Home
Categories
EXPLORE
True Crime
Comedy
Society & Culture
Business
Sports
TV & Film
Health & Fitness
About Us
Contact Us
Copyright
© 2024 PodJoint
00:00 / 00:00
Sign in

or

Don't have an account?
Sign up
Forgot password
https://is1-ssl.mzstatic.com/image/thumb/Podcasts115/v4/96/f3/75/96f375be-cda2-e83c-df72-2c8843220004/mza_11164014232092982709.jpg/600x600bb.jpg
Iran-Tanzania Podcast
Iran.Tanzania
12 episodes
1 week ago
Audio za Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Show more...
Society & Culture
RSS
All content for Iran-Tanzania Podcast is the property of Iran.Tanzania and is served directly from their servers with no modification, redirects, or rehosting. The podcast is not affiliated with or endorsed by Podjoint in any way.
Audio za Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Show more...
Society & Culture
https://d3t3ozftmdmh3i.cloudfront.net/production/podcast_uploaded_episode/15301747/15301747-1650273052912-749362f597a9d.jpg
ATTAR NEYSHABURI MALENGA WA KIIRANI
Iran-Tanzania Podcast
7 minutes 16 seconds
3 years ago
ATTAR NEYSHABURI MALENGA WA KIIRANI

ATTAR  NEYSHABURI  MALENGA WA KIIRANI

 

Tarehe 25 Farvardin kwa mujibu wa ( Kalenda ya Kiirani) inayosadifiana na tarehe 14 Aprili,  ni siku ya  kumkumbuka na kumuadhimisha malenga wa Kiirani Farid al-Din Abu Hamid Muhammad bin Abu Bakr Ibrahim bin Is- haq Attar Neyshabouri, ambaye ni mmoja wa washairi mashuhuri, aaref na mwanafikra mkubwa wa Kiirani aliyeishi  mwishoni mwa karne ya sita na mwanzoni mwa karne ya saba Hijria. Baadhi ya wanahistoria wameandika kuwa, mwanafikra na malenga huyo wa Kiajemi amezaliwa mwaka  513 na wengine wanaeleza kuwa alizaliwa mwaka 537 Hijiria. 

Attar Neyshabouri alizaliwa katika kijiji cha Kadkan au Shadiakh, ambacho wakati huo kilikuwa sehemu ya jiji la Neyshabour. Hakuna habari inayoelezea taarifa zake za utotoni mwake, isipokuwa baba yake aliishi katika mji wa Shadiakh  akifanya kazi ya kuuza dawa za asili,  na alikuwa mahiri na hodari mno katika biashara hii ya kuuza dawa za asili, na baada ya kufariki dunia baba yake, Farid al Din Attar Neyshabouri  aliendeleza shughuli za marehemu  baba yake ya kuuza dawa  za asili. Wakati akishughulika na uuzaji wa dawa za asili Attar Neyshabouri alikuwa akitoa tiba ya asili na wala haijulikani utaalamu huo  wa kutoa tiba ya asilii aliupata kutoka kwa nani. Attar Neyshabouri aliendelea na shughuli zake za kutoa tiba ya asili sanjari na kuuza dawa za asili hadi pale yalipopatikana mapinduzi ya kiroho na kimaanawi kwa upande wake, na jambo  hili limebainishwa kwa kutolewa visa kadhaa, lakini kisa maarufu ni hiki kifuatacho:

 “Siku moja Attar Neyshabouri alikuwa dukani kwake akifanya shughuli zake, mara akaingia “Darwesh" na akaanza kusema maneno kadhaa yanayohusiana na Mwenyezi Mungu, ili Attar aweze kuvutika na  kumsaidia, lakini Darwesh hakupata msaada wowote kutoka kwa Attar Neyshabouri. Darwesh akamwambia Attar : Ewe kijana unataka ufariki duniani  kwa kifo cha namna gani? Attar akajibu: Kwa njia ileile ambayo wewe unataka kufa. Darwesh akasema; Wewe unataka kufa kama nitakavyokufa mimi? Attar akajibu: Ndio, Darwesh akachukua bakuli lake lililotengenezwa kwa mbao na kuliweka chini ya kichwa chake na akasema maneno ya Mwenyezi Mungu na hatimaye  kufariki dunia. Kwa vile Attar Neyshabouri aliliona tukio hilo kwa macho yake aliathirika mno na kubadilika na akaamua kutoka dukani na kubadilisha kikamilifu mtindo na  mwenendo wa maisha yake” .

Attar Neyshabouri aliposhuhudia tukio hilo la Darwesh , akaacha kabisa shughuli za tiba na biashara za dawa za asili, na akaamua kuelekea kwa Sheikh Mkuu Aref Rukniddin Akaf , wakati huo Sheikh Aref alikuwa mtu maarufu na mashuhuri mno na kwa miaka kadhaa Attar Neyshabouri alikuwa akipata elimu na maarifa  kutoka kwa sheikh Aref Rukniddin Akaf. 

Attaf Neyshabouri aliweza kutumia nusu ya umri wake kwa kufanya safari katika miji mbalimbali, na katika safari zake hizo alifanikiwa kukutana na masheikh wakubwa wakubwa katika zama hizo, na safari hizo ziliweza kumfikisha hadi kwa sheikh Majiduddin Baghdadi. 

Inasemekana kuwa Sheikh Aref alipofikia marika ya uzee, Bahauddin Muhammad baba wa Jalaluddin Balkhi alikuwa pamoja na mwanawe walifanya safari ya kuelekea Iraq , wakiwa njiani walipitia Neyshabouri na wakafanikiwa kumtembelea Attar Neyshabouri, hivyo Sheikh Attar Neyshabouri alitoa nakala moja kati ya makala zake za mashairi na kumpa Jalaluddin ambapo wakati huo alikuwa bado kijana mdogo mno.


Iran-Tanzania Podcast
Audio za Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran