Umeshawahi kujiuliza kwanini mpaka leo kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva kina uchache wa Magwiji katika mixing & mastering??? Majina kama Laizer, Mixing killer, Chizan Brain n.k yanatajwa kwa kujirudia kwenye nyimbo za wasanii wengi kwasasababu ni wao tu ndo walioamua kujiongeza kwa kupata knowledge ya ukamilishaji wa project za Audio.Naomba nikukaribishe kwenye ulimwengu wa Chizan Brain, kijana mzaliwa wa Ifakara, Hospitali ya Mtakatifu Francisi, akakulia Tanzania, mpaka alipohamia Kenya kwa Baba yake kumalizia elimu yake sekondari na chuo. Na ndiko aliko anzia safari yake ya muziki kwani Mzee wake pia ni mwanamuziki hodari katika kupiga vyombo takribani vyote, gitaa likiwa ndio chaguo lake la muda mwingi. Akiwa moja wapo wa waanzilishi wa Ukoo flani, akapita studio kadhaa Kenya na muda ulipo fika akahamishia makazi yake nchini Tanzania na kuendelea kukinukisha kwenye tansia ya Muziki wa kizazi kipya. Mezani, Chizan amefunguka kwa kina kuhusu safari yake nzima ya mziki. Karibu ujumuike nasi mezani kumfahamu mkali huyu!!
AshaBaraka ni nani? Asha Baraka ni ASHA BARAKA. Unaweza kwenda mbali zaidi ukamuitaMama wa muziki wa dansi Tanzania na usiwe umemzidishia sifa. Asha Barakamwanamichezo kutoka Tabora Girls, Bima hadi kua kocha wa Netball(mpira wapete).
Lakinileo tunakubaribisha kwenye safari yake kama mwanamke wa kwanza kumiliki bendiya muziki wa dansi Tanzania na mtanzania pekee ambae anaweza sema asilimiakubwa ya wanamuziki wanaofanya mziki wa dansi leo hii wamepita chini ya uongoziwake, iwe ni bendi au chuo cha kufundishia muziki.
Jeni nani walikua wasanii wa kwanza kabisa Twanga? Banza Stone alikua mahirikiasi gani? Unafahamu Luiza Mbutu alifika fikaje Twanga? Kwanini Ally Chokianaitwa kinanda?
Yotehaya ameyanyoosha kuweka rekodi sawa. Na ziada si haba. Karibu mezaniumsikilize The Ironylady, Mama, Bibi, Mkurugenzi na Chairman ila sisi tunamuitaNguzo kubwa ya mziki wa dansi Tanzania.
Kama ulishawahi kuisikia ile story ya mtangazaji wa kwanza kucheza wimbo wa Bongo Fleva kwenye radio. Mtangazaji huyo, leo amepata nafasi ya kutubariki na historia yake. Jinsi alivyochangia muziki huu kuwa kimbilio la vijana wengi sana kama sehemu ya ajira yao.
Jina lake kamili ni Taji George Liundi au MASTER T kama alivyobatizwa na Charles Hillary. Kuanzia alivyoanza kutangaza Redio One, moja ya vipindi vyake vya awali kabisa cha DJ Show, kabla ya kuwaachia mikoba wakina Mike Mhagama baada ya kuikacha Redio one na kwenda kufanya kazi kwenye media zingine.
Karibu mezani umfahamu zaidi.
Marehemu CPWAA anatajwa kama mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya muziki wa Crank (KING OF BONGO FLEVA CRANK) kupitia ngoma ya PWAA iliyotayarishwa na LUCCI chini ya Mawingu Studio. Hii inamaanisha kuwa Lucci ni mmoja wa waandaaji wa kwanza kwa muziki wa Bongo Fleva wenye mahadhi ya Crank. Mbali na kutayarisha muziki vilevile Lucci anasimama kama msanii baada ya kushiriki kwenye nyimbo kadhaa mfano Kaka na Dada aliyoshirikishwa na Jokate ambae kwasasa ni Katibu Mkuu wa UWT kupitia chama cha CCM.
Bado kiwanda cha Bongo Fleva kinaendelea kukumbuka mchango mkubwa wa vijana walioiwakilisha Dodoma mwanzoni mwa mwaka 2001 kupitia ngoma zao kadhaa ambazo zinachezwa na kusikilizwa mpaka hivi sasa.
Wanaitwa Chemba Squad, ambapo ndani yake majina kama Noorah aka Baba stylz, Dark Master, Albert Mangwea na Mez B wa area C yalitajwa kuunda kundi hilo.
