Utunzaji wa mazingira umekua changamoto kubwa sana kote ulimwenguni kwani mabadiliko ya hali ya hewa imeathiri vigezo vingi katika jamii ikiwemo afya, hewa safi, maji safi ya kunywa,chakula na makazi salama.
Kufuatia hali hio wanafunzi katika shule ya Salex Transition Academy iliyoko eneo la Mtongwe kaunti ya Mombasa wamejitosa katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi,kwa kutumia mbinu ya kubadilishana chupa za plastiki kwa sodo,miti na vifaa vingine vya masomo.
Fatuma Hamisi mwenye umri wa miaka 13 ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Salex Transition Academy.Yeye ni mwanafunzi wa gredi ya 6 na pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira katika shule hiyo.
Mwandishi:Athuman Luchi
Licha ya idadi ya wanawake katika taalum ya teknologia kuwa ndogo ikilinganishwa na idadi ya wanaume, wanawake wameonekana kupambana ili kukabiliana na tofauti hiyo.
Ripoti kutoka benki kuu ya dunia inaonyesha kuwa wanawake wako chini ya thuluthi moja ya wafanyikazi ulimwenguni katika nyanja zinazohusiana na teknolojia.
Ambapo wanashikilia asilimia 28 ya kazi zote za kompyuta na hisabati, na asilimia15.9 ya kazi za uhandisi na usanifu
Mwandishi:Nuru Mwalimu
Makala haya yanazungumzia kuhusu uchafuzi wa bahari hasa katika eneo la Mbuyuni-Mji wa Kale kaunti ya Mombasa.
Eneo hilo limeathirika na maji taka yanayotoka katika nyumba zinazopakana na ufuo wa bahari.Makala haya yametayarishwa na Ruth Keah.
17-year-old Jane is among the children with mental disabilities who were molested and impregnated. Jane is currently raising a three-month-old baby boy.
By Rose Tawa.
Mabadiliko ya Tabia Nchi yameathiri sana wakulima na wafugaji hatua inayo wafanya wengi kukumbwa na tatizo la afya ya Akili.Kufuatia hatua hio sasa baadhi ya wakulima wanajizatiti kukabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na mabadiliko hayo.Sasa wakulima hao,wamejitosa katika ufugaji wa nyuki na vipepeo,huku wengine wakifanya biashara ndogo ndogo za kukimu mahitaji ya familia.
Athuman Luchi,ametuandalia makala hayo aliyoyapa jina la Wakulima Wanavyokabiliana na Afya ya Akili Inayosababishwa na Climate Change
Makala haya yanazungumzia kuhusu hatua ambazo zimepigwa na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa dhulma za mtandaoni zinaripotiwa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria. Yametayarishwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu ujangili unaofanyiwa viumbe vya baharini. Yametayarishwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu mbinu ya Rangi ambayo wanabodaboda kaunti ya Mombasa wanatumia kutofautisha sehemu wanazohudumu kama njia moja ya kukabiliana na visa vya uhalifu. Makala yametayarishwa na Ruth Keah.
Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi za mashirika mbalimbali ambayo yamekuja pamoja kukabiliana na uvuvi wa kutumia mbinu haramu katika eneo la Shimoni Kwale. Yametayarishwa na Ruth Keah.
Ukataji wa miti kiholela umesababisha mabadiliko ya tabianchi,kiangazi,mmomonyoko wa udongo,mafuriko na ongezeko la hewa chafu hatua inayochangia athari mbali mbali kwa jamii.
Kufuatia mabadiliko hayo ya tabia nchi,sasa jamii imejitokeza kuja na mbinu mbali mbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Makundi ya wanawake na vijana katika kaunti ya kwale yanaendeleza mpango wa upanzi wa miti,walioupa jina la Mti wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika kila boma.
By Rose Tawa.
Makala haya yanazungumzia kuhusu jamii ilivyoungana kulinda mazingira hasa mikoko katika eneo la Mida Creek Dabaso. Hatua iliyowafanya kujenga mkahawa juu juu ya mikoko na kwasasa mkahawa huo umekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka humu nchini na hata nje ya nchi. Mtayarishi ni Ruth Keah.
Mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kuathiri kila mtu kila siku,kufuatia hayo watu wenye ulemavu wamejikita katika mbinu mbali mbali za kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi jijini Mombasa.Mwanahabri wetu Nuru Mwalimu ametuandalia makala yanayosimulia juhudi za watu wenye ulemavu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Makala haya yanazungumzia kuhusu juhudi mbalimbali ambazo wanahabari wa Radio wanafanya kuhakikisha kuwa habari wanazopeperusha hewani ni za uhakika. Yametayarishwa na Ruth Keah