Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Society & Culture
Business
Sports
History
Fiction
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts115/v4/fd/ee/1a/fdee1afb-232c-158d-f728-70b489183e66/mza_8350944664688333027.jpg/600x600bb.jpg
Sheria Poa Podcast
Privaty Rugambwa
18 episodes
1 day ago
Sheria Poa, ni kipindi ambacho tunaongelea maswala mbalimbali ya jamii kwa mtazamo wa sheria na kwa lugha nyepesi kabisa na ya kiurafiki, ni kipindi cha kufundisha na kusaidia kwa watu wa aina zote.
Show more...
Education
RSS
All content for Sheria Poa Podcast is the property of Privaty Rugambwa and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Sheria Poa, ni kipindi ambacho tunaongelea maswala mbalimbali ya jamii kwa mtazamo wa sheria na kwa lugha nyepesi kabisa na ya kiurafiki, ni kipindi cha kufundisha na kusaidia kwa watu wa aina zote.
Show more...
Education
https://d3t3ozftmdmh3i.cloudfront.net/production/podcast_uploaded_nologo/13276231/13276231-1626169007566-7d2545020ee0a.jpg
Matumizi ya lugha ya kiswahili kwenye mfumo wa utoaji haki; Nini ni faida kwa wadau wa mahakama na mfumo mzima wa sheria.
Sheria Poa Podcast
32 minutes 33 seconds
4 years ago
Matumizi ya lugha ya kiswahili kwenye mfumo wa utoaji haki; Nini ni faida kwa wadau wa mahakama na mfumo mzima wa sheria.

Kiswahili ni Lugha ya Taifa na Matumizi ya Kiswahili yanazidi kukua kadri siku zinavyozidi kwenda, pamoja na kukua kwa lugha hii, Kiswahili kimekuwa hakitumiki katika mfumo mzima wa utoaji haki, kwa maana ya kwamba sheria zote za nchi yetu bado zipo kwa lugha ya Kiingereza na hata Mahakama zetu kuanzia ngazi ya Mahakama ya wilaya mpaka Mahakama ya rufani, lugha inayotumika ni Kiingereza. Kitu ambacho kimekuwa ni changamoto kwenye shughuli mbali mbali za utoaji haki.

Lugha ya Kiswahili nchini imekuwa ikitumika kwenye mabaraza yote na Mahakama zote za Mwanzo tangu mwaka 1985 kwenye kuendesha mashauri na kutunza kumbukumbu zote, lakini kwenye mahakama za wilaya mpaka mahakama ya rufani, lugha ya kiswahili imekuwa ikutumika kuendesha mashauri laikini kumbukumbu zote za mahakama zimekuwa zikiandikwa kwa Kiingereza.

Serikali kupitia Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, wamepetisha mswada wa mabadiliko ya sheria (Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill of 2021 (Muswada), kupendekeza sheria zote za Tanzania Bara kuwa kwa Lugha ya Kiswahili; Hivyo basi katika kipindi hiki tunajadili kiundani ni nini dhumuni kuu la Serikali katika kuleta mapendekezo haya na ni nini zitakuwa changamoto za mabadiliko hayo, kama wanasheria na maafisa wa mahakama ni nini kingine cha ziada kinaweza kufanyika katika kuhakikisha lugha hii yetu adhimu inakuwa na kuendelea kutumika.