni uchovu
- Ndoto unaota kwa sababu una mawazo kwa kitu kinakufanya ukifikirie sana mfano ajira au mke au mume ukiota mara nyingi unasema ni ndoto tu kwa sababu namuwaza sana au unawaza sana
- Ndoto unaota kwa sababu umehadithiwa au kuambiwa kitu Fulani kabla haujalala harafu unaota hivyo hivyo.
Sasa hayo yote ni katika Ulimwengu wa kimwili tuangalie katika ulimwengu war oho ndoto ni nini?
- Ndoto maana yake ni ( Hesabu 12:6)
BWANA akasema, “Sikilizeni maneno yangu: “Akiwapo nabii wa BWANA miongoni mwenu, ninajifunua kwake kwa maono, ninanena naye katika ndoto.
Maana yake kwamba Mungu anaongea na watu wake kwa kupitia ndoto na maono ila watu wengi ukiota unasema ni ndoto tu
Kila ndoto unayoota inawezekana ikawa inakuhusu wewe au ndugu,jirani,mwenza,rafiki au mtu yeyote ambaye Mungu anakuonesha kitu juu yake na ukiwa unafatilia ulichokiota kwa makini unatakiwa uishi katika ndoto au maono yako anayokunesha Mungu
@siri za biblia
www.sirizabiblia.com
+255 758 708 804