Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Society & Culture
Business
News
Sports
TV & Film
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
Podjoint Logo
US
00:00 / 00:00
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts113/v4/5d/19/9f/5d199f1d-c91d-9c74-f4d8-5ab29ffe8083/mza_11480740572108446565.jpg/600x600bb.jpg
Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
The New Life Mission
30 episodes
9 months ago
Haki ya Mungu ipo wazi na ni tofauti kabisa na haki za wanadamu. Haki ya Mungu imefunuliwa katika injili ya maji na Roho ambayo ilitimizwa kwa ubatizo wa Yesu toka kwa Yohana na damu yake Msalabani. Tunapaswa kurudi katika imani inayoamini katika haki ya Mungu kabla hatujachelewa. Je, unafahamu ni kwa nini ilimpasa Yesu kubatizwa na Yohana Mbatizaji? Ikiwa Yohana asingelimbatiza Yesu, basi dhambi zetu zingekuwa hazikupitishwa kwa Yesu. Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye mkuu kuliko wanadamu wote, na ule ubatizo ambao alimpatia Yesu ulikuwa ni sharti muhimu la Mungu ili kuweza kuzipitisha dhambi zetu toka kwetu kwenda kwa Yesu. Yesu alibatizwa ili kuzibeba dhambi zote za ulimwengu katika mabega yake, kisha aliimwaga damu yake Msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi hizo zote. Mambo haya yote yamebadilisha kikamilifu uelewa wangu wa zamani juu ya kuzaliwa tena upya wakati nilipokuwa nikifahamu juu ya damu ya Msalaba tu. Kwa sasa Mungu ametufundisha juu ya haki ya Mungu jinsi ilivyo ili kwamba tuweze kufahamu na kuamini kikamilifu katika haki yake. Ninamshukuru Bwana kwa baraka hizi zote. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
Christianity
Religion & Spirituality
RSS
All content for Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II) is the property of The New Life Mission and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Haki ya Mungu ipo wazi na ni tofauti kabisa na haki za wanadamu. Haki ya Mungu imefunuliwa katika injili ya maji na Roho ambayo ilitimizwa kwa ubatizo wa Yesu toka kwa Yohana na damu yake Msalabani. Tunapaswa kurudi katika imani inayoamini katika haki ya Mungu kabla hatujachelewa. Je, unafahamu ni kwa nini ilimpasa Yesu kubatizwa na Yohana Mbatizaji? Ikiwa Yohana asingelimbatiza Yesu, basi dhambi zetu zingekuwa hazikupitishwa kwa Yesu. Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye mkuu kuliko wanadamu wote, na ule ubatizo ambao alimpatia Yesu ulikuwa ni sharti muhimu la Mungu ili kuweza kuzipitisha dhambi zetu toka kwetu kwenda kwa Yesu. Yesu alibatizwa ili kuzibeba dhambi zote za ulimwengu katika mabega yake, kisha aliimwaga damu yake Msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi hizo zote. Mambo haya yote yamebadilisha kikamilifu uelewa wangu wa zamani juu ya kuzaliwa tena upya wakati nilipokuwa nikifahamu juu ya damu ya Msalaba tu. Kwa sasa Mungu ametufundisha juu ya haki ya Mungu jinsi ilivyo ili kwamba tuweze kufahamu na kuamini kikamilifu katika haki yake. Ninamshukuru Bwana kwa baraka hizi zote. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
Christianity
Religion & Spirituality
Episodes (20/30)
Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 7-1. Utangulizi Kwa Sura ya 7
Kwa kuutambua ukweli kuwa kabla ya ukombozi wake mwili wake ulikuwa umehukumiwa kifo na Sheria ya Mungu, basi ndio maana Mtume Paulo alilifanya ungamo lake kwa kuamini kuwa alikuwa ameifia dhambi katika Yesu Kristo. Kabla hatujakutana na haki ya Mungu—yaani kabla hatujazaliwa upya—sisi ambao tunamwamini Kristo tulizoea kuishi chini ya himaya na laana ya Sheria. Hivyo, ikiwa tusingekutana na Yesu ambaye ametuletea haki ya Mungu basi Sheria ingeendelea kututawala. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
