
Marehemu CPWAA anatajwa kama mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya muziki wa Crank (KING OF BONGO FLEVA CRANK) kupitia ngoma ya PWAA iliyotayarishwa na LUCCI chini ya Mawingu Studio. Hii inamaanisha kuwa Lucci ni mmoja wa waandaaji wa kwanza kwa muziki wa Bongo Fleva wenye mahadhi ya Crank. Mbali na kutayarisha muziki vilevile Lucci anasimama kama msanii baada ya kushiriki kwenye nyimbo kadhaa mfano Kaka na Dada aliyoshirikishwa na Jokate ambae kwasasa ni Katibu Mkuu wa UWT kupitia chama cha CCM.