Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Society & Culture
Business
News
Sports
TV & Film
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts122/v4/51/12/24/51122459-f996-27cb-eb57-0f2cc44385ec/mza_12815542714360086249.jpg/600x600bb.jpg
Salama Na
Salama Na
93 episodes
1 week ago
‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society.
Show more...
Entertainment News
News
RSS
All content for Salama Na is the property of Salama Na and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society.
Show more...
Entertainment News
News
https://d3t3ozftmdmh3i.cloudfront.net/production/podcast_uploaded_episode/2608782/2608782-1669837975348-fda2faeb5f95e.jpg
SE7EP24 - SALAMA NA LULU DIVA | UKIPATA KINYAKUE
Salama Na
1 hour 15 minutes 15 seconds
2 years ago
SE7EP24 - SALAMA NA LULU DIVA | UKIPATA KINYAKUE

Kuna mambo mengi wakati mwengine ambayo yanakua yanaendelea au yalitokea kwenye maisha ya baadhi ya watu ambao huja kukaa kwenye kiti chetu chakavu na meza yenye kigae. Ila kwasababu zilizo wazi za kuwataka wasijisikie uncomfortable na pengine kuwafanya hata ambao wangependa au ambao tungependa waje nao wasijiskie hivyo ndo kanuni ambayo tumeamua au niseme niliamua kipindi huko nyuma kuifuata. Nia na madhumuni ya session zetu hizi zaidi ni kuwapa watu maua yao wakiwa hai, sisi nasi kuskiliza hadithi za maisha yao ambazo zitatupeleka sehemu fulani katika maisha yatu na hili pia humuambia kila mgeni anapokalia tu kiti chetu chakavu kabla hata camera hajiwashwa ya kwamba… Sisi tuko hapa kwaajili ya kutaka ku inspire zaidi na si kumdhalilisha au kutaka kumuangalia kwa chini yoyote kwasababu tu kabla kuna kwikwi kadhaa zilishawahi kutokea kwenye maisha yake na tuka tumia hiyo kama ‘fimbo’ kumchapia nayo. Kama mwenyewe ana simulizi yake ya ‘majuto’ ambayo wengi wanaifahamu na haikumueka sehemu nzuri na angependa kuiongelea basi ruhusa ipo, ila kama ni kitu ambacho mwenyewe hayuko tayari kukiongelea basi kuheshimu hilo ni jukumu letu NAMBARI MOJA. Najua pengine inawezakana kabisa ukaona ah basi kuna haja gani ya kuongea nao then? Haja ipo na naamini tukipatacho hutosha, bila ya kuvunjiana heshima au kuwekana uncomfortable. Ukikua zaidi utaelewa zaidi 😄.

Lulu Diva ni moja ya majina makubwa kwenye muziki wetu hapa nyumbani na pia kwenye kiwanda cha uigizaji, hustle zake za spidi KUBWA ndo ambazo zimemfanya awe anatambulika na mambo mengine kuweza kwenda vizuri kama jahazi kwenye hali ya hewa shwari huko baharini. Ila hayo yote hayakuja tu kwasababu labda yeye ni maalum sana, au mzuri sana au anajua kuimba sana, kiukweli wake, haya yamekuja baada ya jasho tele, mchozi tele na pengine damu kiduchu.

Jinsi alivyokua ilikua kwa malezi ya Bibi maana Mzee wake alikua na mambo mengi, Mama yake nae alikua akimpambania goli kama wengi ambavyo wamekua wakifanya kwa watoto wao. Kukua kwake kwa kiasi kikubwa ni Tanga na ananisimulia kwenye apisode hii jinsi ambavyo alikua akihama vijumba na maamuzi magumu ambayo aliyafanya yeye na Marehemu Mama yake ya yeye kuja TOWN. Lulu ananihadithia pia jinsi alivyokua akijituma ili aweza kumleta Mama yake mjini baada ya kuskia ameanguka kwa mara ya kwanza. Ni binti tu ambaye ndoto yake ilikua ni kuishi na Mama yake mzazi ambaye maisha hayakua hivyo wakati anakua. Ilikua inambidi afanye mambo kadhaa mpaka alipoweza kutimiza ndoto yake hiyo ya kumleta Bi Mkubwa hospitali kwa mara ya kwanza. Mengi yalitokea na ambayo yalikua nje ya uwezo wake ila kwa Rehema za Mwenyezi Mungu kadhaa aliweza kuyakamilisha ambayo kwa mujibu wa simulizi zake naamini Mama ametangulia mbele ya Haki akiwa na roho safi kwa Binti yake.

Story ya Mama Lulu ndo ambayo kwa kiasi kikubwa ilibeba mazungumzo yetu haya, ingawa pia kwa ki upekee kabisa tumeweza kuzungumzia mahusiano yake, kazi zake, ndugu zake, maisha nyuma ya camera , kazi zake, uandishi, muziki na filamu na hakua mchoyo wa kujielezea na kutuelezea hata kidogo. Yangu matumaini pia nawe utaskiliza na kuitimaza kwa MAKINI na kwa kiasi fulani utaweza kuelewa baadhi ya mambo ambayo yatakufanya hata ukimuona uwe na heshima fulani kwa Binti huyu.

Tafadhali Enjoy.

Love,

Salama.

Salama Na
‘Salama na’ – meaning ‘Salama and’ is a one hour Podcast chat show hosted by a re known Radio &; TV personality Salama Jabir and available on Both Video and Audio of Various Platforms. In Salama na, Salama gets to sit down for exclusive chats with Celebrities, Influencers and Change makers in the society.