18 minutes 49 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 7-2. Kiini cha Imani ya Paulo: Ungana na Kristo Baada ya Kuifia Dhambi (Warumi 7:1-4)
Je, umewahi kuona bunda la nyuzi zilizojisokota? Ikiwa unajaribu kuifahamu sura hii pasipo kuufahamu ukweli wa ubatizo wa Yesu ambao Mtume Paulo aliuamini, basi ni hakika kuwa imani yako itakuwa katika wakati mgumu kuliko hapo kabla. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
49 minutes 56 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 7-3. Sababu Inayotufanya Tumsifu Bwana (Warumi 7:5-13)
Ninamsifu Bwana ambaye ameniongoza hadi kuonana na ninyi watu wa Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa kweli ninamshukuru sana Mungu kwa kunibariki na kunifanya niishi maisha yenye furaha hadi leo hii. Mungu ameendelea kuwa pamoja nami na amekuwa akinihurumia ingawa kulikuwa na nyakati ambazo nilikuwa najisikia kukatishwa tamaa, nyakati ambazo nilikutana na magumu na kupata udhaifu ndani yangu katika vipindi mbalimbali. Mungu amekuwa makini na amekuwa upande wangu katika maisha yangu yote katika shida na katika furaha. Hakukuwa na wakati wowote ambapo Mungu aliniacha hata kwa sekunde moja. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
29 minutes 27 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 7-4. Miili Yetu Ambayo Inautumikia Mwili Tu (Warumi 7:14-25)
Sisi hatuwezi kufanya jambo lolote ikiwa Mungu hatendi kazi akiwa upande wetu. Mungu wetu anatutunza na anatusaidia. Hebu tuliangalie Neno la Mungu. Warumi 7:14-25 inatueleza sisi kuwa Mtume Paulo alijiona yeye mwenyewe kuwa anaishi katika mwili hali akiwa ameuzwa chini ya dhambi. Pia aligundua kuwa kwa sababu ya sheria mwili hauwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kufanya dhambi muda wote atakapokuwa hai. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
32 minutes 23 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 7-5. Mwili Unaitumikia Sheria ya Dhambi (Warumi 7:24-25)
Biblia inatueleza sisi pia kuwa, “kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” Na hizo ndio sheria zinazotutawala. Mioyo yetu imeumbwa kumpenda Mungu na kuupenda ukweli, lakini ni kawaida kwa mwili kuitumikia sheria ya dhambi. Neno la Mungu linatueleza sisi kuwa moyo unaitumikia injili na haki ya Mungu ilhali mwili unaitumikia dhambi tu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
38 minutes 38 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 7-6. Tumsifu Bwana, Mwokozi wa Wenye Dhambi (Warumi 7:14-8:2)
Wanadamu wote walirithi dhambi toka kwa Adamu na Hawa na wakafanyika kuwa mbegu ya dhambi. Hivyo sisi ni viumbe wenye dhambi. Kwa asili tunazaliwa kama uzao wa dhambi na hivyo tunajikuta ni viumbe wenye dhambi. Watu wote duniani hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kuwa wenye dhambi kwa sababu ya baba yetu wa kwanza Adamu ingawa hakuna yeyote anayetaka kuwa mwenye dhambi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
45 minutes 17 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-1. Utangulizi Kwa Sura ya 8
Pengine sura ya 8 inaweza kuelezewa kuwa ni sura muhimu sana miongoni mwa sura kadhaa za kitabu hiki cha Warumi. Paulo anatufunulia jinsi ambavyo haki ya Mungu ilivyo ya kushangaza kwa kupitia mada mbalimbali ambazo zinapatikana katika kitabu hiki. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
6 minutes 28 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-2. Haki ya Mungu, Utimilifu wa Hitaji la Sheria Kwa Mwenye Haki (Warumi 8:1-4)
Warumi 8:1-4 inatueleza sisi juu ya aina ya imani ambayo wale walio katika Kristo wanayo. Siri ya kifungu hiki ni kwamba tunaweza kukutana na maagizo yote ya Sheria katika haki ya Mungu kwa imani yetu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