Ngoma kama Ice Cream, Ghetto langu na Kama Vipi zinatajwa kama ngoma bora za muda wote kutoka kwa wakali hao ambapo hivi sasa wamebaki wawili tu (Noorah yupo zake Shy Town na Dark Master akiwa Dar es salaam) huku bahati mbaya Ngwea na Mez B wakiwa ni marehemu (RIP).
Leo tunakusogezea historia kamili na mengi usiyoyajua kuhusu Dark Master aka MwanaChemba.
Je Unamfahamu FERUZI MRISHO? Gwiji na moja wa waanzilishi na NUNDA mkuu wa DAZ NUNDAZ. Mwenyewe akitambulika zaidi kama Kamanda kabla Kamanda haijawa THE ANTHEM it is now. Leo tuko nae mezani akitusimulia safari yake yote ya mziki, toka anaandikiwa mashairi na dada yake Achane mpaka anatunga tungo matata kama Starehe, Kamanda, Nitafanya Nini, Jirushe, Elimu dunia N.K. Karibu Mezani.
Je, Unamfahamu producer ambaye, dare I say it, bila yeye labda kwaya au bendi yako maarufu usingeisikia kama ulivyoisikia? Producer ambaye amefanya zaidi ya 80% ya production ya mziki wote wa bendi na kwaya Tanzania kwa miaka 30. Marlon Linje, bonge la mshika dau, leo yupo nawe mezani, karibu.
Sehemu ya pili ya maongezi yetu na KBC, ambaye wengi wanamfahamu kama Kibacha
Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania.
Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa.
Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT.
Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo.
Mwamba huyu hapa 😊
#MezaniNaKBC
#MezaHuru
Anaitwa KBC, wengi wanamfahamu kama Kibacha
Huyu ni mojawapo wa mwamba muhimu wa Hip Hop ya Tanzania.
Unaambiwa zama zake, Kipaza kilimuogopa kama ukoma, Rafiki wa mashairi na mchenguaji mashuhuri. Gwiji wa mtindo huru na Battle Emcee haswaaa.
Kibacha ni miongoni mwa waanzilishi wa Kundi kongwe na mahiri la KWANZA UNIT.
Ametupa heshima kubwa ya kukaa nasi na kutupa historia ya muziki wake tangu miaka ya 80 mpaka hapa tulipo.
Jumuika nasi mezani kumsikiliza Mwamba huyu hapa 😊
#MezaniNaKBC
#MezaHuru
KR Mullah ,miongoni mwa waasisi wa GWM (Gangstaz With Matatizo), Wachuja Nafaka, TMK Wanaume family
Mwamba huyu kutokea Temeke Dar es Salaam amefanya makubwa sana katika muziki wetu kabla haujaanza kuwa rasmi
Amefanya kazi na wakongwe kama Boniluv, Master Jay na P Funk.
Ametupatia heshima kubwa ya kutupa simulizi yake tangu akiwa kijana mdogo katika muziki mpaka sasa bado anawakilisha Temeke popote pale alipo
Muite KR Mullah Jibaba Muziki Mkubwa CD Mia Saba Njoo kichwa kichwa akupe za uso saba.
#MezaniNaKakaRashidi
#MezaHuru
Ras Innocent Nganyagwa ni miongoni mwa wanamuziki nguli katika kizazi cha tatu cha muziki wa Reggae kutoka Tanzania.
Muziki wa Reggae Afrika ulianza kushamiri baada ya Uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa za mwanzo kupata mapokeo ya muziki huo.
Tumezungumza na Ras Inno kuhusu imani ya RastaFari, muziki wa Reggae
Ras Innocent Richard Nganyagwa ni shule haswa, Ana ufahamu mkubwa sana wa maisha ya asili ya mwafrika na anaamini kila mtu mweusi ni Rastafarian. Ras Inno ni mtetezi wa haki za binadamu na za wasanii pia,
Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu.
#MezaniNaRasInno
#MezaHuru
Anchor - https://anchor.fm/meza-huru
Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0...
Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683
Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...
Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797
Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...
Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087
Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...
YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...
Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...
Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Carola Kinasha, ukimuona huwezi kuamini ana miongo sita duniani. First lady wa Bene Bene na baadaye Shada.
Msomi wa chuo kikuu aliyechagua kufanya muziki kama kazi. Mwanaharakati wa mwanzo kabisa wa stahiki na haki za utunzi, na moja walioupeleka mbali sana muziki wa asili ya Afrika. Ni mcheshi na mwenye maarifa mengi sana kuhusu maisha na safari ya muziki wetu tangu miaka ya themanini mpaka leo hii.
