All content for KaBrazen is the property of The LAM Sisterhood and is served directly from their servers
with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Ardhi kuibwa, ndimi zenye sumu na safari ya kishujaa!
Katika kipindi hiki cha KaBrazen, Tata Nduta anasimulia hadithi murua inayohusu msichana aliyeota juu ya uhuru wa kweli. Katika ulimwengu wa kutisha ambapo vyura wasio na rangi wala nyoyo wamenyakua ardhi na hata kubadili nyoyo za watu wake, Muthoni mdogo kamwe hakati tamaa. Muthoni anatukumbusha kwamba hatua kwa hatua, hata sisi tunaweza kufikia uhuru wa kweli kwa kutokata tamaa katika kutimiza ndoto zako.
Zingatia kwa makini: Kupigwa shoti ya umeme kunatajwa na pia dhuluma ya kimwili dhidi ya mtoto.