33 minutes 44 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-3. Mkristo ni Nani? (Warumi 8:9-11)
Ikiwa mtu ni Mkristo wa kweli au la mtu huyo anatofautishwa kwa kigezo ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yake au la. Inawezakanaje kwa mtu kuwa Mkristo ikiwa mtu huyo hana Roho Mtakatifu katika moyo wake? Paulo anatueleza sisi kuwa hata kama tunamwamini Yesu hilo sio suala muhimu sana bali ikiwa tunamwamini Yesu hali tukiwa tumeigundua haki ya Mungu au la. Imani ya kweli inayohitajika kwa watakatifu ni ile imani ambayo iko tayari kupokea na kufanywa makao ya Roho Mtakatifu. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndio unaoweza kukutambulisha ikiwa wewe ni Mkristo au la. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
4 minutes 2 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-4. Kuwa na Mawazo ya Kimwili ni Kifo, Bali Kuwa na Mawazo ya Kiroho ni Uzima na Amani (Warumi 8:4-11)
Watu wamekuwa wakiteseka kwa karne tano zilizopita hali wakidanganywa na mafundisho potofu ya kiimani kama vile Fundisho la Utakatifu Unaozidi, Fundisho la Kuhesabiwa Haki kwa Imani, na mafundisho mengine ambayo yanasisitiza kuwa ukombozi unawezekana kwa kupitia sala za toba. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
32 minutes 30 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-5. Kutembea Katika Haki ya Mungu (Warumi 8:12-16)
Mtume Paulo, kama mtu aliyepokea wokovu toka kwa Mungu alisema kuwa wale waliozaliwa tena upya hawapaswi kuishi kwa jinsi ya mwili bali kwa jinsi ya Roho. Hasahasa Paulo alisema kuwa ikiwa sisi ambao tunayo haki ya Mungu tutaishi kwa jinsi ya mwili basi tutakufa, na kwamba kama tutaishi kwa jinsi ya Roho basi tutaishi. Hivyo ni lazima tuamini katika ukweli huu. Je, inakuwaje basi kwa wale wanaoamini katika haki ya Mungu? Je, wanapaswa kuishi kwa mujibu wa haki ya Mungu au kwa tamaa ya mwili? Ni lazima watambue kile kilicho sahihi na kisha waiadabishe miili yao ili kujitoa kwa kazi za haki ya Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
8 minutes 23 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-6. Wale Waurithio Ufalme wa Mungu (Warumi 8:16-27)
Watu wote ambao wamesamehewa dhambi zao wanaamini katika injili ya maji na Roho na wana Roho Mtakatifu katika mioyo yao. Katika 1 Yohana 5:10 Biblia inasema, “Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake”. Yeye aliye na haki ya Mungu katika moyo wake anaye huyo Roho Mtakatifu ndani yake, na ni imani katika injili ya maji na Roho inayomfanya Roho Mtakatifu aweze kukaa milele katika moyo wa mtu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
45 minutes 17 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-7. Kuja Kwa Bwana Mara ya Pili na Ufalme wa Milenia (Warumi 8:18-25)
Wale ambao ni wenye haki kwa kuamini katika haki ya Mungu basi hao wameupokea utukufu wa mbinguni. Hii ndiyo sababu wanateseka pamoja na injili ya maji na Roho ya Yesu ili kuwavika watu wote kwa utukufu huo wa mbinguni. Waamini wanajitoa wao wenyewe kwa injili ya haki ya Mungu na kisha wanateseka hapa duniani kwa sababu kushiriki katika mateso ya Kristo ni utukufu na haki. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
16 minutes 15 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-8. Roho Mtakatifu Anayewasaidia Wenye Haki (Warumi 8:26-28)
Roho Mtakatifu yumo katika mioyo ya wale wanaoamini katika haki ya Mungu. Roho Mtakatifu anawafanya wao kuomba na anawasaidia kufanya hivyo. Pia Roho Mtakatifu huugua kwa kufanya maombi kwa niaba yao kusikoweza kutamkwa. Hii ina maanisha kuwa Roho Mtakatifu anawasaidia kuomba kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo sababu wale wanaoamini katika haki ya Mungu wanaitwa wana wa Mungu. Bwana anawaahidia wao kuwa atakuwa pamoja nao wakati wote hadi mwisho wa dahari. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
