Home
Categories
EXPLORE
Society & Culture
Sports
History
News
Science
Business
Leisure
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
Loading...
0:00 / 0:00
Podjoint Logo
HU
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts126/v4/49/cb/a5/49cba576-3738-1277-905f-861918b2f5d3/mza_4809734486509274541.jpg/600x600bb.jpg
H.W PODCAST - Positive Vibes!
Hub of Wisdom inc.
39 episodes
4 days ago
Ni muda wa kuchukua nafasi yako katika meza ya H.W nasi tutawasilisha kwako mawazo ya thamani kwa maneno ya dhahabu. Mahali pa kwanza na pekee unapohitaji kuwa kwa ajili ya ustawi wako. Karibu tujifunze vingi. Pata nafasi ya kusikiliza mambo ya msingi sana yatakayonoa stadi zako, kukuongezea maarifa na kuchochea maendeleo yako ya kiutu. #Karibu_nyumbani.
Show more...
Self-Improvement
Education
RSS
All content for H.W PODCAST - Positive Vibes! is the property of Hub of Wisdom inc. and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Ni muda wa kuchukua nafasi yako katika meza ya H.W nasi tutawasilisha kwako mawazo ya thamani kwa maneno ya dhahabu. Mahali pa kwanza na pekee unapohitaji kuwa kwa ajili ya ustawi wako. Karibu tujifunze vingi. Pata nafasi ya kusikiliza mambo ya msingi sana yatakayonoa stadi zako, kukuongezea maarifa na kuchochea maendeleo yako ya kiutu. #Karibu_nyumbani.
Show more...
Self-Improvement
Education
Episodes (20/39)
H.W PODCAST - Positive Vibes!
UHURU WA KIFEDHA KUPITIA UWEKEZAJI - Emilian Busara (MBA, CPA)

Ikiwa unaanza au ni mzoefu tayari katika eneo la uwekezaji kupitia hisa, UTT, hati fungani (bonds) katika video hii mwanataaluma Mwl. Emilian Busara (MBA, CPA) katika uongozi katika biashara, miradi na fedha anakufundisha hatua kwa hatua mbinu rahisi na za kipekee za kuwekeza kwenye hisa na masoko ya fedha kwa mafanikio makubwa! Utajifunza: jinsi ya kuchagua hisa sahihi, kuanza uwekezaji hata kama una mtaji mdogo, na siri za kukuza pesa zako polepole lakini kwa uhakika. Usikose fursa hii ya kipekee ya kujifunza hatua kwa hatua kuelekea uhuru wa kifedha kupitia uwekezaji. Kumbuka kusubscribe ili uendelee kujulishwa pindi matoleo kama hili yanapotoka katika Youtube channel H.W TV. Fatilia kupitia H.W Podcast katika majukwaa ya sauti na kupitia mitandao yetu ya kijamii @hubofwisdom.inc au tovuti www.hubofwisdom.com/media Anza safari yako ya mafanikio leo! #Hisa #Utt #uwekezaji #fedha #mapato Toleo hili limeletwa kwako na @h.w.multimedia.inc Welcome to the home of positive vibes!

Show more...
4 months ago
53 minutes 26 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
Najma Paul - KUIJENGA NGUVU YAKO & KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

"Nianze kwa kuzungumzia hili eneo... Mitikasi ya maisha yako, kutafuta kwako, kupambana kwako. Lifestyle yako, maizingira unayoishi, vinaamua, vinahitaji na vinajenga NGUVU YAKO." Anasema Najma Paul "Fanya vitu vinavyokukwaza, vitu vinavyokukera, katikati ya hivyo vitu kuna miujiza. Niamini mimi."

Angalia toleo hili na mengine mengi kwa njia ya Youtube (H.W TV) www.youtube.com/hubofwisdom-inc

Tuma ujumbe wako wa sauti kwenda namba 0753825794 nasi tutaujumuisha katika toleo lijalo. Kumbuka unaweza kuaccess matoleo haya na kuyapakua kupitia tovuti yetu www.hubofwisdom.com/media wakati wowote pasipo bughudha ya matangazo yanayoweza kuingilia usikivu wako.


Tunathamini maoni yako, tafadhari tuandikie ujumbe wako kupitia anuani ya barua pepe info@hubofwisdom.com


#karibu_nyumbani

Welcome to the home of positive vibes!

You will love it!

