Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia mradi wa TANZIE huko Chuo Kikuu Mzumbe, mkoani Morogoro, mashariki mwa Tanzania, unaolenga kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na uchambuzi wa neno la wiki.
- Mamilioni ya watu nchini Jamaica na katika ukanda wote wa Karibea wanajiandaa kukabiliana na madhara makubwa ya kimbunga Melissa huku Umoja wa Mataifa na washirika wake wakionya kuhusu tishio kubwa na la haraka la kibinadamu.
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameelezea wasiwasi wake mkubwa kufuatia kuongezeka kwa mapigano ya kijeshi mjini El Fasher, jimbo la Darfur Kaskazini, nchini Sudan. Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wake usiku wa tarehe27 Oktoba 2025 kwa saa za New York marekani, Guterres amesema kwa zaidi ya miezi kumi na minane, wakazi wa El Fasher na maeneo ya jirani wamekuwa wakikabiliwa na mateso makubwa huku makundi ya Wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) yakizingira mji huo.
- Na hii leo, Ofisi ya Umoja wa Matiafa ya Haki za Binadamu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Usaidizi nchini Afghanistan wamechapisha waraka wa taarifa kuhusu madhara makubwa ya kina za haki za binadamu yaliyotokana na kusitishwa kwa huduma za mawasiliano nchini Afghanistan tarehe 29 Septemba hadi tarehe mosi mwezi huu, — hatua ambayo imezidisha changamoto nyingi ambazo tayari zinawakabili wananchi.
- Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno "KIMBIMBI"
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!