Neno "Gnosis" hurejelea ujuzi tunaopata kupitia uzoefu (experience) wetu wenyewe, lakini pia si sawa na ujuzi ambao tunaambiwa au kuamini. Gnosis - kwa jina lolote katika historia au utamaduni - ni maarifa, uzoefu, si ujuzi wa kiakili au dhana tu, imani, au nadharia. Neno hili ni sawa na neno la Kiebrania "Daath" na la Sanskrit "Jna."
All content for Tanzania Gnosis's podcast is the property of Tanzania Gnosis and is served directly from their servers
with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Neno "Gnosis" hurejelea ujuzi tunaopata kupitia uzoefu (experience) wetu wenyewe, lakini pia si sawa na ujuzi ambao tunaambiwa au kuamini. Gnosis - kwa jina lolote katika historia au utamaduni - ni maarifa, uzoefu, si ujuzi wa kiakili au dhana tu, imani, au nadharia. Neno hili ni sawa na neno la Kiebrania "Daath" na la Sanskrit "Jna."
Gnosis siyo dini kana kwamba watu wake ni wa kutafuta kukusanya watu na kuanzisha nyumba za ibada. Gnosis ni maatifa ya ndani ambayo huambatana na juhudi katika natendo hata kupata matokeo chanya. Wana-gnosis tunaheshimu dini zote maana tunapotizama mafundisho yake tunakuta ni kivuli ya majukumu ambayo kila mwana-gnosis hupaswa kupitia yaani njia yenyewe ya kuelekea nuruni. Njia ya Gnosis haijihusishi na kunyoshea watu vidole wala hatujikwezi ya kwamba sisi ni bora kuliko yeyote. Tunatambua jukumu la kubadilika sisi kwanza ili wengine nao wabadilike na siyo kupambana kuona mabovu ya wengine huku ya kwetu hatuyaoni. Kila mwana-gnosis huipita njia ya maarifa hatua kwa hatua, kupanda na kushuka hata kuufikia ukamilifu. Pamoja na kwamba mwana-gnosis atafikia kizio cha juu ya utimilifu, hakupo kujikweza kusema kwamba yeye ni bora kuliko fulani. Vilevile ni siri ya mtu kusema kizio alichofikia kwa maana kizio afikiacho mtu ni ya ndani yake na wala hakihusiani na mwili huu wa uharibifu. Ndiyo maana tunajifunza maarifa ya ndani ambayo hayahusiani kabisa na maarifa ya akili (intellectual mind).
Utajifunza maarifa yatokanayo na utu wa ndani kwa faida za nafsi yako. Kwa maana ni muhimu sana kuyafahamu maarifa ya ndani yako na mengine yote huja kama mshahara wa ufahamu wako juu ya Muumba aliye ndani yako. Maarifa haya siyo yale yaliyozoeleka yaani ya mwili ama ya kiakili, la hasha. Pamoja na yoye, ni kwamba tunatumia mwili kama ni mlango wa kutupitisha kule tuendako kwa maana tupo kwenye miili kwa kusudi maalumu.
Tanzania Gnosis's podcast