3 minutes 26 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-9. Vitu Vyote Vinafanya Kazi Pamoja Kwa Ajili ya Mema (Warumi 8:28-30)
Leo, hebu tukiangalie kifungu hicho hapo juu kinachotoka katika Warumi sura ya 8. Kifungu kinasema kuwa Mungu alituchagua tangu asili, alituita, na akatutukuza sisi tulio katika Yesu Kristo Mwana wa Mungu. Tutazungumzia juu ya hili na jinsi watu wanavyolielewa Fundisho la Utakazo Unaozidi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
35 minutes 44 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-10. Mafundisho ya Kidini Yenye Makosa (Warumi 8:29-30)
Vifungu hivyo vinatueleza sisi kuwa Mungu alichagua tangu asili ili kuwaokoa watu katika Yesu Kristo. Ili kufanya hivyo, Mungu amewaita wao katika Kristo, amewahesabia haki wale aliowaita, na amewatukuza wale aliowahesabia haki. Misingi yote ya maandiko imepangwa na kutekelezwa kwa kupitia Yesu Kristo. Hivi ndivyo kitabu cha Warumi kinavyotueleza, lakini wanatheolojia wengi na watumishi wa uongo wameubadilisha ukweli huu ulio wa wazi kuwa katika fundisho la kawaida la dini hali likiwa na mawazo na matakwa yao binafsi na wanalieneza fundisho hilo kwa nguvu. Sasa tunageukia kuchunguza jinsi watu wengi wanavyouelewa vibaya ukweli huu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
30 minutes 5 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-11. Upendo wa Milele (Warumi 8:31-34)
Ikiwa Mungu alikwisha amua kutufunika sisi kwa haki yake katika Yesu Kristo hata kabla ya uumbaji, basi hakuna mtu anayeweza kusumbua na kuharibu mpango huo. Kwa kuamini katika haki ya Mungu, na wala si kwa kupitia katika Fundisho la Kuhesabiwa Haki kwa Imani, basi wale ambao wamekuwa hawana dhambi kiuhakika ndio watoto wa kweli wa Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
5 minutes 4 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-12. Ni Nani Anayeweza Kudiriki Kusimama Kinyume Nasi? (Warumi 8:31-34)
Katika Warumi 8:31-34, Paulo anashuhudia juu ya upendo wa Kristo usioweza kutenganishwa na waamini kwa kufanya majumlisho ya injili ya maji na Roho na kisha kufikia hitimisho lake la mwisho. Kifungu hiki kinaelezea furaha kuu ya wokovu ambayo imefikiwa katika kiwango cha juu cha imani. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
37 minutes 11 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 8-13. Ni Nani Atakayewatenga Wenye Haki na Upendo wa Kristo? (Warumi 8:35-39)
Aya ya 35 inasema, “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?” Ni nani anayeweza kututenga na upendo wa Kristo uliotolewa kwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho ambayo ina haki ya Mungu ndani yake? Je, mateso na matatizo vinaweza kutukata toka katika upendo huo? Je, yale mapigo makuu ya miaka saba yanaweza kututenga na upendo huo wa Yesu? Kwa kweli hapana! https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
36 minutes 42 seconds

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
SURA YA 9-1. Utangulizi Kwa Sura ya 9
Kwa nini Paulo alisema kuwa anahuzuni sana na uchungu unaoendelea katika moyo wake kwa ajili ya watu wake? Ni kwa sababu Paulo alikuwa ana kitu anachokitaka kwa ajili ya ndugu zake, na ndio maana alikuwa radhi kulaaniwa na kukatwa toka katika Kristo kwa ajili yao. Kwa mujibu wa mwili wake, Paulo alipenda sana kwamba watu wake waweze kuokolewa. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Show more...
2 years ago
32 minutes 52 seconds