Show more...
6 months ago
23 minutes

H.W PODCAST - Positive Vibes!
KUFIKIA KIWANGO CHA JUU ZAIDI KATIKA KILE UTAKACHOKIFANYA - Sebastian Kolowa

"Sisi sote tuna nafasi ya kustawi zaidi katika chochote tunachokifanya. Changamoto inayotukumba vijana wengi ni kwamba hatutambui na kuzifuata zile hatua muhimu zenye kutufikisha hapo. Muda ni mchache na sio sawa kwenda bila dira. Ndio maana leo nimeona niyazungumze haya yafuatayo..." Anasema Sebastian Kolowa katika mkutano wa nne wa Hub of Wisdom Community Jijini Dar Es Salaam. Fuatilia Matoleo mengine zaidi kupitia H.W TV kwa njia ya YouTube Au sikiliza kupitia H.W PODCAST. Au tuma maoni yako kwa njia ya ujumbe wa maandishi au sauti kupitia 0753825794 ili jukwaa hili lizidi kuwa bora kwa ajili yako na wengine. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi. Tunafurahi unapojifunza lakini tunafurahi zaidi unapofanya. Nenda duniani, kafanye zaidi na uwe zaidi!

Show more...
1 year ago
18 minutes 16 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
MAKOSA MAKUBWA YANAYOFANYIKA KATIKA MAHUSIANO NA NAMNA YA KUYAEPUKA - Sadaka Gandi #Mapenzi

"Wewe unaamini kwamba huyo mwenzako unampenda kumbe kuna makosa makubwa sana. Twende pamoja tuangalie vijana wanakosea wapi na namna gani ufanye ili kuepuka au kurekebisha makosa." Anasema Bi Sadaka Gandi, mtaalamu wa saikolojia ya familia na mshauri mbobevu katika maswala ya mahusiano. Fuatilia matoleo haya katika H.W TV kwa njia ya YouTube na kwa mfumo sauti kupitia H.W PODCAST. Pia usisite kutuandikia maoni yako ili jukwaa hili liendelee kuwa bora zaidi kwa ajili yako na wafuatiliaji wengine. Tuandikie kupitia hubofwisdomorg@gmail.com au tuma ujumbe wa sauti kwa njia ya WhatsApp kwenda namba 0753825794. Tembelea www.hubofwisdom.com kufahamu zaidi au tuma neno WISDOM kwenda namba 0753825794 uunganishwe katika jamii ya H.W na ushiriki vipindi hivi moja kwa moja. Endelea kujifunza, Endelea kufanya. Tunafurahi sana ukiangalia zaidi lakini tunafurahi mara dufu ukifanya. Nenda duniani ukafanye zaidi na uwe zaidi! #karibu_nyumbani Welcome to the home for positive vibes!

Show more...
1 year ago
12 minutes 53 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
KUONGEZA THAMANI

Hauwi wa thamani kwasababu ya kile unachokipata bali kile unachokitoa. "Kwakuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna, apandaye haba atavuna haba. Apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu."

Kitakachofanya bidhaa zako au huduma zako ziwe za thamani sio gharama yake bali ni manufaa yanayotokana na hiyo huduma. Ili upate faida kubwa kutokana na kile unachokifanya unatakiwa upande mbegu ya thamani. . . Fuatilia mtiririko wa matoleo haya kupitia H.W TV na H.W PODCAST kila wiki. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi. Maoni yako ni ya thamani sana kwetu ili toleo lijalo liwe bora zaidi kwa ajili yako na wafuatiliaji wengine. Tuma ujumbe wako wa maoni kwenda namba 0753825794 au andika barua pepe kwenda hubofwisdomorg@gmail.com . TUNAFURAHI UKISIKILIZA LAKINI TUNAFURAHI ZAIDI UNAPOFANYA, KWAHIYO NENDA DUNIANI UKAFANYE ZAIDI NA KUWA ZAIDI! #karibu_nyumbani

Show more...
1 year ago
9 minutes 29 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
NAMNA SAHIHI YA KUJENGA

"Start Small think Big". Zingatia mambo madogo.

"Start Small, Think Big". Ukifanya vizuri katika uwanda mdogo hata siku ukiwa katika uwanda mkubwa, uwezekano ni kwamba utafanya vizuri. Wakati unapofikiria kujenga mambo makubwa anza kidogokidogo. ....................................................................... Maoni yako ni muhimu na atunayathamini sana, hivyo tuma ujumbe wako wa sauti kwa njia ya WhatsApp nasi tutaumbatanisha katika toleo lijalo au tuandikie kupitia 0753825794 au barua pepe hubofwisdomorg@gmail.com. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi kuhusu program zetu na kuwa sehemu ya jamii hii.

