All content for Babananiii is the property of Fabian C. Mwakabanje and is served directly from their servers
with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
A literate African empowering the community through literacy programs.
Tujisahihishe, kitabu kiliandikwa na Hayati Baba Wa Taifa Letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania, mwezi Mei mwaka 1962, Dar es Salaam, Tanganyika.
*JINSI YA KUWEKA MIPANGO*
A. Marlene Wilson anasema kwamba mchakato ulioratibiwa unapaswa kuzingatia kanuni zifuatazo:
1. *Malengo;* ni matokeo yanayotazamiwa; mahali ambapo mtu au taasisi inataka kufika -- hatima au maazimio yake.
2. *Maazimio;* kutafsiri malengo na madhumuni kwa njia iliyo wazi na rahisi ya kueleweka na kutekelezeka (wakati mwingine huitwa mipango kazi).
3. *Kazi;* ni mambo gani ya kuyatekeleza ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
4. *Mipango;* ni mbinu na mtiririko wa kazi ili kufikia malengo.
5. *Bajeti* ni sehemu ya mpango iliyoainishwa kitarakimu na kuwekewa kiasi cha fedha.
6. *Ratiba;* ni mpango wenye tarehe za utekelezaji na watumishi wahusika.
7. *Tathmini;* ni kuipima kazi inayofanyika kama vinawiana na mipango iliyowekwa. Kubaini iwapo mpango umefikia malengo yaliyokusudiwa.
B: Ili timu iwe na tija ni sharti mipango au kazi ifafanuliwe waziwazi - iandikwe.
1. Mungu ni Mungu anayekusudia na kutenda mambo yake (Isaya 46:11).
2. Mfano wa Wanawali kumi: watano waliojiandaa na watano wapumbavu (Mathayo 25:1-13)
3.Tunajifunza Daudi alivyoandaa mpango wa kulirejesha sanduku lakini uliokuwa kinyume na mpango wa Mungu (1 Nyakati 13:1-15:19; Kutoka 25:10-15)
JINSI YA KUANZISHA HUDUMA ZENYE TIJA (VIJANA)
Gharama ya ulinzi ni ya asili na kubwa sana kwa mwanadamu. Anahitaji kuwa salama, na mali zake kuwa katika ulinzi na usalama. Ndiyo dhima ya sehemu hii ya Saba (7) katika mfululizo wa simulizi ya TAJIRI WA BABELI.
"Zawadi uliyopewa na mfalme inatakiwa kukufundisha hekima. Ukitaka kubaki na vipande vyako hamsini
vya dhahabu, unatakiwa kuwa makini. Utavutiwa na vitu vingi na utapata ushauri mwingi sana.
Utaambiwa fursa nyingi zinazodaiwa kutoa faida kubwa. Habari na hadithi kutoka kwenye sanduku langu
la dhamana zinatakiwa kuwa onyo kwako. Kabla hujaruhusu pesa yako kutoka kwenye pochi hakikisha
utaweza kuirudisha. Kama utahitaji ushauri zaidi unaweza kurudi nami nitafurahi kukupatia.
'''Mwisho naomba usome nilichoandika. Chini ya mfuniko wa sanduku la dhamana. Maneno haya yana
faida kwa mkopeshaji na mkopaji pia.
Bora tahadhari kidogo kuliko majuto makubwa.
"Ukiambiwa uchague kati ya mfuko uliojaa dhahabu na mabamba ya vigae yaliyoandikwa maneno ya
hekima na busara, utachagua nini?"
Wasikilizaji walikuwa wamekaa jangwani wakiwa wamekusanyika kuzunguka moto. Walikuwa
wakisikiliza kwa makini. Mwanga wa moto ulionyesha nyuso zao ambazo zilianza kuwa nyeusi sababu ya
jua la jangwani.
"Dhahabu, dhahabu," walijibu wote ishirini na saba kwa pamoja.
Mzee Kalabab alitabasamu kama vile kuna siri anaifahamu yeye peke yake.
Hizi ndizo jumla ya tiba saba za pochi tupu. Kwahiyo tiba ya saba na ya mwisho ya kutibu pochi tupu ni kuwa mtu bora. Kujifunza na kujizoeza kupata maarifa zaidi, kupata ujuzi zaidi na kujiendesha maisha yako kwa heshima. Hapo unaweza kujiamini na utaweza kutimiza malengo yako.