Siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA (International Girls in ICT Day) huadhimishwa kila Alhamisi ya nne ya mwezi Aprili kila mwaka. Hii inafuatia makubaliano ya nchi wanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU), kuhimiza wasichana kupenda kusoma masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, kwa kifupisho cha kiingereza –STEM, yaani Science, Technology, Engineering and Mathematics. Nchi wanachama wa ITU pia zilikubaliana kuhamasisha Wasichana na Wanawake kushiriki kwe...
Show more...