Neno "Gnosis" hurejelea ujuzi tunaopata kupitia uzoefu (experience) wetu wenyewe, lakini pia si sawa na ujuzi ambao tunaambiwa au kuamini. Gnosis - kwa jina lolote katika historia au utamaduni - ni maarifa, uzoefu, si ujuzi wa kiakili au dhana tu, imani, au nadharia. Neno hili ni sawa na neno la Kiebrania "Daath" na la Sanskrit "Jna."
All content for Tanzania Gnosis's podcast is the property of Tanzania Gnosis and is served directly from their servers
with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Neno "Gnosis" hurejelea ujuzi tunaopata kupitia uzoefu (experience) wetu wenyewe, lakini pia si sawa na ujuzi ambao tunaambiwa au kuamini. Gnosis - kwa jina lolote katika historia au utamaduni - ni maarifa, uzoefu, si ujuzi wa kiakili au dhana tu, imani, au nadharia. Neno hili ni sawa na neno la Kiebrania "Daath" na la Sanskrit "Jna."
Mti wa ujuzi ni elimu ya kiroho inayohusiana na nafsi ya mwanadamu. Mwili wa mwanadamu ni chombo kinachobeba nafsi na roho hivyo hatuwi na miili kana kwamba haina cha kufanya ambacho kinahusiana na ukombozi wa nafsi zetu.
Kumekuwa mkanganyiko wa mafundisho juu ya elimu nzima inayohusiana na bustani ya Eden pamoja na mwanaume na mwanamke yaani Adam na Eva ndani ya bustani. Vizazi vilivyotangulia vilikuwa na uhodari wa kuficha maarifa kwa maana si kitu ambacho kila akipataye hukitumia kwa mtizamo chanya. Ni watu wachache sana waliochaguliwa ambao waliweza kupana nafasi ya kujifunza. Kwa kipindi kirefu sana kilichopita, maarifa haya yalifundishwa kwa wachache lakini nyakati zimefika, maarifa kufundishwa kwa kizazi hiki cha sasa.
Maarifa ama ujuzi ni neno "Da'ath דעת" kwa Kiebrabia. Neno hili "Da'ath דעת" ni muunganiko wa herufi za Kiebrania tatu: Daleth ד, Ayin na Tav ת. Pia, zingatia kwamba maneno ya lugha ya Kiebrania husomwa kuanzia upande wa kuume (kulia) kuelekea kushoto.
Karibu sana darasani.
Tanzania Gnosis's podcast