
Kama ulishawahi kuisikia ile story ya mtangazaji wa kwanza kucheza wimbo wa Bongo Fleva kwenye radio. Mtangazaji huyo, leo amepata nafasi ya kutubariki na historia yake. Jinsi alivyochangia muziki huu kuwa kimbilio la vijana wengi sana kama sehemu ya ajira yao.
Jina lake kamili ni Taji George Liundi au MASTER T kama alivyobatizwa na Charles Hillary. Kuanzia alivyoanza kutangaza Redio One, moja ya vipindi vyake vya awali kabisa cha DJ Show, kabla ya kuwaachia mikoba wakina Mike Mhagama baada ya kuikacha Redio one na kwenda kufanya kazi kwenye media zingine.
Karibu mezani umfahamu zaidi.