Show more...
1 year ago
4 minutes 12 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
KWANINI MAHUSIANO MENGI YA KIMAPENZI HAYADUMU? - Sarah Ngonyani

Kwa uwazi na utaalamu Mis Sarah anaelezea namna ya kudumisha mahusiano ya kimapenzi. Sikiliza

Show more...
1 year ago
36 minutes 24 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
WATU

"The more hands you shake, the more opportunities you create." Katika hatua za awali za kujenga biashara au asasi uwezekano mkubwa ni kwamba watakaojihusisha na wewe ni watu wanaokufahamu. Vivyo hivyo ili watu wakufungulie milango ya fursa kigezo kimoja wapo kikubwa ni namna gani wanakufahamu. Fuatilia mtiririko wa episode hizi katika YouTube: H.W TV na Podcast: H.W PODCAST kila wiki. Maoni yako ni muhimu na atunayathamini sana, hivyo tuma ujumbe wako wa sauti kwa njia ya WhatsApp nasi tutaumbatanisha katika toleo lijalo au tuandikie kupitia 0753825794 au barua pepe hubofwisdomorg@gmail.com. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi kuhusu program zetu na kuwa sehemu ya jamii hii. Tunapenda sana ukisikiliza, lakini tunapenda zaidi ukifanya. Kwahiyo fanya zaidi na uwe zaidi. Cheers!

Show more...
1 year ago
5 minutes 55 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
MIPANGO

Watu wengi hudhani kuwa wakipata fedha nyingi ndio watafanya mambo fulani makubwa. Lakini ukweli ni kwamba wengi hawana umadhubuti wa matarajio yao, yapo hewani tu. Fuatilia mtiririko wa episode hizi kwa katika YouTube: H.W TV na Podcast: H.W PODCAST kila wiki. Maoni yako ni muhimu na atunayathamini sana, hivyo tuma ujumbe wako wa sauti kwa njia ya WhatsApp nasi tutaumbatanisha katika toleo lijalo au tuandikie kupitia 0753825794 au barua pepe hubofwisdomorg@gmail.com. Tembelea www.hubofwisdom.com/media kufahamu zaidi kuhusu program zetu na kuwa sehemu ya jamii hii. Tunapenda sana ukisikiliza, lakini tunapenda zaidi ukifanya. Kwahiyo fanya zaidi na uwe zaidi. Cheers!

Show more...
1 year ago
1 minute 28 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
SIRI ZA USHINIDI - Halima Kopwe (MISS WORD TZ 2023)

'From a Rough to a Diamond' Mis. Halima Kopwe anaelezea safari yake ya ushindi na kile anachowashauri vijana wengine wenye kiu ya kustawi katika nyanja walizopo. EDITION 4 - THE WISE MEGA MEET-UP (Episode) Tembelea www.hubofwisdom/media kuangalia na kusikiliza zaidi. Toa maoni yako ili jukwaa hili lizidi kuwa bora kwa ajili yako, tumia 0753825794 au tuandikie katika barua pepe hubofwisdom@gmail.com Welcome at the home of positive vibes! #karibu_nyumbani

