All content for FRANSISCO MAGNETICS is the property of Fransisco Magnetics and is served directly from their servers
with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Kuna Kelele nyingi sana ambazo zinawakatisha tamaa watu wengi kwenye biashara au vitu wanavyoviamini. SIRJEFF Denis anakabiliana nazo vipi mpaka kufika pale alipo. Alianzaje safari yake ya biashara mpaka kuwa hapa alipo leo? Kwanini tunaona ananata sana na kujisikia? Ukweli juu ya hili ni upi?
Kumekuwa na mkanganyiko na mvutano mkubwa kuhusu strategies gani ni nzuri kupita nyingine na wengine wameenda mbali mpaka kudharau watu wanotumia strategy fulani huku wakijitutumua kuwa strategies wanazitumia ni bora kuliko za watu wengine. Nini ukweli katika hili? . Nimekaa na rafiki yangu Elisha Chengula na ameelezea kwa umakini kuhusu hili. Karibu
Saikolojia inachukua nafasi kubwa sana kwenye biashara ya forex. Watu wengi wamekua wakijikuta kwenye wakati mgumu pindi hisia zikiingia wanapotrade na kujikuta wanarudia makosa hayo hayo mara kwa mara. Mimi na rafiki yangu Under30 Millionaire tumefanya majadiliano ni kwa namna gani unaweza kutoka kwenye huu mtego.
Kila msimu unakua na tabia tofauti sokoni. Jambo la msingi ni kuhakikisha unakuwa flexible kuzingatia msimu upi utahitaji nini ili kuwa katika mazingira salama. Hapa tumechambua na kueleza Uncertainity principles na Market most fundamental characteristics hasa kipindi hiki cha janga la Corona ambazo zina-athiri soko la Forex pia.
Umewahi kujiuliza kuhusu Aina mpya ya biashara au makampuni iliyo katika mfumo wa startUp inavyofanya kazi!? Kwanini mfumo huu unatrend sana kote duniani kwa sasa!? Na nini tofauti yake na aina mifumo mingine ambayo imezoeleka kama small, medium na cooperate business. Sikiliza hii podcast kuelewa zaidi.
Namshukuru sana rafiki yangu Nkonya Maduhu (Francis CEO) kukubali wito wa kufanya nae Podcast ili kuelezea zaidi usalama katika hii biashara, aina gani ya broker umtumie na vigezo gani vya kuangalia. Je ukitaka kufungua kampuni ya Forex Afrika Mashariki vitu gani uangalie na masuala ya insurance katika kampuni na wawekezaji wako.
Umeshawahi kujiuliza ni kwa namna gani kutimiza ahadi kutakutengenezea mahusiano mazuri baina yako na hii biashara!? Unajua ni kwa namna gani kushindwa kutimiza ahadi kutakugharimu katika hii biashara!? Sikiliza hii Episode.