Katika kipindi cha "Get Visible with Lucia", tunaangazia ulimwengu wa kutokuonekana hata tunapojitahidi sana. Katika kipindi hiki, nitakujulisha sababu tatu ambazo zinaweza kufanya jitihada zako za kuonekana zisifanikiwe.
Sababu ya kwanza ni kutokuwa na mkakati madhubuti. Mara nyingi tunajikuta tukifanya vitu bila mpangilio wa kina au dira, hali ambayo inaweza kusababisha kutofaulu kuonekana.
Sababu ya pili ni kukosa kuweka malengo ya wazi na kufuatilia maendeleo yetu. Bila malengo thabiti na njia za kufuatilia matokeo, inakuwa vigumu kujua ikiwa tunaelekea kwenye lengo letu au la.
Sababu ya tatu ni kukosa kuwa na mtandao wa kijamii au msaada wa kutosha. Kuwa na watu wanaokusaidia na kukusapoti katika safari yako ya kuonekana ni muhimu sana.
Kupitia mjadala wa kina, nitakupa njia za kukabiliana na changamoto hizi na kujinasua kutoka kwenye hali ya kutokuonekana. Usiache kusikiliza ili upate mwanga katika safari yako ya kuonekana na kufanikiwa.
Karibu kwenye Ukurasa wa Kwanza wa Get Visible with Lucia
Kwenye ukurasa huu utapata majibu ya kila swali lako kuhusu podcast ya Get Visible with Lucia
Bila shaka utapata kufahamu kidogo kuhusu muongozaji wa podcast hii, Lucia, atakusafirisha kuelekea uwanja mpana wa kujenga jina, ujasiri na kuelewa Uhalisia wako.
Tutazama kwa karibu maisha yetu na jinsi tunavyoweza kutumia tofauti zetu kama nguvu kwetu.
Kama mwanzo wa safari yoyote ile, hii ni nafasi ya kugundua na kuelewa kwa kina zaidi jinsi ya 'Kuonekana' yani Visibility "na kuuishi uwezo na uhalisia wako.
Jiunge nasi kwenye mazungumzo haya yenye kusisimua na hatua ya kwanza kuelekea utambulisho wako bora!
Usisahau kutufuata kwenye mitandao ya kijamii kwa habari zaidi na mazungumzo mazuri.
Tembelea ukurasa wetu wa @GetVisible with Lucia kwenye Instagram na Facebook.
Link: https://www.instagram.com/getvisiblewithlucia_?igsh=MWk2d21oeHFqdWFzaw%3D%3D&utm_source=qr
Karibu, rafiki!
Asante kwa kuchagua 'Get Visible with Lucia!' Jiandae kufungua uwezo wako kamili, Mimi ni Lucia Mwashala, mwongozaji wako, rafiki yako wa karibu, na your Digital supporter. Jiandae kung'aa!