Show more...
1 year ago
6 minutes 36 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
DONDOO ZA MPENYO WA KIUCHUMI - James Mwang'amba.
"Tunaposema mpenyo wa kifedha maana yake ni kwamba mtu anatoka sehemu moja ya chini na kwenda katika sehemu nyingine ya juu. Ushindani ni mkubwa na hakuna mtu anayejali kwamba unalia au unalalamika. Watu wanataka kuona kwamba unaleta nini mezani." Anasema James Mwang'amba. Fuatilia muhtasari huu wa mazungumzo ili kufahamu dondoo za kukuweka sehemu ya juu kifedha katika eneo lako la kazi au biashara na maisha binafsi. Toa maoni yako kupitia www.hwtz.wordpress.com au tutumie ujumbe wako wa sauti na tutauambatanisha katika toleo lijalo.
Show more...
2 years ago
19 minutes 16 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
MALENGO (Goal Setting) - Anthony Luvanda
Unachotakiwa kufahamu kuhusu malengo. Anthony Luvanda anazungumzia manufaa ya kuweka malengo, sababu zinazowafanya watu wengi wasizingatie kuweka malengo na Kwanini watu wengi wenye malengo wanashindwa kutekeleza. Ufanye mini kuliepuka hilo? Tia maono yako kuhusu toleo hili. Tuma ujumbe wa sauti na kuelezea ulichojifunza nasi tutaambatanisha katika toleo lijalo.
Show more...
2 years ago
38 minutes 12 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
Dina Marios anatoa funzo kubwa kutoka katika historia ya kusisimua ya maisha yake. Hamasika!
Mwanadada Dina ni mmoja wa watu wanaoshangiliwa sana hapa Tanzania. Ameotesha mizizi ya ushawishi kwa hadhira yake kupitia umaridadi alionao katika media na harakati za kuwaleta wanawake wa kitanzania pamoja. Lakini nani ajuaye kuhusu mapito yake na kilichomfanya asimame na kuwa mfano bora hata leo. Hapa anatoa hamasa ya maisha. Mawazo yake juu ya kinachopaswa kufanywa na kila mwanajamii mwenye kiu ya kustawi. Usiache kutoa maoni yako kwa njia ya sauti kupitia link iliyopo hapo chini nasi tutayaambatanisha katika toleo lijalo au tuandikie kupitia 0753825794. Furahi!
Show more...
2 years ago
20 minutes 5 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
MAPENZI YA BLUETOOTH - Irene Kamugisha.
"Connection kwenye mapenzi ni suala la muhimu sana. Inawezekana kufanya mapenzi yakashamiri na yakawa na tija kwa wewe na mwenzako kama kuzingatia mambo haya niyakayoyazungumza hapa." Anasema madam Irene Kamugisha. Mmoja wa washauri bora sana wa masuala ya mahusiano hapa Tanzania.
Show more...
2 years ago
9 minutes 17 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
Mafanikio ya Kifedha | Victor Mwambene - (Kanuni kumi za kutengeneza fedha)
"Mafanikio ya kifedha sio bahati, mafanikio yanakuja kwa kuwa na maarifa sahihi juu ya fedha, kwa juhudi, nidhamu binafsi na kwa kupambana. Mungu ametupa wote neema ila ni tabia zetu, imani na fikra zetu ndio zinazoamua ustawi wetu. Hizi ni kanuni kumi zitakazokujengea uwezo wa kustawi kiuchumi." Anaeleza Mwalimu Victor Mwambene, muelimishaji wa maswala ya fedha na biadhara. Sikiliza kanuni kumi muhimu unazopaswa kuzifahamu na ukitekeleza haya, hautobaki kama ulivyo.
Show more...
2 years ago
18 minutes 21 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
Mkakati wa maendeleo Binafsi - Mosses Raymond (Samora)
Ili mwanadamu aweze kutimiza kusudi la uwepo wake maishani ni lazima atumie na kuboresha uwezo wake binafsi. Kwa kufanya hivyo ndio atakuwa mwenye tija. Mosses Raymond anaeleza ukweli wa maisha, kwanini tujinoe, kwa namna ipi, na namna gani tujiendeleze kibinafsi. Kuwa sehemu ya mijadala hii kwa kutuma neno WISDOM kwenda namba 0753825794.
Show more...
2 years ago
13 minutes 30 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
Kujiandaa kwa ajili ya ndoa - Chris Mauki
"Ndoa ni kama nyumba, msingi usipokuwa mzuri, nyumba haiwi imara."
Show more...
2 years ago
13 minutes 30 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
KUFUNGUA MILANGO YA FURSA ZA KIFEDHA - James Mwang'amba.
Kustawi kifedha na mafanikio ya uchumi kwa ujumla ni matokeo ya maarifa na juhudi zinazoelekezwa katika kutengeneza fursa na kuzitumia. James Mwang'amba ni mtaalamu wa masuala ya biashara na mhamasishaji. Ni mjasiriamali na mbobevu katika masuala ya fedha. Katika episode hii anazungumzia mbinu muhimu za kukua kifedha.
Show more...
3 years ago
10 minutes 36 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
KUOA NA KUOLEWA. Upi ni muda sahihi? Fahamu sababu na namna ya kushulika nazo - Sadaka Gandi.
"Tunaongea habari ya kuoa na kuolewa. Pamoja na kwamba wanasema ndoa haina fomula lakini kuna _best practices_ ambazo ukizifuata utaona matunda." Anasema Aunt Sadaka. Pata kufahamu kuhusu madhara ya kuoa au kuolewa mapema, kuchelewa, sababu zipi hupelekea na namna gani ya kushughulika nazo. Kuwa sehemu ya mijadala hii kwa njia ya whatsApp. Tuma neno WISDOM kwenda namba 0753825794.
Show more...
3 years ago
32 minutes 33 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
Masoud Kipanya - MBINU MBADALA ZA MAENDELEO
Maendeleo ni kitu muhimu na tunahitaji uthubutu na uimara wa kifikra ili tufaulu. "Na ukitaka kufaulu kuliko kwingi, jifunze sana kutokulaumu watu, jifunze kutokutegemea watu. Jifunze kutengeneza njia." Anasema Ally Masoud. "Mambo yote haya yanaanza na fikra ndugu zangu." @masoudkipanya .................................................... Kuwa sehemu ya mijadala hii kwa kutuma neno WISDOM kwenda namba 0853825794. Welcome to the hub of positive vibes #Karibu_nyumbani
Show more...
3 years ago
20 minutes 30 seconds

H.W PODCAST - Positive Vibes!
Ni muda wa kuchukua nafasi yako katika meza ya H.W nasi tutawasilisha kwako mawazo ya thamani kwa maneno ya dhahabu. Mahali pa kwanza na pekee unapohitaji kuwa kwa ajili ya ustawi wako. Karibu tujifunze vingi. Pata nafasi ya kusikiliza mambo ya msingi sana yatakayonoa stadi zako, kukuongezea maarifa na kuchochea maendeleo yako ya kiutu. #Karibu_nyumbani.