
Washirika wa Kanisa la Rhema Outreach Ministries Kyabajwa, walipata nafasi ya kufika kwenye Studio za Redio Rumuli kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kujitolea, ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa mazingira. Kitendo hiki kiliwabariki zaidi watendakazi wa Kituo hiki, na zaidi ya yote watumishi hao wakapata nafasi ya kueleza kuhusu msukumo wa wao kufanya hivyo. Karibu upate kusikiliza shuhuda zilizomo kwenye rekodi hii kwa baraka zaidi.