
Katika jamii inayomtazama mwanaume kama mhimili wa familia na mtafutaji mkuu wa riziki, changamoto za kiuchumi zimewasukuma wengi kutafuta njia mbadala za kujikimu. Moja ya njia hizo ni kamari.
Lakini je, kamari ni suluhisho la kweli kwa changamoto za kiuchumi, au ni mtego mwingine unaozidi kudidimiza maisha ya wanaume wengi?
Katika episode hii, tunachambua kwa kina ongezeko la michezo ya kubahatisha miongoni mwa wanaume wa Kitanzania. Tunaangazia sababu, athari, na uhalisia wa maisha yao baada ya kuingia katika mzunguko wa kamari.
Tupo na Tumaini Maligana, mshauri wa michezo ya kubahatisha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 10, ambaye anatuongoza katika mjadala huu kwa maarifa, ushuhuda, na maonyo yenye msingi wa uhalisia wa maisha.
Karibu usikilize, tafakari, na shiriki.
#MenMenMenPodcast #KamariNaMaisha #ChangamotoZaMwanaume #UkweliWaKamari