
Dr. Lwidiko Mhamilawa ameibuka kwenye studio zetu siyo kwa ajili ya kutuambia jinsi maisha ni magumu (tulishajua hiyo), bali kutufundisha jinsi ya kufurahia safari ya maisha – hata pale unapotaka kutupa lapa na kusema, “Inatosha!”
Unajua, kuwa mwanaume ni kama kuwa kocha wa timu isiyoelewa mchezo: kila mtu anakutegemea wewe, lakini hakuna anayekuelewa! 😂 Maisha yanakuhitaji utafute hela, ulee watoto, ujenge nyumba (na siyo ya mbwa), huku ukifanya yote haya kwa tabasamu la Kimasai.
Lakini badala ya kulalamika juu ya maisha haya mazito, Dr. Lwidiko anatufundisha siri moja kuu: Kupenda mchakato wenyewe. Swali la kitofauti linakuja – Je, unafurahia kuwa mwanaume, au unaishi kwa survival mode tu?
Kwa usaidizi waMichael na Nadia, tunazungumzia pia umuhimu wa kushukuru na kushangilia mafanikio madogo madogo. Kwani, kama unaweza kusherehekea unapoipata *“charge” ya simu kwa 1%, kwa nini usifurahia hatua zako ndogo za maisha? 😂
Hii siyo tu episode, ni therapy session yenye jokes, insights, na motisha ya kuendelea kuwa mwanaume mwenye maana – bila kusahau furaha. Usikose hii safari ya kuelewa maana ya kuwa mwanaume!
Kumbuka, maisha ni safari – lakini angalau unaweza kucheka njiani. 😎