Wengi huitazama hisia ya Upweke kwa mtazamo hasi lakini episode hii itakufundisha namna ya kuitazama hisia kama fursa ya kutambua mahusiano sahihi kwako pamoja na mbinu ya kukabiliana na Upweke. Zaidi utajifunza kupitia maisha ya Education Specialist Remi ambaye alikabiliana na changamoto hii ya upweke.
Fahamu zaidi kutoka kwa mwanasaikolojia mzoefu kuhusu stress na njia bora za kukabiliana nayo. Na kwa namna ya kipekee jinsi Stress ilivyogeuka kuwa Fursa na kubadilisha maisha Banker mzoefu, bwana Stephen Matinya.
Hofu ni sawa na alarm ya mwili kwenye maisha, ikitoa taarifa za hatari na kukumbusha yale yalio muhimu zaidi. Sikiliza episode hii ufahamu zaidi kutoka kwa Mwanasaikolojia mzoefu ni kwa namna gani Hofu huifanya kazi hiyo ya alarm pamoja na mengine muhimu kuhusu hisia ya Hofu.
Sikiliza kufahamu namna Emotional Intelligence invyoweza kuwa Baraka kubwa kwenye Ajir ama Biashara yako kupitia faida zake. Pia utapata muongozo kutoka kwa Mwanasaikolojia mzoefu wa namna gani unaweza kuitumia Emotional Intelligence kwa tija kwenye Ajira au Biashara yako.
Fuatilia episode hii kujifunza kama mzazi unawezaje kuikaribisha Emotional Intelligence kwenye Familia yako na manufaa yake kwako na kwa familia ni yapi?
Fahamu namna ambavyo unaweza kuitumia Emotional Intelligence kutatua changamoto mbalimbali kwenye mahusiano yako ya kimapenzi.
Fahamu mbinu ya kujifanyia tathmini kihisia ili kujua vyanzo na masuluhisho ya changamoto mbalimbali unazopitia kihisia.
Fahamu kutoka kwa mwanasakolojia mzoefu kuhusu maana ya Akili Hisia (Emotional Intelligence), tofauti kati ya Emotions na Feelings, nguzo za kuijenga Akili Hisia pamoja na faida zake kwenye maisha yako.