
Kwa maelfu ya miaka sasa, Wairani wamekuwa wakisherehekea usiku wa mwisho wa msimu wa mapukutiko (maarufu kama Shabe Yalda) kwa kutekeleza mila na desturi katika miji mbalimbali nchini Iran, usiku unaotajwa kuwa ni mrefu zaidi wa mwaka na wenye giza nene mno.
Historia inaeleza kuwa, sherehe ya usiku wa Yalda ilianza zama za kale mno, na wala haifahamiki ni muda gani hasa ilipoanza, lakini wanaakiolojia walio wengi wanaeleza kuwa, usiku huo ulianza yapata miaka elfu saba iliyopita. Happy Shabe Yalda