
Msaada utokao Mbinguni ni kipindi ambacho kinamsaidia msikilizaji kuutazama msaada wa Mungu ambao huyafanya yale yaliyoshindikana na kumpa upenyo wa namna ya kiMungu katika kuuendea ushindi aliokusudiwa na Mungu mwenyewe. Katika Kipindi hiki, utapata kusikia na kufahamu Baraka za Mungu zitokanazo na kazi ya msalaba wa Yesu Kristo kwa wanandamu wote, ushindi uliomo pamoja na wokovu uliopatikana Kalvari kwa kifo cha Yesu Kristo.