
Ulimwengu wa Mkristo ni kipindi ambacho kinakuletea mkusanyiko wa mambo tofauti hususani habari na matukio yanayojiri katika ulimwengu huu na kuligusa moja kwa moja Kanisa la Yesu Kristo. Katika kufuatilia kipindi hiki, utapata kuyafahamu mambo mengi yanayojiri na pengine kukupa neema ya kujiimarisha kiroho wakati Kanisa likipita katika vipindi tofauti na vigumu, hususani kipindi hiki cha nyakati za siku za mwisho.