Unajua kisa chake na Remmy Ongala kilichozaa kibao maarufu cha Karola? Unajua nini maana ya segese?
Unajua kwamba yeye ni mtu aliyekuwa nyuma ya chorus nzuri na tamu za Bongofleva yetu hii? Carola Kinasha ni nyota wa muziki wetu na Almasi inayowaka kama taa.
Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu
#MezaniNaCarolaKinasha
#MezaHuru
Anchor - https://anchor.fm/meza-huru
Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0...
Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683
Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...
Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797
Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...
Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087
Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...
YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...
Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...
Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Wengi wanamjua kwa jina la Mnyalu, Mike Tee, The Dangerous Emcee ila jina lake kamili ni Mike Francis Mwakatundu.
Mike Tee alianza kuimba mwanzoni mwa miaka ya 90, akiimba kwaya kanisani na taratibu akaanza kujifunza kuandika na kuimba mistari kupitia mashairi ya gazetini baada ya kukutana na Ntwa mmoja wa waanzilishi wa WWA (Wagumu Weusi Asilia).
Amefanya kazi na watayarishaji kama P Funk na Master Jay, amefanya hits na wasanii kama Juma Nature, Q Chief, Mad Ice na Komando Jide
Unajua kuhusu ugomvi wa Mr. Nice na Dudu Baya? Mike Tee amenyoosha taarifa. Sitaki kumalizia stori yake. Jumuika nasi mezani umsikilize, Karibu
#MezaniNaMikeTee
#MezaHuru
Anchor - https://anchor.fm/meza-huru
Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0...
Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683
Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...
Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797
Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...
Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087
Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...
YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...
Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...
Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Mzee Kitime ama Ango "Uncle" Kitime kama mwenyewe anavyojitanabaisha kwenye mitandao. Ni mwanamuziki nguli wa Muziki wa Dansi kutoka Kilimanjaro Band maarufu kama "Wana Njenje", mmoja wa wanakamati ya kutetea muziki wa dansi na tasnia ya muziki kwa ujumla, Mtangazaji wa Radio, Muigizaji wa Filamu, Mchekeshaji na Mtunza historia ya Music wa Tanzania.
Tumekaa naye na kupata historia ya muziki wake na harakati zake tangu mwaka 1967 hadi leo akiwa na JFK BAND.
Jumuika nasi mezani tumsikilize Gwiji huyu wa Tasnia yetu, Karibu.
#MezaniNaJOHNKITIME
#MezaHuru
Sehemu ya pili ya maongezi na Master Jay. Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji
Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu
Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini 😁
Tumepata nafasi ya kuzungumza naye na ametupa simulizi ambazo zinaweza kutumika kama chanzo rasmi cha historia za muziki wetu kuanzia mwanzo mpaka tulipo.
Jumuika nasi mezani, tusikilize PART II ya MTABE huyu wa sanaa 😉 Karibu.
#MezaniNaMasterJay
#MezaHuru
Anchor - https://anchor.fm/meza-huru
Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0...
Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683
Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...
Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797
Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...
Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087
Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...
YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...
Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...
Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Nani asiyemfahamu Master Jay? Kama hujasikiliza nyimbo alizotengeneza (naamini ni vigumu), utakuwa umemuona kwenye mashindano ya kusaka vipaji
Joachim Marunda Kimaryo ni Gwiji kabisa katika tasnia ya muziki wetu
Amehusika katika Hip Hop, Bongofleva, Dansi mpaka nyimbo za Dini 😁
Tumepata nafasi ya kuzungumza naye na ametupa simulizi ambazo zinaweza kutumika kama chanzo rasmi cha historia za muziki wetu kuanzia mwanzo mpaka tulipo.
Jumuika nasi mezani, tusikilize PART I ya MTABE huyu wa sanaa 😉 Karibu.
#MezaniNaMasterJay
#MezaHuru
Anchor - https://anchor.fm/meza-huru
Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0...
Apple Podcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683
Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...
Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797
Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...
Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087
Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...
YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...
Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...
Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Sehemu ya pili na Kaka Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv. Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya muziki na maisha tangu miaka hiyo mpaka leo. Jumuika nasi mezani, tusikilize PART II ya Poppaluv 😉 Karibu. #MezaniNaBoniluv #MezaHuru
Anchor - https://anchor.fm/meza-huru
Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0...
Applepodcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683
Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...
Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797
Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...
Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087
Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...
YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...
Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...
Twitter - https://twitter.com/MezaHuru
Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya muziki na maisha tangu miaka hiyo mpaka leo. Jumuika nasi mezani, tumsikilize Poppaluv 😉 Karibu.
#MezaniNaBoniluv