Katika episode hii ya saba cha TEN OVER TEN Podcast, tunazungumzia mada ya kuchochea fikra na vitendo: Ubunifu na Kujiajiri. Katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi, ubunifu ni silaha ya kufanikisha ndoto na kutengeneza nafasi mpya za ajira. Tukiongozwa na Jackson na Kefa Victor, Pamoja na mgeni Mr Saad tunachambua kwa kina:
- Umuhimu wa ubunifu katika soko la kisasa la kazi na biashara.
- Fursa zilizopo kwa wale wanaotaka kujiajiri na jinsi ya kuzitumia.
- Changamoto zinazowakumba vijana na mbinu za kuzikabili.
- Jinsi teknolojia inavyoweza kuwa chombo kikuu cha ubunifu na ajira.
- Njia za kukuza biashara za kibunifu na nafasi ya serikali katika kusaidia wabunifu.